Tuesday, December 29, 2009

Nawaza kwa sauti......Niwazue

Picha toka www.ica.org.uk
Desemba 20 mwaka jana niliuliza swali kuwa Ni kweli sote tu-wabinafsi? (Jiulize hapa) na ninaendelea kujiuliza swali katika nyanja na maisha ya aina mbalimbali.
Leo nimewaza kuwa ikiwa mtu ataamua kuoa na kuchangisha michango ya harusi, lakini unachangia bila kuandika mahala popote kuwa ulitoa kiasi fulani, unadhani ni wangapi watatoa kiasi kama ambacho wangetoa iwapo wangewekwa kwenye kumbukumbu ya waliochangia harusi hiyo?
Ama je! Ikitokea muoaji akaomba mchango wa harusi lakini akaomba harusi isiwe na sherehe ili pesa mtakayochanga iwasaidie kuanzia maisha, ni wangapi wangekubaliana na wazo hilo?
Ni kweli twafanya tuyafanyayo kwa kuwa tunapenda kuyafanya ama twafanya kwa kuwa yanatunufaisha na kuturidhisha kwa namna fulani?
Ndio maana narejea kulekuleeee nilikowahi kusimulia kuwa Tunajidanganya wenyewe kudhani tunawajali wenzgine.(Bofya hapa kujikumbusha)

Nawatakia mwanzo mwema wa mwisho salama wa mwaka.

Blessings

2 comments:

Simon Kitururu said...

Katika hili jibu langu liko kimya wakati nakiri ujumbe umenifikia kwa sauti.:-(

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

nimeoa / funga ndoa /fanya shoo ya ndoa juzi tu.

sikutaka michango wala mamilioni ili tunywe na kula siku moja! that being the case, watu lukuki wa familia walinigomea kuhudhuria na haikuzuia kitu.

nilifanya ndoa iliyonigharimu kama shs laki nne tu!
tatizo ukitaka kuoa na kuwaambia watu kama wazazi wanaanza kusheherekea ndoa zao badala ya yakwako na ndio maana wataanza kuchangisha eti kwa sababu tu nawao huchangishwa na wengine kwahiyo wanarudisha pesa zao!

mimi silijali hilo na sikutaka ndoa yangu iwe ya mwingine isipokuwa mimi. kwa wnaotaka labda wanaweza kuona mkanda wa DVD simple wedding

unaweza kujiuliza maswali mengi juu ya ndoa hizi. kwamba ndoa bila pombe itakuwaje nk, nk japo yangu haikuwa na pombe wala Nyama!!!!