Sunday, December 27, 2009

Kinachoua soko la kazi za wasanii wetu

Oktoba 8 2008, niliandika kuhusu tasnia ya filamu na zaidi kuhusu filamu iliyokuwa ikitegemewa kutoka ambapo nilisema Filamu ya Richmond yaja: Naanza kuhisi vitakavyonikera (Bofya hapa kuisoma) na hata kabla ya hapo, niliandika kuhusu muziki wa kiTanzania nikiuliza Ni kipi tulichopoteza kwenye muziki wetu kisichorejesheka? (Bofya hapa) na kwa ujumla niliongelea kinachopotosha sanaa nzima ya muziki na filamu nchini
Najijua kuwa si mtaalamu MKOSOAJI wa filamu na muziki lakini kinachonisikitisha zaidi ni kuwa hauhitaji kuwa na utaalamu wowote wa sanaa hizi kuona UOZO uliopo ndani yake.
Kila siku nasoma kuhusu "mzigo wa nguvu" ama "albamu iliyo moto wa kuotea mbali" ama "filamu ya kufa mtu" inayotegemewa kutoka karibuni lakini unapokuja kuangalia filamu hizo ama kusikiliza nyimbo hizo utajihisi KINYAA kwa yaliyomo humo hasa kwa yale yanayokuwa yamesemwa na waandaaji.
Lakini kubwa ni kuwa LINALOKOSEKA NA KINACHOUA SOKO LA KAZI ZA WASANII WETU NI KUKOSEKANA KWA UHALISIA KATIKA KAZI ZAO.
Wasanii wetu wanaendekeza zaidi malipo ya haraka pamoja na kukamilisha kazi lakini kwa hakika kinachokuwemo humo ni aibu. Inashangaza saana kuona wasanii hawa wanaamua kuwa wasimamizi wa kazi zao katika nyanja ambazo hawana ujuzi nazo na hawawashirikishi wataalamu kuleta uhalisia wa matukio katika sehemu zihusuyo hizo.
Waigizaji wetu wanaigiza sehemu nyeti kama SHERIA, HUDUMA ZA AFYA na ULINZI NA USALAMA na kushindwa kufuata hatua sahihi zinazofuatwa huko na matokeo yake kujikuta wanavuruga maana nzima ya mchezo kwa kuondoa uhalisia wa hatua zinazochukuliwa katika kukabiliana na mambo fulani katika jamii.
WASANII WETU HAWANA WASHAURI na hili ladhihirika kwa kazi wazitoazo na hata kauli wasemazo kwa vyombo mbalimbali vya habari.
INASIKITISHA
Mfano halisi ni kipande hiki cha chini cha "hadithi" hii iliyoitwa REVENGE ambacho baadhi ya mambo yanachefua hata kuyaangalia.
1: Muonekano wa mshiriki mkuu Ray. Alivyovuja "damu" nyingi (na damu yenyewe duuuh!) bila mikwaruzo yoyote na kutoonekana kuathiriwa na upotevu wa damu hiyo. Na hata askari kuendesha mahojiano kwa mtu aliye katika hali hiyo, kutomtajia ama kumueleza haki zake za msingi, kutohoji alipopata na alivyopata huo ushahidi alionao na hata mateso wanayompa akiwa kama mhojiwa.
2: Askari na mandhari mazima ya uhoji. Wanahoji kwa kutisha wakiwa na bastola jambo ambalo si sahihi kufanywa kwani hilo laweza kulazimisha kupata taarifa ama maelezo yasiyo sahihi kwani mhojiwa anakuwa ametishwa.
3: Askari walivyokwenda kumkamata mtuhumiwa. Hapa ni zaidi ya ucheshi. Namna askari wanavyokwenda kumkamata MTUHUMIWA HATARI WA MAUAJI wanaingia kwa namna ambayo kama angekuwa hatari kama wanavyojitahidi kumuonesha angewaua hata kabla hawajakaribia mlango wa nyumba yake.
4: Utaratibu wa kusoma hukumu na hasa vifungu vilivyosomwa. Ninalotumai ni kuwa vifungu hivyo vipo na vimekaririwa sahihi. Lakini sina hakika na MFUMO MZIMA WA KUHUKUMU KESI KAMA HIYO.

MAKOSA haya na mengine mengi yanayoonekana katika "maigizo" haya yaitwayo movies yangeweza kuepukwa kama wahusika wangeweza kuOMBA USHAURI kutoka kwa walio na elimu na ufahamu wa kazi hizo. Lakini yaonesha wasanii ndio waandishi ndio wasimamizi wa kazi na ndio wahariri na ndio ma-prodyuza na ndio wanaopigia debe filamu na pengine kusimamia mauzo.
NI AIBU
Mpaka wasanii watakapojua namna ya kuweka UHALISIA kwenye kazi zao, tutaendelea kuzishuhudia zikiwa na "utamu wa bigjii" kwa hadhira finyu na uwezo duni.
Ni mtazamo tuuuu. Labda namna nionavyo tatizo ndilo tatizo
Blessings

4 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ama kweli ni AIBU.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

wasanii wetu bwana. anyway ishu ni kukpoteta kwa fani. badala ya kuigiza kama kilivyo kipaji chako, wee unasomea uhasibu. tunahitaji waigizaji wanaojiamini

lakini pia kuna wasanii wanaofanya vyema kama vile zecomedy nk, sijui unasemaje hapo

Godwin Habib Meghji said...

TATIZO WASANII WETU WANAIGIZA KUIGIZA WAKATI WENZAO WANAIGIZA HALI HALISI

Faith S Hilary said...

No wonder tunaiba...I am just saying...