Saturday, December 26, 2009

WALIWAZA NINI????? Videos

Natumai kuwa KRISMAS yako imemalizika vema na umeweza kuisherehekea kwa usalama zaidi. Kwangu (ama niseme kwetu mimi na familia) ilikuwa saaafi kabisa. Niliweza kuungana na familia yangu na za ndugu na jamaa kwenye makazi ya Mzee Kassembe (soma habari yake nilyoiandika HAPA) na kwa hakika tuliifurahia.
Lakini sasa ni mwisho wa wiki na mwisho wa mwaka pia. Tunaendelea kujiuliza mengi kuhusu tuliyotenda na hata waliyotenda wenzetu. Ni kipengele cha WALIWAZA NINI?? kwa mara nyingine wikiendi hii.

Ok. Kwanza kabisa nakiri kuwa mimi si mjuzi wa kupanga KUMI BORA lakini kwangu hii inaweza kuwa katika "TOP ONE" ya mwaka. Ninalojiuliza ni kuwa, japo ilikuwa ni bahati mbaya, lakini huyu BestMan ALIWAZA NINI baada ya kufanya alivyofanya? Na nawaza ni nini kilifuata baada mbindembinde hiyo?
Angalia nawe uwaze aliwaza nini?

HII HUNIUMIZA TUMBO KWA KICHEKO!!!! Ila yaonesha alivyo jasiri.
Ninalowaza ni kuwa yeye na aliyempa nafasi ya kuimba WALIWAZA NINI?
Hawakujua uwezo wake wa kuimba? Na sasa wakiangalia hii wanawaza nini? Angalia ujiulize..
Hawa ni kati ya waliotawala ulimwengu wa habari miezi mitatu iliyopita. Wakipanga njama za kujitafutia umaarufu lakini hawakujiandaa vya kutosha kwani baadae iligundulika kuwa licha ya kufanya yote yaliyowasumbua waokoaji, walijua fika kuwa hakukuwa na kijana ndani ya baloon hilo... HIVI WALIWAZA NINI?

Na sasa wazazi wanaenda kutumikia kifungo baada ya kuhukumiwa. Soma habari kamili ya hukumu yao HAPA

Nilicheza soka saana kabla mugongo haujaharibiwa na ajali. Na bado napenda mchezo huo. Ninalowaza ni kuwa baada ya kukosa goli kama ilivyokuwa kwa huyu ndugu hapa chini alijifikiriaje? ALIWAZA NINI alipofika kwenye chumba cha kubadilishia nguo? I hope walishinda maana kama walishindwa ama walitoka sare tena kwa tofauti ya goli moja, basi atakuwa analiwaza bao hili kila alionapo

Lakini hata katika kucheza kwangu sikuwahi kukutana na wachezaji ama wapinzani waliowaza kama dada huyu. Hivi kucheza ukijua kuwa mchezo watangazwa na bado ukatenda aliyotenda haya unakuwa unawaza nini?
Mwangalie hapa chini

Ndondi ni mchezo niupendao saana. SIPENDI KUCHEZA, BALI KUUANGALIA. Na nadhani hapo ndipo nilipotofautiana na bondia huyu ambaye nina wasiwasi kama anajua hata namna ya kukunja ngumi. Hebu mwangalie kisha jiulize, yeye na waliomuweka ulingoni wakijua uwezo wake WALIWAZA NINI?


KAMA UMEBURUDIKA NA / AMA KUSHANGAZWA NA HAWA, JIULIZE NI VIPI HAYA YANAWEZA KUTOKEA KWA WATU KAMA HAWA TUKASHANGAZWA NAYO?
LABDA KUNA YALE "MABAYA" TUTENDAYO YANAYOWAFANYA WATU WAJIULIZE WALIWAZA NINI?
Jikague ujirekebishe
Tuonane "Next Ijayo"

***"Waliwaza nini ni kipengele cha kuelimishana tukifurahia. Hiki kitakuwa kikikuletea habari za kweli na kushangaza kuhusu watu ambao wamefanya "UJINGA" na kujikuta wakiingia matatani. Wale watendao ambayo unaweza kujiuliza kuwa WALIWAZA NINI? wakati wanatenda haya.
Kitakuwa na habari fupifupi kutoka ulimwenguni kote. Kwa habari zaidi kuhusu kipengele hiki
BOFYA HAPA"***

5 comments:

Faith S Hilary said...

Hahahahahahahahahahahhaha!!!!! My highlight was "AMAZING GRACE"

"Amaaaaazing graaaaace...", "I wanted everybody to sing with me.."..."Amaaaaaaaazing graceeeee how sweeet the sound....mmmh emmnhmhnhmhnhmhnhh eeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeh"

You gotta love him! Hahahahahaha! Na mwisho mwisho ndio kaniua kabisa na kunizika! hahahahaha

I watched all the videos but this was the one for me....mpaka kapigiwa makofi mwisho mwisho...cnt stop laughin man! lol

Mzee wa Changamoto said...

Hahahahaaaaaaaaaa Candy
Mwanzo nilidhani ni "talent show" ya walio na mtindio wa ubongo lakini baadae nikaona maneno nyuma yake kuonesha kuwa ni kanisa.
Sijui WALIWAZA NINI kumuacha aimbe?

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

"Pluggins" za "kichezeshi" (player) changu hazifanyi kazi na nimejaribu kuzirekebisha lakini zimegoma. Kwa hivyo sijapata bahati ya kutazama hizi video.

Kulikuwa na kipindi kilichokuwa kinaitwa "The Dumbest people/criminals in the World" nilikuwa nakirekodi. Mpaka leo huwa nikiangalia huwa naishia kujiuliza "Waliwaza nini???"

Lakini huyu ndiye binadamu - kiumbe mwenye akili kuliko wote - au kama wanasayansi wanavyomwita "Homo Sapiens!"

Mzee wa Changamoto said...

Pole sana Kaka Matondo
Natamani kama ungeweza kuona japo mbili za mwanzo.
Na kwa kuwa wapenda ndondi kama mimi, ningependa uone ya mwisho pia.
Natumai zitakubali kucheza soon

mwandani said...

huyu jamaa anayeimba Amazing Grace ana uhakika na achokifanya 100% lakini doh!