Nimetafakari changamoto yake nikaona inafaa kweli kufikiria upya kiwekwacho kwenye kipengele hiki. Kwa hiyo sasa nitajumuisha kile kinifanyacho kufikiria ufikiri wao (si kwa mapungufu, bali hata kwa ushujaa na fikra zenye changamoto)
Nikirejea kwenye kipengele chetu leo hii, August 4 2009 niliuliza Kwani kazi ya jela zetu ni ipi???? (Bofya hapa kuirejea) na niliuliza baada ya kuona namna ambavyo jela za wenzetu hapa Marekani zinavyojitahidi katika uzalishaji na kuwafunza wafungwa ujasiriamali ili kuwa na maisha ya kujitegemea wakitoka.
Mwezi uliopita nilikutana na habari hii ya wafungwa wa jela yenye ulinzi mkali ya Cebu Provincial Detention and Rehabilitation Center (CPDRC) huko Ufilipino, waliotembelewa na choreographer wa muda mrefu wa Michael Jackson Travis Payne aliyeambatana na wachezaji wake Daniel Celebre na Dres Reid kuwafunza namna ya kucheza nyimb zilizopo katika albamu yake iliyokuwa itoke ya THIS IS IT.
Baada ya kuiangalia nilikaa chini na kutafakari kuwa WALIWAZA NINI kwenda kufanya mazoezi haya na wafungwa? Labda wimbo una ujumbe kuwahusu na pia labda kwa kuwa hata wa mwanzo uliwahusisha wafungwa, lakini pia, unadhani ni wafungwa wangapi ambao watauwa WAMEGUNDUA VIPAJI VYAO VYA UCHEZAJI na kutambua "utamu" wa kushiriki kwenye mchakato huo?
Unadhani hakuna watakaobadili mfumo wa maisha na kujikita kwenye masuala kama haya waatakapotoka jela? Nawaza tunachoweza kuwafanyia wafungwa waliopo nyumbani kuwawezesha KUPENDA FANI MBALIMBALI WANAZOWEZA KUJISHUGHULISHA NAZO WATOKAPO JELA.
Watazame wafungwa hawa walivyomudu dansi hii hapa chini.
Lakini pia nirejee kwa huyu Bwa'Mdogo Charlie Simpson ambaye kama ilivyo kwa wengi wetu, aliona taswira za kusikitisha kuhusu athari za tetemeko la Haiti. Lakini yeye (pia kama wengi wetu) aliweza kuchukua hatua kusaidia. Akakaa na Mama yake na kufikiria kuendesha baiskeli kuchangisha pesa. Swali ni kuwa WALIWAZA NINI kufikia kuamua kutumia baiskeli kama kichangisha pesa. Na kwa hakika hili lilifanikiwa maana licha ya kuweka malengo ya kuchangisha $500, walipata mara 500 zaidi ya walivyofikiria kwa kukusanya zaidi ya $ 250,000.
Mtazame hapa chini
***"Waliwaza nini ni kipengele cha kuelimishana tukifurahia. Hiki kitakuwa kikikuletea habari za kweli na kushangaza kuhusu watu ambao wamefanya yale ambayo unaweza kujiuliza kuwa WALIWAZA NINI? wakati wanatenda haya.
Kitakuwa na habari fupifupi kutoka ulimwenguni kote. Kwa habari zaidi kuhusu kipengele hiki BOFYA HAPA"***
5 comments:
Waliwaza nini? Nami nimejiuliza mara nyingi. Nadhani ndani ya fikra zao hawawazi juu yao na maisha yao binafsi. Bali wanawaza namna wawezavyo kuutumia wasaa wao kwa ajili ya wengine.
kaka Mubelwa, Je na wewe uliwaza nini kuanzisha hiki kipengele cha WALIWAZA NINI KATIKA BLOG YETU YA changamoto yetu?
Hivi ni asilimia ngapi ya tuwazayo huwa twachagua zinafaa kushea na wengine?
Hivi kila mtu akichangia anachowaza kila siku hivi bloga Rasta Luihamu au Nyahbingi Worrior a.k.a Mkulima asiyelima Mjini na Bloga aliye kuwa wa Ze utamu huwezi kugundua wafananavyo kimawazo?
Si unajua labda wakati nachangia changamoto ya Mzee wa Changamoto naweza kuwa namuwaza kimapenzi Dada Koero?
Samahani bado nawaza!:-(
Kaka Fadhy. Ni kweli kuwa hawa wa leo wanawaza yao na ya wenzao.
Da Koero, niliwaza wazo la wazo lao likawazika wawazavyo nikiwazisha WALIWAZA NINI? Bado na nawaza.
Kaka Kitururu. Mmmmhhhhh!!!
We toboa siri Kaka. Ila waza lililo jema (kwako na kwa "Koero" umuwazaye)
@Mzee wa Changamoto:Kwa bahati mbaya nilikuwa simuwazi kikweli Koero ila umenianzishia wazo la kuwaza kumuwaza Dada Koero .:-(
Hivi lililo jema ni lipi?
Na wasiwasi na lakibinadamu jema hasa liwezavyo kuwa zuri kwangu na baya kwa Koero wakati huohuo.
Najaribu kuwaza kama ni kweli namuwaza Koero nikikubaliana nawe ama kweli kuna mambo mengi ya kuwaza DUNIANI .
Bado nawaza!:-(
Hivi inawezekana hakuna mwisho wa wazo ukishalianzisha wazo?
Post a Comment