Wednesday, February 17, 2010

Kwa wapenda muziki na "WANAMUZIKI TANZANIA"

*Wewe ni mpenzi wa muziki halisi wa Tanzania?
*Una swali kuhusu Muziki na wanamuziki wetu?
*Unapenda kujua ama kusoma historia za wasanii na kujua kwa ufupi walipokuwa, walipo na (pengine) wanachofanya? (kwa kadri ya kumbukumbu zinavyoruhusu)
*Unajua lolote kuhusu muziki wa Tanzania na ungependa kushiriki nasi (wapenzi wa muziki huo)?
Basi nakukaribisha kujiunga na Mkongwe katika kushiriki, kuutetea na kuuendeleza muziki wa Tanzania, UNCLE JOHN KITIME katika blogu yake ya WANAMUZIKI TANZANIA (Bofya hapa kuitembelea)
Meeeengi mema ya kujua na kujifunza utayakuta huko ambako Uncle Kitime ameanza kwa kusema
"Nadhani kuna haja ya kueleza muziki na wanamuziki wa Tanzania kiukweli, na si kwa ajili ya promosheni au kwa ajili ya kusifia au kuponda kama mpenzi au shabiki wa muziki bali kavu kavu.Tanzania nchi kubwa yenye watu zaidi ya milioni 35, ina makabila zaidi ya mia moja kumi na tano, ina muziki wa aina nyingi sana. Bahati mbaya kwa wanamuziki , muziki , Watanzania, na ulimwengu kwa ujumla, wale wachache ambao wanauwezo wa kuweka hadharani hazina hii kubwa ya muziki hawana habari wala shida ya asilimia zaidi ya tisini ya muziki wa Tanzania."
NA TUKUTANE HUKO

3 comments:

John Mwaipopo said...

asante sana 'musee ya' changamoto. sikujua uwepo we hii kitu. imekuja wakati muafaka. unajua tunapoongelea muziki wa kitanzannia na kongo mie upande wangu ni old skul. hapa wa jina kitime kanipatia. atakuwa hanikosi. ngoja niende huko nsije chelewa. ntamuliza mwaswali huyo mpaka akome.

Yasinta Ngonyani said...

Usengwili kwa habari hii yabwina. Ok nimeona umebadili picha pia nimeipenda umependeza.

EDWIN NDAKI (EDO) said...

ni habari njema zaidi..

tutafika tu maana mamabo ya kudanganywa Ndombolo muziki asili wa tz imetosha ngoja Kitime aonyeshe njia