Thursday, February 18, 2010

Natamani kuona ........

Nikiwa mpenzi mkubwa wa muziki wa kiTanzania, NATAMANI KUONA kitu ambacho kitakuwa kikitoa mjumuisho wa muziki huo na KUENZI KAZI NA WASANII wa muziki wa Dansi nchini.
Natamani kuona SIKU YA DANSI NCHINI ambayo bendi zitajumuika kuimba nyimbo za wasanii mbalimbali waliochangia kwa kiasi kikuuubwa kuufanya muziki wa Tanzania kuheshimika. Waliotumika kuelimisha, kuburudisha na pia kukamilisha harakati mbalimbali katika jamii.
Natamani kuona tamasha litakalowaenzi nyota wengi wanaoendelea kutuelimisha kwa miaka nenda rudi na pia waliotangulia mbele ya haki kama kina Marijani Rajabu, M'baraka Mwinshehe, Hemed Maneti, Lovy Longomba, Eddy Sheggy, Kalala Mbwembwe, Agrey Ndumbalo, Fred Benjamin, Adam Bakari, Jerry Nashon, Kyanga Songa, Moshi William, Seleman Mbwembwe, Othman Momba, Joseph Maina, Abel Baltazar, Seleman Mwanyiro na wengine wengi.
Najua ni wengi nawe msomaji waweza kumbusha ambao ungependa kuona wakienziwa kwa kazi zao wawe hai ama wametangulia mbele ya haki.
Natamani kuona TAMASHA LA KILA MWAKA likionesha thamani halisi kwa wale ambao hawakuendekeza URAHISI WA KAZI bali umuhimu na ubora wake.

Natamani kuona......natamani saaaaana
Kwa wale mliotangulia mbele ya haki, mpumzike vema huko mlipo. Kazi zenu zingali zaelimisha na kuburudisha

9 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Nanukuu "Natamani kuona SIKU YA DANSI NCHINI ambayo bendi zitajumuika kuimba nyimbo za wasanii mbalimbali waliochangia kwa kiasi kikuuubwa kuufanya muziki wa Tanzania kuheshimika. Waliotumika kuelimisha, kuburudisha na pia kukamilisha harakati mbalimbali katika jamii." mwisho wa kunukuu:- Natamani kuona wote wangetamani bendi zitajumuika kuimba nyimbo za kale. Kwani kale ilikuwa safi. NATAMANI....UPENDO DAIMA

Mija Shija Sayi said...

Mzee wa Changamoto unajua hata mimi, wewe, Yasinta, Matondo, Kamala n.k tukiamua tunaweza kufanya au kuanzisha jambo hili, ni kiasi cha kujiamini tu. Naamini kila kitu kinawezekana na si lazima kifanywe na mwenye fani, cha msingi ni kukubali kuwa mwanzo ni mgumu na hivyo tegemea lolote utakapoanzisha tamasha la kila mwaka, ila kama uta-FOCUS nakwambia baada ya muda utaona matunda yake.

Mubelwa kwa vile wazo hili ni lako, ni wewe ndo unajua linakukeleketa vipi, hivyo siku ukiwa katika nafasi na wakati mzuri naomba utimize hili, YES YOU CAN akili yako imetulia Mubelwa YOU CAN DO IT.

Stay blessed kaka.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

tamani tu mzee, mwisho wa siku ni kufanikisha au kufa na tamaa

Born 2 Suffer said...

Usikondi Mzee utaoni tu.

Koero Mkundi said...

KAMA VILE SIJAONA JINA LA PATRICK BALISSIDYA!!!????

Anonymous said...

Hayo macho du! Watuua siye mabinti tulio single...maweeee!!!!!!

Mzee wa Changamoto said...

Da Yasinta. Ni kweli kuwa ITAKUWA TUKIO NA TAMASHA LA AINA YAKE KWA BENDI KUJUMUIKA. Hili laweza kutusaidia hata kuanzisha "Tanzania All Stars Band" inayoweza kusafiri huku na kule kututangazia nchi kwa MUZIKI HALISI.
Da Mija. Wewe si mwanamke tu, bali wa shoka. Nashukuru kwa CHANGAMOTO na naamini nahitaji kuwa sehemu ya suluhisho. Si wajua zile TATU KUU ZA MAISHA????? KUWAZA, KUNENA na kisha KUTENDA. Naamini nimebakiza moja. Asante kwa kuwa nasi.
Kaka Kamal. Shumalamu waitu!! Naamini ntafanikisha kabla "sijauacha mwili" Na hilo ndilo lengo.
Kaka B2S....Hayo uliyonifanyia ni maombi na hakuna ninaloshukuru kupata kama maombi. Muungano utuwekao pamoja licha ya umbali uliopo. Na katika hili, ni kuniwezesha kufanikisha nilichowaza na sasa kukinena / kukiandika. Blessings Mankind.
Dada K. Hujaona nilipoomba msaada wa "kujazia" majina mengine? Sasa umesema Patrick Balisidya nami naongeza Mzee Morris Nyunyusa na Dr Hukwe Zawose. Naamini utarejea kuongeza tuone NI WANGAPI WANAOSTAHILI KUENZIWA NA HAYAFANYIKI?
Weeee Anon weweeeeee!!!! Ungekufa ungeandikaje??? Lol
Ntakuombea ujitahidi ku-concentrate kwenye mada kuliko "macho"
Asante kwa uwepo wako.
Blessings

Simon Kitururu said...

Hivi kutamani sio DHAMBI?:-)

John Mwaipopo said...

basi hunishindi mimi. siku hizi kuna wadhamini kibao ambao hawana pahala kwa kuzipeleka pesa zao. yapo makampuni ya simu na viwanda vya 'vilevi'. hawa wanafanikisha mambo mengi ya kijamii. tunaweza anza nao, au?