Saturday, February 20, 2010

Blogu kama "shule msumeno"

Nakumbuka msemo wa "sheria ni msumeno, unakata pande zote". Ina maana aiwekaye na awekewaye wote waathirika ama kulindwa na shetia hizo hizo.
Na blogu ni vivyo hivyo. Inaelimisha wamiliki na wachangiaji. Na kwa watu kuchangia wanasababisha maswali mengi ambayo huendeleza uelimishaji. Lakini wakati mwingine kwa sisi wasomaji hujifunza meeengi tunaposoma maoni ya wachangiaji wetu na wa wenzetu ambao ni wenzetu.
Niliwahi kuandika kuwa Blogu ni shule. Wafunzao ndio wafunzwao (Irejee hapa) na hapo niliandika niliyojifunza kutoka kwa wachangiaji kutokana na mada niliyoiweka.
Hivi karibuni nilipokuwa natembelea Blogu mbalimbali nikagota kwa Prof Mbele na kuvutiwa na mada ihusuyo Kiapo cha Uraia wa Marekani.
Kilichonifurahisha na kunielimisha zaidi ni maoni na majibu ya Profesa Mbele kwa maswali ya Kaka Kamala.
Ama kwa hakika wamenipanua fikra na nakualika kujiunga nao kwa kusoma mada na maoni yote HAPA

3 comments:

Koero Mkundi said...

Ni kweli kaka Blog ni kama shule kabisa, kwani nimejifunza engi san kupiia blog

Sisulu said...

una mkono wangu unaokuunga! blog zina sisimmua fikra ina tufanya tufikiri zaidi nje ya mipaka ya akili zetu. naunga mkono umahiri wako katika uchokozi wa kihoja na malimbuko ya changamoto zako ndugu yangu Mubelwa. Sisi tuanoblogu tusiache tuendelee tuendelee kuinua juu mawazo tuendeleee tusiache UDUMU UMOJA!

Fadhy Mtanga said...

Pengine nikopi na kupesti mawazo ya wengine. Lakini naweza kusema kwa lugha yenye wepesi, kwamba, kublog kwangu kumenisaidia kupata ufahamu wa mambo mengi. Kublog kunaamsha udadisi kwa kiasi kikubwa. Hata unapokusudia kuandika post yako, wachekecha kichwa, wachimba, wafungua vitabu, wazuru wavuti kadha wa kadha ili kupost kitu chenye kuleta changamoto. Kisha waja watu na michango yao. Mingine yakuongezea maarifa. Mingine yakurudisha kuchimba tena.
Haya yanafanya kublog kuwe na manufaa makubwa sana kwa mwandishi na msomaji.
Huwa nasema, kublog ni jambo nilifurahialo sana. Kwani, humu, najifunza mengi sana.