Wednesday, February 3, 2010

TAARIFA.......HAKI YA WANANCHI AMA?

Kama kuna linalosikitisha na kukatisha tamaa nchini Tanzania ni suala zima la TAARIFA NA MAWASILIANO. Hili ni bovu na la kusikitisha kuanzia ngazi ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu MPAKA WANANCHI WA KAWAIDA.
Rais na utawala wake wanapoondoka kwenda nje hawawaelezi wananchi ni kwanini wanakwenda waendako, ni wangapi wanakwenda waendako, watawagharimu wananchi kiasi gani na kuna ulazima gani wa kwenda badala ya kutumia mabalozi na wawakilishi wengine. Hata Blogu ya Ikulu Mawasiliano ambayo ilikuwa na lengo la kuwawezesha wananchi kujua kinachoendelea katika ziara na taarifa za Rais lakini hata muendelezo wa habari zake unasikitisha.
Leo nimetembelea tovuti ya Kaka Paul Kato Ndiho na kusoma habari juu ya UWEZEKANO WA KUPOTEA KWA MADINI YA TANZANITE IFIKAPO 2016.

Mpaka leo Serikali haijawaeleza wananchi kinaga ubaga kuwa madini hayo yapatikanayo Tanzania pekee yamewanufaisha vipi wananchi ama kuinufaisha nchi? Kama madini haya yaliyokuwa kati ya madini yenye thamani ya juu zaidi duniani yamekuwa kwenye mzunguko wa kibiashara kwa miaka 40, yameweza kuinufaisha vipi nchi na wananchi?
Najua kuna uwezekano wahusika hawatagusia lolote kuhusu HABARI HII.
Umeshawahi kujaribu kufungua inayostahili kuwa tovuti ya IKULU ya Tanzania?. Basi jaribu uone. Ninalotaka kukuhakishia ni kuwa kompyuta yako iko sawa ila tovuti ndio mfu. Lakini bila aibu, blogu ya Ikulu Mawasiliano imeweka viunganishi vya Tovuti ya Ikulu ya Uganda na pia tovuti ya idara ya mawasiliano ya Kenya.
NI KIHAKIKISHO KINGINE KUWA SERIKALI HAIJALI MAWASILIANO KATI YA SERIKALI NA WANANCHI.
Lakini pia kipo kingine kinachosikitisha kuwa WALIO NA DHAMANA YA KUSEMA HAWAJUI KUSEMA.
Nimekuwa na tatizo sana na kauli za Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar SACP Suleiman Kova ambaye kauli zake ni nje ya sheria na anaongea kibabe na akihukumu ama kutoonekana kama mtu anayewakilisha CHOMBO CHA SHERIA.
Matukio ya hivi karibuni kuhusu kesi ya RUSHWA / UMILIKI WA PINGU / UTAPELI imeonesha tusivyo na watu walioandaliwa kuwasiliana na wananchi.


Hii ndio Tanzania Yangu....... ambayo TAARIFA KWA WANANCHI SI HAKI BALI NI ANASA NA WANAPEWA PALE WATAWALA WANAPOJISIKIA NA SI SEHEMU YA WAJIBU WA WATAWALA KUFANYA HIVYO.
Tanzania Yangu ni kipengele kinachozungumzia ytale yaendeleayo nchini Tanzania na namna ambavyo "ndivyo sivyo" inavyozidi kupamba moto nchini. Kwa matoleo yaliyotangulia BOFYA HAPA
Tuonane "Next Ijayo"

4 comments:

nyahbingi worrior. said...

Kaka Habari,leo kuna swali nimetaka kukuuliza lakini gafla nikajiambia kimoyomoyo ngoja kwanza nivute muda kisha nitakuuliza hilo swali siku moja.

Respect man.

Jeff Msangi said...

I see..yaani unamaanisha suala zima la Public Relations...mmmh,pingu.Za nini?Kamata jambazi,usalama,fetish,mapenzi.Pingu...mbele ya umma.Uhalifu.Innocent until proven guilty.Vice versa.Huko huko Ulaya..labda.Rushwa...sio kosa kubwa.Kosa kubwa ni kukutwa na pingu.Watuhumiwa wa utapeli...nasema watuhumiwa sugu.Sugu?Kwanini hukuwakamata siku zote?Usiniulize bwan mdogo..next.Jiuzulu basi..eti?Thubutu,shika adabu yako bwana mdogo.Nijiuzulu kwanini?Mmmh..si inaonekana una chuki binafsi...na huyu jamaa wa kwenye luninga?No...huyu ni mhalifu.Ana pingu wakati yeye sio mtu wa usalama.Mbona ana risiti?Ah labda kafoji...twende mahakamani..hakuna rushwa huko!!

Mija Shija Sayi said...

Inakera sana..

Mzee wa Changamoto said...

Kaka Nyahbingi, heshima kwako na NASUBIRI SWALI MKUU.
Najua wawaza lililo jema hivyo usilikawize.
Mkuu Jeff.
Mkuu wa polisi IGP Mwema ameunda kikosi kuchunguza suala la Pingu kujua kama ni halali na kosa kuwa nazo ama la.
Sasa nabaki kujiuliza "kama Kamanda Kova alisema alivyosema na kwa namna na style aliyosema, ina maana mkuu wake hajamuona kumuuliza amkumbushe isivyo halali kuwa na pingu?" Maana Kova kaongea kama vile ni KOSA LINALOTAMBULIKA japo Mkuu wake kasema wanasubiri uchunguzi. Labda "Kanda maalum ya Dar" ina tu-sheria twake.
Ila na switch ya makosa imenifurahisha. Ninalojua ni kuwa Mkuu Kova anahitaji DARASA LA SPEECH. Tena Introduction to Public Speaking maana anavyoeleza kitu utadhani mtemi fulani hivi.
I just hope kwamba Kova alikuwa right, maana la sivyo nitakerwa na hatua itakayofuata. Guess what?
Either NO ACTION AGAINST HIM OR TRANSFER.
Uozo wa huku wahamishiwa kule. Ndivyo tunavyo-balance nchi yetu. Si kwa kuondoa waliotibua, bali kuwahamishia kwingine wakatibue. Lengo ni ku-balance japo twa-balance UJINGA NA MAKOSA..
Dada Mija. Tanzania inatusaidia kupata misamiati mingine. Nadhani twahitaji neno lizidilo INAKERA SANA.
Labda yakereketa mkereketoni.
Bless to y'all