Jumamosi ya tarehe 10 oktoba mwaka jana niliandika kuhusu muungano wa wasanii wa Kenya ambao walitoa wimbo wao waliouita TUPENDANE na pia kuhusu wimbo ulioimbwa na muungano wa wasanii wa Uganda kuhamasisha vita dhidi ya UKIMWI na Kisha nikajiuliza ni lini ntaona waTz Pamoja? (bofya hapa kuirejea).
Lakini hatimaye wasanii mbalimbali wa Tanzania wameungana na kutoa wimbo katika "kampeni tata" ya ZINDUKA.
Achilia mbali kampeni yenyewe ambayo imepata umaarufu zaidi kwa MAJIBIZANO YA UHALALI WA KUFANIKISHA KAMPENI HIYO, wasanii wameweza kutimiza sehemu nyingine ya kampeni hiyo kwa kurekodi wimbo huu.
Kilichonifanya niukodolee macho.
Kwanza ni kupenda kujua walivyozungumzia ugonjwa wenyewe.
Pili ni muungano wa wasanii ambao licha ya kutoshirikisha "majina makubwa" pekee, umetoa muziki unaochangamotoa.
Midundo yake haijawa mbali na mchanganyiko wa wasanii
Rekodi yake haijawa ya kimazingira zaidi. Wametumia weusi kwa nyuma jambo ambalo litasaidia kutopitwa na muda kwa video hiyo kutokana na mabadiliko ya mazingira.
HONGERENI SAANA WASANII KWA HATUA HII KUBWA, MUHIMU NA YA KWANZA.
Twataraji ushirikiano zaidi katika kuisaidia zaidi jamii
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
Hakika wanstahili hongera....
Post a Comment