Thursday, March 4, 2010

Kingine cha ajabu, thamani na manufaa kwa Tanzania

Photo: Marlene Hill Donnelly, Field Museum
A life reconstruction of Asilisaurus kongwe, a close dinosaur relative, from the Middle Triassic of Africa

Julai 20 2009, Dada Subi aliandika makala akishangazwa na habari kuwa Tanzania ina MJUSI MKUBWA AINA YA DINASOUR ambaye "amehifadhiwa" huko Ujerumani. Nami nilipoisoma sikuweza vumilia nilichokisoma kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga amesema wanaendelea kuangalia uwezekano wa kumuacha Dinasour huyo aendelee kukaa nchini Ujerumani na Tanzania ikusanye mapato. Kwa mujibu wa chanzo cha habari ambacho Dada Subi alikinukuu, kimesema "Kwa mujibu wa Waziri Mwangunga, mjusi huyo anaweza kuendelea kubaki Ujerumani na Tanzania kukusanya mapato yatokanayo na mjusi huyo akiwa huko kwani gharama za kumrudisha nchini ni pamoja na kubomoa mifupa yake, kuisafirisha na kuiunda upya. “Tunajaribu kuangalia kama kuna umuhimu wa kumrudisha mjusi huyo ama abaki Ujerumani, alisema Mwangunga akijibu swali la Mbunge wa Masasi (CCM), Raynald Mrope."
Leo tumesikiauwa Dinasour anayeaminika kuishi miaka mingi zaidi ulimwenguni anaaminika kuwa aliishi / kufia nchini Tanzania na mifupa yake ilipatikanaatika Bonde la Ruhuhu nchini Tanzania mwaka 2007.
Waweza kusoma undani wa ufumbuzi na utafiti huu ukurasa wa sayansi na teknolojia wa VOA hapa ama ukurasa huu wa habari hapa National Geographic
Na hili ni DHIHIRISHO jingine la kile nilichoandika Nov 12 09 kuhusu Tanzania Yangu....Yenye vingi vyenye u-wingi wa manufaa usio na manufaa kwa wengi.(Irejee hapa)
SWALI LANGU LABAKI PALEPALE KUWA HIVI VYOTE (nilivyoandika kwenye hiyo link hapa juu) VYAMFAA VIPI MTANZANIA WA KAWAIDA?

4 comments:

Masangu Matondo Nzuzullima said...

"Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga amesema wanaendelea kuangalia uwezekano wa kumuacha Dinasour huyo aendelee kukaa nchini Ujerumani na Tanzania ikusanye mapato."

Oh Boy!

Faith S Hilary said...

Hehehehe kaka Masangu, gotta love the "oh boy" lol!

Personally naona bora huyo angepelekwa National Museum (ndio iko Posta au?), maybe somehow Tanzanians wangefaidika lakini Wajerumani? Hawamrudishi ng'o! lol. Just like the way wanavyomshupalia Tutankhamun...

Yasinta Ngonyani said...

Jamani kazi kwelikweli kupiganaia mjusu..lol

mumyhery said...

Tanzania ikusanye mapato!!!