Sunday, March 14, 2010

Ama kweli mawazo yetu hayafanani.

Hii ilikuwa ya wiki-jana lakini nikaiweka kando kupisha SIKU-KUU ya Da'Mogo wangu Faith.
Ni mwisho mwingine wa wiki na kama kawaida, twaendelea kujiuliza mengi mema na ya kushangaza wayawazayo wenzetu.
Nilipoanza ku-blog nilishangazwa na kuamua kuibandika habari ya huyu ndugu ambaye aliacha usia kuwa akifa, watakaokuja kumuona wamuone akiwa amesimamishwa NA NDIVYO ILIVYOKUWA (kama ionekanavyo hapa). Nimeikumbuka hii kwa kuwa wiki iliyopita nilikuwa natembelea "vibaraza" nikakutana na hii ya huyu ambaye alisema akifa, jeneza lake liwekwe UKWELI WA KILICHOMUUA MSOME HAPA KWA DA SCOLA. Nililowaza ni kuwa WALIWAZA NINI kuacha usia wa hivi?
Tuwaangalie wezi katika mwisho wa wiki hii.
Huyu wa nchini Brazil alienda kuiba kwenye sehemu ya mlo hukoo Brazil. Lakini bahati mbaya alishukia kwenye chimney isiyo sahihi kwani aliyoshukia ilikuwa imetumika kutengeneza BBQ hivyo alilazimika kuomba msaada. Waokozi wa zimamoto waliokuwa wameambatana na polisi walimuokoa na waweza kujua alipoelekea baada ya hapo. ALIWAZA NINI kushukia kenye chimney? Tazama "mnaso" na alivyookolewa hapa chini.

Hawa wameenda kuiba mahala na "wakafanikiwa" katika wizi wao. Ambalo hawakuwa wamelipanga vema ni namna ya kuondoa "troop" nzima waliyokuwa nayo katika kukamilisha "kazi" yao. Wakasahau mtoto. Easy catch. WALIWAZA NINI kwenda "kazini" na mtoto? Na pia WALIWAZA NINI kumuacha mtoto wao ambaye angekuwa na aligeuka kuwa "GPS" ya kujua walikotoka? Tazama taarifa hapa chini

Tumalizie na huko Florida (kwa kina Kaka Maondo) ambako simu ilipigwa kwenye kituo cha DHARURA (911) kuhusu wizi wa gari uliokuwa ukiendelea. Kilichokuja kugundulika baadae ni kuwa simu hiyo ilijipiga kwa bahati mbaya toka kwa mmoja wa wasichana hao waliokuwa wanaiba. Hebu ifuate kwa ufupi wake HAPA

***"Waliwaza nini ni kipengele cha kuelimishana tukifurahia. Hiki kitakuwa kikikuletea habari za kweli na kushangaza kuhusu watu ambao wamefanya yale ambayo unaweza kujiuliza kuwa WALIWAZA NINI? wakati wanatenda haya.
Kitakuwa na habari fupifupi kutoka ulimwenguni kote. Kwa habari zaidi kuhusu kipengele hiki
BOFYA HAPA"***

2 comments:

Faith S Hilary said...

Haya, nilikuwa nataka ni-comment since jana except sijui hii laptop iliwaza nini ilivyojizima yenyewe lol....anywho..

hehehhehe huyo mwizi wangemuacha humohumo!!! Ingekuwa bongo wangewasha kabisa moto...lol its not funny but it kinda is lol

Na hao...mmh...mtoto? sasa hizo "kazi" wanazofanya hawana pesa za kutosha kumpeleka mtoto kwenye daycare or sumtin...that's really weird...to the maximum level!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

tehe tehe tehe