Thursday, May 5, 2011

Pale teknolojia inapotubadilishia tafsiri ya maisha

Taswira toka University of Sydney Prometheus Research Team
Kuna tafsiri pana sana juu ya suala zima la URAFIKI.
Na kila mtu aweza kuwa na namna anayotafsiri, lakini mwisho wa siku, yaonesha tafsiri zoote nilizokutana nazo zahusisha KUJALIANA KWA WATU AMA PANDE HUSIKA. Ina maana yajumuisha kuwa na wakati maalum na wa kutosha wa kujitolea kwa yule uaminiye kuwa rafiki yako. Katika wimbo wa FRIENDS ulioimbwa naye Beres Hammond ambaye alizungumzia suala zima la urafiki, alisema "friends don't mean a thing if when I'm down you keep me down. Friends don't mean a thing, if I can't cry on your shoulder".
Sasa tunapozidi "kuendelea" tunaona namna ambavyo tafsiri za vitu mbalimbali vyabadilika. Oktoba 6, 2008 nilibandika toleo lenye kichwa cha habari Inapotafutwa maana mpya ya kifo kukidhi mahitaji ya afya (Irejee hapa). Yote ilikuwa katika kuangalia namna ambavyo MAENDELEO na sasa TEKNOLOJIA zinakotupeleka.
Leo nimepita kwenye ukurasa wangu wa FACEBOOK na kukuta nina marafiki 231. Nikawaza ninawasiliana na wangapi na ni wangapi ambao hata nikiandika kwenye "wall" zao wananijibu? Nina desturi ya kuwajulia hali wale ambao hawajawasiliana nami mara kwa mara na ambao hatuwasiliano kwa namna yoyote ile (ikiwa ni pamoja na kutembelea na kuacha maoni kwenye blogs zao), lakini bado nikagundua kuwa wapo ambao tangu wametuma "mwaliko" wa urafiki hawajajisumbua kujua maendeleo mengine ya "rafiki" yake mimi. Pia nikagundua kuwa wapo ambao nami sijawajibika kuwasiliana nao kama ambavyo ningependa.
NIKAJIULIZA...KWANINI SIWASILIANI NAO NA BADO NAWAWEKA KWENYE KUNDI LA RAFIKI?
Ni kweli kuwa wale tulionao kwenye rodha ya tuwaitao "marafiki" wanastahili kuitwa MARAFIKI?
Hivi tunajua WAJIBU WA RAFIKI? Tunajua TUNACHOTAKIWA KUFANYA KWA YULE TUNAYEMHESABU KUWA RAFIKI KWETU? Tunatekeleza kila tutakiwalo kutekeleza kwa wale tunaowaita marafiki?
Katika wimbo huu usindikizao hapa chini, Beres ameanza kwa kumuuliza kila ajionaye kuwa rafiki (nami nakuuliza wewe kuwa)
"Friends, what are you supposed to do? Should you build me up or break me down?
Friends what are you there for, if in my needs you're never around.
Friends what are your duties? Doesn't mean loyalty? Tell the truth even if when hurts, no matter what it may be.
Cause I got my problems and you know that I got them but still you say nothing though you know I'm hurting. Half way smiling when something is hurting and you're keeping the solution...friends don't mean a thing if when I'm down you keep me down. Friends don't mean a thing, if I can't cry on your shoulder"
Usikilize kwa umakini na kwa urefu / Ukamilifu hapa chini nawe ujiulize kuhsu URAFIKI

Tujiulize mengi katika kile tuaminicho kuwa ni MAENDELEO na hiki kiitwacho TEKNOLOJIA. Tuangalie namna ambavyo kwa mwendokasi wa kipekee, tunajipoteza kwa kufuata mfumo wa kile tuonacho kwenda na wakati.
Tujiulize MAJUKUMU yetu kwa wale wawasilianao nasi na kujua kama tunahitaji kuwa nao wote ama tuwe na wachache wanaotusaidia katika kukua kwetu na kukuza fikra zetu.

Ni CHANGAMOTO tuu katika kuyaangalia mambo kwa kile ambacho Dadangu Mija alikiita JICHO LA NDANI

No comments: