Wednesday, March 3, 2010

"Viongozi wengi wa Afrika wana fikra za kikoloni"..Dr Garvey

Wiki iliyopita Kaka Sunday Shomari alinitaarifu juu ya mkutano / kongamano kuhusu CLEAN WATER FOR AFRICA lilioandaliwa kwa ushirikiano kati ya Harambee International Development na Constituency for Africa ambalo lilifanyika Jumamosi na kuzungumzia meengi kuhusu ufanikishaji wa kusambaza maji safi na salama barani Afrika. Nilibahatika kuhudhuria.
Kati ya waliohudhuria kongamano hilo ni Dr Julius Garvey ambaye ni mtoto wa mwisho / kitindamimba wa mpigania haki za watu weusi Hayati Marcus Garvey ambaye pia alianzisha Universal Negro Improvement Association mwaka 1914.
Katika kongamano hilo la kwanza kufanyika na ambalo linataraji kuwa la kila mwaka, yalizungumzwa mengi na mwisho wake nikabahatika kupata nafasi ya kuzungumza na Dr Garvey. Nilimuuliza kuhusu UKOLONI MAMBOLEO UNAOENDESHWA NA WAZALENDO JUU YA WAAFRIKA WENZAO NA KUBWA ALILOSEMA NI KUWA VIONGOZI WENGI WA AFRIKA WANA FIKRA ZA KIKOLONI.
TAZAMA SWALI NA JIBU LAKE HAPA CHINI

BLESSINGS

1 comment:

Sarp said...

HE HAD A POINT...........