Saturday, April 10, 2010

Familia zinapowazana

Photo: Katu.com
Naaam waungwana.
Wiki hii, mwenzenu nimebanwa kiasi lakini nimeweza kukusanya mbili hizi kutuwazisha WALIWAZA NINI??
Tuanzie huko TEXAS ambako mzazi mmoja amekamatwa kwa kosa la kuwalazimisha mabinti zake kuangalia matendo ya ngono kupitia mitandao wa tovuti. Katika tukio hilo (la kuonesha watoto picha na video hizo), yasemekana kuwa mzazi huyo alifanya hivyo lakini ilikuwa ngumu kumchukulia hatua za kisheria kwa kuwa (sheria) inamruhusu mzazi kuonesha watoto matukio ya ngono ikiwa tu atakuwa nao. Sheria hiyo ninanukuliwa ikielezewa kuwa na lengo "to protect the privacy of parents who want to teach their children about sex. It states that parents can't be prosecuted for showing "harmful material" to their kids."
Sasa mwendesha mashitaka wa Tawala ya Randall anapanga kudhihirisha kuwa kwa wakati ambao Baba alikwenda chooni ama jikoni ama kutoka kwa dakika chache, watoto wake waliendelea kuangalia ngono hizo bila uwepo wake jambo ambalo ni kuvunja sheria.
Jina la mzazi huyo halijatolewa ili kuficha majina ya wanawe.
Soma habari kamili HAPA.
Photo: Passion4fashiontz Blog
Kisha nikiwa napitapita "mitaani", nikagota kwa Dada Schola ambako nako nikajikuta najiuliza mkasa wa wanafamilia kuwa WALIWAZA NINI?
Hawa sasa "dili" lao lilikuwa la kusafirisha maiti kama mtu aliye mahututi (maana sote twajua gharama za kusafirisha maiti ukilinganisha na mtu aliye hai)
Hii sitaieleza kwa urefu maana Da Schola ameieleza veeema kabisa "ndanje"
(ndani-nje) HAPA

***"Waliwaza nini ni kipengele cha kuelimishana tukifurahia. Hiki kitakuwa kikikuletea habari za kweli na kushangaza kuhusu watu ambao wamefanya yale ambayo unaweza kujiuliza kuwa WALIWAZA NINI? wakati wanatenda haya.
Kitakuwa na habari fupifupi kutoka ulimwenguni kote. Kwa habari zaidi kuhusu kipengele hiki
BOFYA HAPA"***

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

MMmhhhh!!

Faustine said...

...Nadhani nisingekuwa nafanya ninayofanya sasa hivi, ningependa kuwa pyschologist. Nami upenda kujua nini kinachoendelea ndani ya kichwa cha binafsi, inakuwaje tunafikia maamuzi tunayofikia.....
Nadhani umesikia stori ya yule mama wa Marekani ambaye amezua kasheshe ya kimataifa kwa ku-adopt mtoto toka Urusi na baadaye kumrudisha mtoto huyo nchini huko bila mwangalizi baada ya kushindwana naye...