Thursday, April 22, 2010

Them, I & Them......PROPHECY...Luciano

Photo:BBC Africa Beyond
Watu wana imani tofauti juu ya kinachotokea sasa ulimwenguni lakini ukweli wa mambo ni kuwa MAAFA YA KUTISHA yanachukua roho za watu wengi. Lakini pia wapo wengi wanaonusurika ambao walikuwa miongoni mwa wale waliokuwepo. Licha ya kuwa taswira za tetemeko lililotokea Haiti bado zaendelea kusumbua fikra za wengi, lakini pia rekodi zaonesha kuwa kumetokea zaidi ya matetemeko 11 tangu kuanza kwa mwaka huu siku 113 zilizopita. Orodha toka wavuti ya Chuo Kikuu cha Wisconsin katika kitivo cha GeoScience inaonesha mfululizo wa matetemeko yaliyotokea tangu januari mosi ni:
1/3/10 Solomon Islands 7.2
1/10/10 Offshore of Northern California 6.5
1/12/10 Haiti Region 7.0
2/10/10 Illinois 3.8
2/27/10 Offshore Maule, Chile 8.8
3/5/10 Southwest of Sumatra, Indonesia 6.5
4/4/10 Baja California, Mexico 7.2
4/6/10 Northern Sumatra, Indonesia 7.7
4/11/10 Solomon Islands 6.8
4/11/10 Spain 6.3
4/13/10 Southern Qinghai, China 6.9

Haya ni mbali na mafuriko na "machafuko' mengine yasababishwayo na UASILI WA DUNIA.
Kisha kuna mauaji ambayo kila kukicha twayasikia ambayo nayo yaonekana kuua wengi. Wapo wanaouawa wakiwa safarini kwenye ajali mbalimbali, wale ambao wanavamiwa tu, wanaokufa wakiwa usingizini na kadhalika.
Binafsi si muamini wa ile filamu ya kutabiri mwisho wa dunia mwaka 2012, lakini ninalojua ni kuwa MWISHO WA DUNIA KWA WENGI NI KILA SIKU ambapo wengi wanafariki katika matukio ambayo mwenzao ama wenzao waliokuwa nao pembeni wananusurika. Na hii yaweza kuwa inatukumbusha kuwa WAKATI WA MWISHO WA MAISHA YETU HAUNA UMOJA na ni kila mmoja kwa nafsi yake ataionja mauti. Labda hii ingeeleweka vema, ingesaidia watu wengi kutenda yale watendayo wakijua kuwa hawatahukumiwa na yeyote bali pekee. Ni hapa ambapo UPENDO watakiwa uanzie ndani na kwa mtu binafsi, USHIRIKIANO unapotakiwa kutoka moyoni na si kwa kuwa fulani anafanya na hata HESHIMA pia.
Kwa hiyo ni vema kujua umuhimu wa kushirikiana ilhali kutambua umuhimu wa kujitegemea na kufanya maamuzi chanya ambayo yataakisi u-sisi kama mtu mmoja mmoja na si kama kundi.
Na ndipo tunapogota IJUMAA YA LEO kwake Jephter Washington McClymont ambaye wengi wanamfahamu kama LUCIANO ambaye katika albamu yake ya Jah Words, alilizungumzia hili kwenye wimbo PROPHECY.
Ameanza moja kwa moja na ukweli wa tukio kuwa "two shall be sleeping and one shall be taken away. In these trouble times the wise must watch and pray, the light is shining yet fools go astray, guaranteed not to them another day"
Na ni hapo anapoeleza yale ambayo yanastahili kutokea maishani mwetu lakini akisema WALIO HAKI WATAKUWA NA AMANI NA WOKOVU akisema "see there will be DEATHS and DESTRUCTIONS taking all over the world, and WARS and CONFUSIONS taunting the hearts of men, but there will be PEACE and SALVATION for the rightheous men, REJOICING and REDEMPTIONS for the clean hearted one"
Na mwisho anaeleza namna ambavyo twatakiwa kuwa wema na kukabiliana na MAJARIBU mbalimbali ambayo twakumbana nayo katika maisha kwani Mungu atatushindia tukimwamini na tushindapo, basi turejeshe shukrani kwake na si kujsifu kama vile ni sisi tulioweza kuyashinda. Anatueleza bayana kuwa utafika wakati ambao WALE WALIOTENDA MABAYA HAWATAKUWA NA PA KUKIMBILIA anaposema "some will run to the rocks, and the rocks will cry out, THERE'S NO HIDING PLACE HERE and some will run to the mountains and the mountains will cramble into the sea of dispear"
Tuwe wema, Tuwaze Vema na Tutende Mema kwani FADHILA ZETU ZI PEMA.
Msikilize Luciano hapa chini

**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ni ujumbe mzuri sana Ahsante. Ijumaa njema nawe pia na familia yako. UPENDO DAIMA!!

Albert Kissima said...

Kwa namna walimwengu walivyo sasa,thamani ya binadamu imekuwa ni ndogo mara nyiiiiingi ya 'pesa' na thamani ya pesa inavyozidi kupanda ndivyo thamani ya binadamu inavyozidi kushuka. Shaka ya kwanza naiweka kwenye Dini (zenye kumjua Mungu ajulikanaye kwa kuumba mbingu na nchi).Nina shaka sana na namna watu wapatavyo mafundisho. Haiwezekani kwenye nyumba za ibada watu waonyeshe unyenyekevu wa hali ya juu,upole,ukarimu,upendo,moyo wa kutoa,huruma na washindwe kuyafanya haya wanapochangamana uraiani!



Leo hii dini zikiambiwa zitaje mafanikio zilizoyafikia, wataweza kuyataja kweli? Swali hili laonekana ni jepesi lkn ukweli ni ligumu! Hali ya sasa ya ulimwengu,kama alivyoeleza kaka Mubelwa,nadhani dini zatakiwa zione hali hizi kama changamoto kwao na ziweke mikakati thabiti ya kukabiliana nazo.