Wednesday, May 5, 2010

Binadamu anapowaza FITINA katika kushukuru

Image @ INFINITY BLOG
ONYO: USISOME KAMA UNAKASIRIKA KABLA YA KUTAFAKARI.
Mara kadhaa nimekuwa nikiwaza kuhusu SHUKRANI mbalimbali nizisikiazo kama huwa zatolewa zikimaanishwa ama zatoka ili kuwafurahisha waliozitoa kwa waliopokea?
Labda nianze na maswali:
Umeshawahi kumsikia ASKARI SHUJAA wa nchi yoyote?
Ama askari yeyote anayeitwa shujaa?
Unadhani atakuwa shujaa kwa sababu gani?
Kwani RAIS MWENYE MAFANIKIO ama MPAMBANAJI YEYOTE ni yupi?
Unadhani wote kwa pamoja wana lipi lifananalo?
Ntarejea kwenye majibu yake ila niendelee na tafakuri.
Unaweza kudhani kuwa Tanzania yetu haina ma-askari jasiri ama sehemu za Tanzania hazina askari ama watu jasiri, lakini kumbe wanaweza kuwa jasiri kuliko wengi tuwajuao, lakini tofauti ikawa kwenye "mtu wa kuwafanya waonekane jasiri"
NINAMAANISHA WAHALIFU.
Ukisoma (hapa) juu ya askari aliyepambana na majambazi kwa kutumia jiwe unaweza kuona kuwa askari huyu HAKUWA shujaa mpaka alipoamua kupambana na wale walio "kinyume" na ushujaa wake kumfanya awe shujaa. AKAZAWADIWA. Lakini nina hakika wakati wa kutoa shukrani hakuwashukuru wale waliomfanya"afikie mafanikio" hayo.
HIVI HII NI HAKI?? TWAWAZA NINI?
Leo hii mtu akitunukiwa tuzo ya uandishi bora wa kufukua rushwa, ataanza kuwashukuru wooote waliomuwezesha kupata tuzo hiyo lakini hatawashukuru wala rushwa ambao ndio waliomfanya apate cha kuandika, kuonekana, kuthaminika na hata kupata zawadi aliyopata.
Nirejee hapa nchini Marekani:
Nilipokuwa nasoma darasa na SPEECH, tukawa tunajadili maisha ya Rais wa sasa wa hapa Marekani na swali nililouliza ni kama wapo wanaoamini kuwa kama angelelewa na wazazi wote (akiwamo baba yake ambaye hakuonekana kuwa mtu wa kujali familia) angeweza kuwa namna alivyo. Je! Haiwezekani kuwa amekuwa alivyo kwa kuwa alikabiliana na mapungufu ya kutolelewa na baba yake? Unadhani atakapokuja kutoa shukrani atamshukuru baba yake "kwa kuchangia kuwa jasiri na makini" kwa namna alivyo? Sidhani. Ila ni halali?
Ni yale yaleee niliyoandika April 8, 2009 nikikumbusha kuwa Huwezi kuwashukuru wote, waombee tu!!! (rejea hapa) na kati ya niliyosisitiza ni umuhimu wa ma-adui ama wale wenye mtazamo tofauti na wa kwetu katika ukuaji wetu. Sasa kama nao wapo katika UMUHIMU kwetu, ni kwanini TUSIWASHUKURU?
Hivi leo hii kuna ambaye hajui kuwa Rais Obama alichukua madaraka kwa kuwa alionekana kuwa SULUHISHO la mmomonyoko aliouacha Rais Bush? Umeshamsikia akimshukuru mwenzake huyo hadharani kwa "kulikoroga" kiasi cha yeye kupata kura?
Ama uliwahi kumsikia mtu anayepewa tuzo ya "kuwa na akili zaidi" darasani akiwashukuru wanaoonekana kuwa mazezeta ambao ndio waliomfanya aonekane yuko juu?
LABDA matajiri wangestahili kuwashukuru maskini kwanza kwa kuwafanya wao waonekane kuwa na umuhimu (wa nje) unaowafanya wawafanye wasio na fikra za ndani kuwaona ama kuwafanya kuwa na nguvu za ziada katika maamuzi ya maisha ya watu.
Ama yule aonekanaye "amependeza" aanze kuwashukuru wale ambao hukosoa "mitoko" ya wenzao jambo ambalo huwafanya wawe makini katika kuvaa ili wasije kuwa gumzo.
Najua kuna walioniambia kuwa anarejea makala zake mara mbili kwani hakutaka Kaka Kamala amkosoe na sina hakika kama alishamshukuru Kaka Kamala kwa kumuongezea umakini wa maandalizi ya maandishi yake.
Na naamini kama serikali zetu zingekuwa na UVUMILIVU wa kupokea marekebisho toka kwa wakosoaji, wangeboresha utendaji wao na kuwa na huduma bora kwa wananchi. Lakini wao "wanawanyamazisha"
KWANI WEWE UNAPOSHUKURU HUWA UNASHUKURU NANI NA NANI NA KWA LIPI? LILE UONALO KUWA JEMA AMA HATA WALE AMBAO WANAKUFANYA UHAKIKISHE UNATENDA MEMA ILI "USIWAPE LA KUSEMA"?
Msikilize NASIO akisema HYPOCRITES

***"Waliwaza nini ni kipengele cha kuelimishana tukifurahia. Hiki kitakuwa kikikuletea habari za kweli na kushangaza kuhusu watu ambao wamefanya yale ambayo unaweza kujiuliza kuwa WALIWAZA NINI? wakati wanatenda haya.
Kitakuwa na habari fupifupi kutoka ulimwenguni kote. Kwa habari zaidi kuhusu kipengele hiki
BOFYA HAPA"***

6 comments:

MARKUS MPANGALA said...

Mkuu umenikumbusha SHUKRANI ZA EMINEM mwaka 2004 katika tuzo za Grammy, sijui aliwaza nini kwakweli kwasababu alisema maneno haya ambayo nayaweka katika kiswahili. NASHUKURU WOTE WANAONIPENDA, NAWASHUKURU WOTE WASIONIPENDA,NAWASHUKURU WOTE WANAONICHUKIA.

yaani hapo alikuwa na tuzo mkononi kila nikiwaza, nabaki domo wazi ALIWAZA NINI?

Yasinta Ngonyani said...

nitarudi hapo baadaye ngoja nikapate kikombe cha chai kwnza....

Fadhy Mtanga said...

Umenifikirsha sana kaka.

Mkuu hivi majuzi tu mwanautambuzi Kamala alisisitiza haja ya kumshukuru na kumtukuza Yuda Iskariote kwani ndiye aliyefanikisha kukamilika kwa unabii na kazi ya Yesu Kristo. Kwa maana Yuda ni mtu muhimu sana kupewa shukrani na utakatifu.

Nirejee salamu zangu kwa siku yangu ya kuzaliwa gonga hapa kuisoma
niliwazungumzia wale wanichukiao. Nikasema...lakini nafahamu kuna wale wanichukiao. Hawa huwa sipendi kuwaita maadui. Hawa huwaita wanaonipa changamoto. Ninajivunia kuwa na kundi hili la watu katika maisha yangu. Kundi hili huwa chachu ya mimi kujitahidi kupiga makasia ili nisonge mbele. Nikasema mengi, nikiwashukuru sana kundi hili na kuwaombea wazidi kuwepo.

Kuna methali moja ya Kidanishi inasema, "ujasiri huja pale jambo linapokuogofya...kama hakuna jambo lililokuogofya ukakabiliana nalo, kamwe usijihesabu kama jasiri."

Kwa hiyo tunapaswa kuyashukuru mambo yanayotufanya kuwa hivi tulivyo. Changamoto zake. Yule trafiki wa Ubungo asingepongezwa kwa ujasiri na kupandishwa cheo kama tukio la ujambazi lisingetokea pale NBC Ubungo. Nadhani katika maisha yake na hata katika shukrani zake kwa wananchi na vyombo vya habari na jeshi, angewashukuru majambazi wale. Maana bila wao angesota na ukonstebo miaka mingi.

Ha ha haaaaaaaa!

Kaka umenifikirisha sana.

Ahsante mkuu.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

ndio imetulia, ni somo kati ya masomo

eti unadhani NGOs zote zinazopingana na mfumo dume ni kweli zinauchukia mfumo huo???

hivi mwanamke akiacha kunyanyaswa wenye NGOs hizo watafurahia?? si watakuwa hawana kazi tena??/

japo inahitaji moyo kutoa shkrani za kweli kwa yule aoonekanaye kuwa adui au sio??

Koero Mkundi said...

Labda nami niulize. Hivi kaka uliwaza nini?

Faith S Hilary said...

Sometimes inaweza kuchukuliwa kama ni "SARCASM" kama huo mfano alioutoa kaka Markus coz imagine Obama starts to say "Finally, we have solved this and it is all thanks to George Bush!" (as you said it...somehow), people will be like "WHAT?!?!".

It is an interesting way to "THANK" and I will take that on board to help me later in life (u knw I m still mtoto lol)...Ningeandika something about dad na redio "stesheni" alizokuwepo mwanzo lakini ngoja niache tu...sitaki fimbo...I think you know what I mean...Later! x