Wednesday, July 21, 2010

Uhiari wetu wa lazima....Tunautumiaje????

Image @ WalkerNews.net
Haya sasa. Huu ndio wakati muafaka wa kuelekea UWEKEZAJI wa maisha na maendeleo ya waTanzania na Tanzania kwa ujumla. Wakati wa UCHAGUZI. Wakati ambao wananchi wanaelezwa mengi kuliko wanavyoweza kuelewa na pengine kupelekwa kwingi kuliko wanakoweza kwenda.
Wanawazishwa mengi kuliko uwezo wa fikra zao na kutamanishwa meengi kuliko uwezo wao wa kupatiwa.
NI WAKATI AMBAO WANACHAGUA WALE WATAKAOCHUKUA DHAMANA YA MAISHA YAO NA NCHI YAO.
Lakini ni nani mwenye mwajibu wa kumuelimisha mTanzania wa kawaida juu ya Ukweli vs Uongo usemwao? Ni nani wa kumuamsha mTanzania kuwaza na kuuliza maswali muhimu kwa ajili ya kupata njia sahihi za kutatua matatizo yao?
Niliwahi kuuliza kuwa YAKO WAPI MAHITAJI YA WAHITAJI? (irejee hapa) na nia hasa ilikuwa kuwaamsha wale wanaoongoza vyama na mashirikisho ya WAHITAJI kuandaa maswali na mikakati mbalimbali. Mpaka sasa sijasikia lolote toka kokote kuhusu mikakati ya "kuwabana" wagombea juu ya haki za WAHITAJI.
Sasa ninashuhudia UTITIRI wa wagombea kwenye mabandiko mbalimbali, nawaza AZMA ya kuwaweka bila kuwaeleza kwa kina. Kila siku twaona "blah blah blah atangaza nia" na baada ya hapo twaona blogu na tovuti nyingi zikiishia hapo na kutoeleza nia ya huyo mgombea kufanya hivyo. Hatuelezwi historia na uzoefu wake kikazi na kiutawala na mara chache tumeelezwa undani wa nia ya mgombea na kufaulu na kufeli kwake.
Labda tuanze kuwa KUTHAMINI NA KUTAMBUA UMUHIMU WA NJIA HII YA UPASHANAJI HABARI AMBAYO NI HIARI.
Na japo ni ya hiari, bado ina ulazima katika kuitekeleza kwa ufanisi. Hatutaki kurejea yaletale niliyoandika juu ya Tanzania Yangu.. Yenye vyombo vingi vya habari visivyo na habari zaidi ya taarifa (irejee hapa). Ni wakati wa blogu na tovuti zetu kuacha KUTAARIFU JUU YA WAGOMBEA na kuanza KUTUHABARISHA JUU YAO.
Natambua na kuheshimu ukweli kwamba ku-blogu ni hiari, lakini katika kuelimisha umma juu ya maamuzi muhimu kama UCHAGUZI ujao, basi ELIMU HII INA ULAZIMA.
Tuonane Next Ijayo

Uchaguzi Tanzania ni "label" inayozungumzia namna niionavyo nchi yangu ya Tanzania ijiandaavyo na uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2010. Kwa maandishi mengine juu ya mada hii katika "label" hii BOFYA HAPA

4 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

mh, sijui, ngoja nilee kwanza kasijekuwa kanasihasa, kawa hasa

Fadhy Mtanga said...

kaka Mubelwa umejadili jambo la maana kweli. Nadhani huu si wakati wa kuripoti, bali kuzijadili siasa kwa marefu na mapana.
kundi fulani la vijana hususani wa mjini (utafiti usio rasmi) linatumia mitandao hii ya jamii kama blogu, fesibuku, twita na kadhalika.
kama tutaelimishana vema kupitia mitandao hii, basi tutakuwa tumetoa mchango wetu mzuri wa ushiriki katika mustakabali wa nchi yetu.

Kamala mfundishe kijana ubunge kabisa kabisa.

SN said...

Mubelwa, yaani haya mambo.. utadhani tulikaa kitako tukaamua tuandike kuhusu haya mambo; kwa mpigo. Na mimi nitaandika mpaka kieleweke:

http://vijana.fm/2010/07/21/vijana-wa-tanzania-tuamke/

Jeff said...

Muhimu na ni kweli.Wakati wa kurekodi kila ahadi.Wakati wa kuhoji kila kitu.Kwanini?Ni haki.Kesho ikiwa mbaya,tusije kutwa tumeduwaa.Mlikuwa wapi wakati ule?Watauliza huku wakifunga vioo.Joto kali.Hakikisha briefcase yangu iko salama.Ina ten percent.Si mlinichagua kwa ahadi zangu zisizotekelezeka?

Blog zina kazi ya ziada.Wakati ni huu.