Wednesday, August 11, 2010

RAMADHANI NJEMA NDUGU ZETU

Kwa siku kadhaa zilizopita, asilimia kubwa ya takribani watu Bilioni moja waumini wa dini ya Islamu wamekuwa wakijiandaa kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani, mwezi wa tisa na MTUKUFU zaidi katika kalenda ya kiIslamu.
Mwezi huu uambatanao na mafunzo na njia sahihi za kuishi kiIMANI, na uwe nguzo ya maisha yetu hata baada ya kumalizika kwa mwezi huu
Yafunzwayo na kuhimizwa kwenye mfungo na mwezi mzima, ni mambo ambayo naweza kuyaita NJIA SAHIHI ZA KUISHI KATIKA JAMII na ninaamini yale yafunzwayo na maisha tuishiyo mwezi huu, tutayaendeleza maishani
Blogu ya CHANGAMOTO YETU yawatakia wale wote wafungao na kuamini katika mwezi huu, MWEZI NA MFUNGO MWEMA na kwa wale wote waishio na waamini twawatakia ushirikiano mwema kwa waamini
RAMADHAN KAREEM.

2 comments:

emu-three said...

HERI NA BARAKA KATIKA MFUNGO HUU. Natumai lengo ma madhumuni ya nguzo hii itatekelezwa ipasavyo, kwani hata gari linahitaji `kila muda linapumzishwa kwa matengenezo' na kwa imani ya Kiislamu, mwezi wa Ramadhani ni kipindi cha matengenezo ya mwili. Kuna faida zake nyingi za kufunga kama kuondoa takataka zisizofaa, kufanya mpangilio mzuri mwilini, kuijua njaa ni nini ili ukimuona mwenye njaa iwe rahisi kwako kumsaidia, kuongeza imani, kujenga upendo, na kubwa lao kumtii mwenyezimungu.

Yasinta Ngonyani said...

Kila la khei kwa mfungo huu wa ramadhani.