Wednesday, October 13, 2010

Mwaka mmoja "baadae".......

Kuna mambo niliyoambiwa kuwa UTAMU wake hutokana na UCHUNGU wake. Nilisimuliwa na kupewa mfano wa mtu aunguapo kisha akaweka barafu sehemu iliyoungua (japo nilihusiwa kuwa si nzuri kwa afya), lakini ati kwa m'badiliko wa ghafla wa joto, mtu husikia maumivu huku akihisi unafuu wa maumivu.
Labda ndivyo ninavyoweza elezea maisha yangu kwa mwaka mmoja uliopita.
Yamekuwa na changamoto nzuri za malezi na mafunzo kuhusu mwana na wana. Majumuiko ya ki-uzazi na mengine mengi. Haya yote yalikuwa mabadiliko ya ratiba na haya yote yalitokea bila kupunguza pilika nyingine na hivyo kuweka mchakato mwingine, lakini ni mchakato huo ambao leo hii naukumbuka na kujivunia. Ni hekaheka hizi ambazo zimeyafanya maisha yangu kwa mwaka uliopita kuwa mazuri na yenye mtazamo chanya zaidi licha ya mengi "kuvuta".
Leo hii ni mwaka kamili tangu MWENYEZI MUNGU atubariki na mwana wetu Paulina Arianna na kwa hakika tuna kila sababu ya kumshukuru kwa kutuonesha njia na pia kutulinda. Tumeona mengi, tumejifunza mengi na pia tunaendelea kujifunza.Mwaka wa kwanza umekamilika na twamuomba aendelee kutujaalia mengi mema kama awajaliavyo wengine wengi KULINGANA NA MAPENZI YAKE.
Na kumzungumzia Paulina bila kusema kuhusu mamake ni kutokamilisha "hesabu". Shukrani kwa muumba kwa kunipa "nusu yangu njema" iliyo na ukamilifu zaidi ya nilivyowahi tarajia. Haya machache yanakamilisha umuhimu wa uwepo wako. UPENDO KWAKO MAMA P.
Na pia kwa wale ndugu, jamaa, marafiki na wale wote ambao kwa namna moja ama nyingine wamehusika na maisha yetu kama mtu mmoja mmoja na kama familia kwa ujumla. Bila ninyi tusingekuwa hapa. Upendo kwenu.
HERI YA KUMBUKUMBU YA SIKU YA KUZALIWA MWANA.

23 comments:

malkiory said...

Kiwango cha malezi mazuri ya wazazi yanaonekana kwenye uso wa Paulina kwa jinsi anavyotabasamu.

Hongera Paulina kwa kutimiza mwaka. Mungu akubariki na akuzidishie afya njema.

Mija Shija Sayi said...

Hongera Paulina, anaonekana ni wa shoka kuzidi hata wazazi wake, hivi vizazi vya siku hizi vimebarikiwa sana. Hongera malkia wetu na Mungu azidi kuwa nawe daima na daima. Amen.

Yasinta Ngonyani said...

Kweli kabisa matunda tunayaona Hongera sana shangazi Paulina kwa kutimiza mwaka leo. Na Mungu azidi kuwapa nguvu wazazi wako. Baraka kwako na kwa baba na mama yako .

EDNA said...

Hongera Paulina Mungu na akulinde,akukuze uwe na busara na upendo kama wazazi wako.

Simon Kitururu said...

Hongera Paulina!

emu-three said...

Hongera hongera tena sana...mmmh, naona karibu anadai mdogo wake..!

emu-three said...

Hongera hongera tena sana...mmmh, naona karibu anadai mdogo wake..!

John Mwaipopo said...

paulina mamaaa
shemeji kaleta mashitaka
sielewi lengo la ndunguyoo.....

mie namtakia kila la heri the litle woman akue aje kuwa dokta kama babake mkubwa chib na shangazi yake subi wa nukta sabasaba

hiyo ndiyo shida ya kublog tanzania. ukiclick 'publish comment' hakuna mabadiliko yoyote. unadhani bado unaclick tena. nothing changes, unaclick tena na tena na tena halafu matokeo yake ndio hayo.

for this post, it means more happy birdhay wishes from me

PASSION4FASHION.TZ said...

Kweli mwaka umekimbia jamani!juzi tu.mwanamke wa shoka Paulina alizaliwa hata sijasahau ujio wake tayari mwaka?

Hongera sana shangazi,mungu azidi kukupa afya njema,uendelee kuwa mwanamke wa shoka! kama shangazi yako Mija Shija anavyosema nawe umo kwenye kitabu chake tayari....lol.

Albert Kissima said...

Hongera sana mtoto Paulina Mubelwa Bandio kwa kutimiza mwaka mmoja, Mungu amlinde, ampe siha njema na maisha marefu yenye furaha tele.

Hongereni pia wazazi wa Paulina. Kulea si lelemama, ni jukumu hasa, na twashukuru, wazazi jukumu hili mwalisimamia na mtaendelea kulisimamia vyema, twamuona Paulina pichani, mwenye furaha, mwenye afya njema. Nasema hongereni sana. Mungu awape uwezo zaidi ktk malezi na katika shughuli za maisha za kila siku. Mungu awajalie baraka ya miaka mingi yenye amani, upendo, mafanikio na furaha daima.

Faith S Hilary said...

woooooooooooooo...why didn't anyone tell me about this? Am I late?...(UK I think so but there, not yet and there is where she is...) Jamani I am sorry but I didn't see this (or remembered) but HAPPY BIRTHDAY PAULINA!!!!!!!!! May God Bless you so much and guide you in life...there's a lot to learn, see and experience....Love you girlie! xoxo (give her my special kiss on the cheek...please :-))

Mbele said...

Hongera sana, na kila la heri. Baraka kubwa hii. Katoto kazuri sana. Kalivyo makini, kanaonekana kataanza kublogu muda si mrefu :-)

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Kila la heri Paulina Arianna. Kuna somo yako mwingine huku Florida na sijui mtakutana lini. Ubarikiwe!!!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

uwiiiiii umefikia pazuri katika kulea mkuu

Anonymous said...

Yes yes that is my gaarl' yap yap Paulina mtoto umejazia jazia. Mashaallah mungu akupe afya njema na long life. Just know that your aunt here Tennesee love you and thinking about you. Hongereni familia ya Muberwa. mtoto totoo'guuu guu. HEY'

Ashura Mbeyu- MEMPHIS, TENNESEE

Subi Nukta said...

Hongera sana kwa Paulina kutimiza mwaka mmoja wa kuzaliwa.
Hongera pia kwa familia, ndugu na jamaa wote walio bega kwa bega katika malezi.
Hongereni sana.