Saturday, October 23, 2010

Sikiliza Times Fm live

"Ingilio" la studio mpya za Times Fm. Kawe Dar
Kama kuna kitu ambacho nimefurahia siku ya leo ni kuweza kusikiliza matangazo ya Radio Times Fm moja kwa moja toka studio zao mpya za Kawe jijini Dar Es Salaa. Kwa wale wenzangu ambao mko nje ya nchi, mnatambua namna ambavyo tunakosa mawasiliano ya moja kwa moja ama matangazo toka nyumbani. Lakini kwangu mimi ni zaidi ya ku-miss matangazo. Najijua kama "mlevi" wa masuala ya utangazaji na pia "mpenzi" wa kituo hiki. Wenyewe wanasema "it's where it all started". Hapa (Times Fm) ndipo nilipopata fursa ya awali kuonesha kipaji na pia kuendeleza kile nipendacho. Na sasa naendelea kupaheshimu kama CHANZO cha furaha katika kazi niitendayo
Studio mpya za Radio Times Fm
Lakini pia najivunia JUHUDI ZA DHATI za uongozi wa Times Fm kuifanya radio hiyo kuwa ya kisasa zaidi na pia kuendelea kusikiliza na kuheshimu maoni ya wasikilizaji (na wasikilizaji watarajiwa kama sisi)
Kaka Shaaban Kondo akiwa kazini
Mwisho nitoe shukrani za pekee kwa Kaka Shaaban Kondo ambaye licha ya kukubali kushirikisha picha hizi zote (toka ukurasa wake wa Facebook) lakini pia ndiye aliyenijuza kuhusu kupatikana kwa matangazo ya moja kwa moja ya radio hiyo mtandaoni
LAKINIIIIIIIIIIIII......
Si wanasema ya kale dhahabu? Ona "dhahabu" ya Times Fm (picha ya chini) miaka ya awali ya 2000. Hapo ndipo walipopita kina Paul James Swea, Godwin Gondwe, Master T, Zuhura Yunus, Fred Fidelis, Rahab Fidelis, Ally Kashushu, Sigory Paul, DJaro Arungu na wengine wengi ambao kwa sasa wako katika "viwango" vya juu vya utangazaji.
Well!!! Nami nimejisahau (japo sijakua kiwango) lakini bado nina kumbukumbu ya Times iliyozaa hii ya sasa
"The real Times Fm". Iliyokuza UBUNIFU kwa watangazaji wake. Hahahahaaaaaaaaaa
Tofauti ni ndoooogo tu jamani. Nyie mwaonaje?

Ukitaka kusikiliza Times Fm moja kwa moja, basi BOFYA HAPA

2 comments:

Subi Nukta said...

Nyeeeeeeeeeeeeeeee! Nimefurahije?
Asante saaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaana!

Mzee wa Changamoto said...

Dada Subi shukrani kwako kwa KUONESHA NJIA. Pia kwa uongozi wa Times Fm kwa kutuwekea "hii kitu" mtandaoni na pia kwa Kaka Shaaban Kondo kwa kushirikiana nasi kutujuvya.
Mimi nimefanya kuwasilisha ili na wengine WAFAIDI kama nifaidivyo mimi
KARIBU TENA DADA