Friday, October 8, 2010

Them, I & Them.....CLOSE ONE YESTERDAY.....Buju Banton

"This nine to five is a joke compare to the pressure
The minister say the economy is getting better
Misleading the people, the mass still suffer, oh Jah
Scarce benefits and spoils
Jah know that we feel it, day and night we cry, cry, cry
Jah know that we feel it, who can help a weeping soul like I"

Majuma kadhaa yaliyopita nilikuwa nikiwasiliana na Kaka Jeff Msangi wa BONGO CELEBRITY na katika mazungumzo yetu mema (kama ambavyo tumekuwa tukifanya mara kwa mara) tukagusia suala la UCHAGUZI TANZANIA na alizungumza jambo moja ambalo mpaka sasa linajirejea kichwani. Alisema "hata kama Dr Slaa hatashinda nafasi ya uraisi, atakuwa amewaamsha wengi". Nilikubaliana na bado nakubaliana na kauli yake japo wasiwasi ukaja kama MOTO ATAKAOUWASHA DK SLAA UTAENDELEA KUWAKA?
Ni nani alizima moto uliowashwa na Mrema mwaka 2005? Ni nani alizima moto wa Dr Lamwai bungeni? Na je aliouwasha Dr Slaa huko bungeni utaendelea "kukolezwa" na nani?
Nimekumbuka haya ndio maana nikaona niandike hapa siku ya leo.
Kinachoonekana sasa ni kuwa japo kwa mwendo wa kinyonga, wananchi wanaanza kutambua mahitaji na haki zao na wanaanza KUHOJI yale yaliyo muhimu na haki kwao. Swali ni kuwa, Je! wataendelea kuhoji haya?
Tunaona hili joto limeanza kuwawewesesha hata waliokuwa kwenye uongozi. Baadhi ya wananchi wameona wasipofanya maamuzi ya busara wataishia kuangukia patupu hivyo kuamua kubadili "wawakilishi" watarajiwa.
Tumeona hata chama tawala kinavyoanza kuweweseka na kufanya mambo yanayowafanya wengi kuwaza "kama ni hawahawa" tuwajuao
Labda ni kweli kuwa Dr Slaa hatashinda mwaka huu, labda ni kweli kuwa hatamuona rais wa upinzani akiingia madarakani katika uhai wake ama wetu, LAKINI KAMA TUTAFANYA LILILO SAHIHI, BASI MABADILIKO YATAKUJA.
Si unaona namna ambavyo waMarekani weusi hawakuona miaka ambayo wangeweza kuwa na ruhusa ya kushirikiana na wazungu, kusafiri pamoja na kupata haki za msingi kama kupiga kura ama kupigiwa kura?
Lakini sasa twaona namna ambavyo Rais wa nchi hii ana asili ya Afrika tena uzao wa kwanza wa ki-Africa.
Lakini twakumbuka "njia ilisafishwa" na kina nani? Wakumbuka bandiko langu la tarehe siku ya kuapishwa kwake Jan 20, 2009 niliposema A NEW DAY: Toka Frederick Douglas mpaka Barack Obama (irejee hapa)
Basi tuamini kuwa kila siku ichao yaanza na MABADILIKO MAPYA.
Mabadiliko chanya na yale "yatakayofunga' matatizo yaliyopita nasi siku ya siku tuje kushuhudia MCHAKATO WA MAENDELEO kutokana na uwepo wa uwiano mzuri serikalini.
Na juma hili tunaye Buju Banton akisema CLOSE ONE YESTERDAY. Sikiliza, soma, suatilia kisha JIFUNZE


One more day in the struggle
Have to get up and go juggle
Yu done know
Want a little sugar inna de pan
Me nah see fi trouble no man

Oh oh...

Said I had a close one yesterday
Jah put an angel over me, be strong
Hold a firm meditation
One day things must get better
Don't you go down
Keep your head above the water
Say, one day things must get better, be strong
Hold a firm meditation
One day things must get better
Don't you go down
Keep your head above the water
Say, one day things must get better

The rich is wise in his own conceit
But the fool with overstanding search him out
Poor man mourn the rich riches increase. I say
Be not grieved, riches are not forever
Envy not the oppressor chose none of his ways
Be not wise in his own eyes only Jah you must praise
Strive not with a man without cause
If he have done no harm let by gone be by gone

Said I had a close one yesterday
Jah put an angel over me, be strong
Hold a firm meditation
One day things must get better
Don't you go down
Keep your head above the water
Say, one day things must get better, be strong
Hold a firm meditation
One day things must get better
Don't you go down
Keep your head above the water
Say, one day things must get better

This nine to five is a joke compare to the pressure
The minister say the economy is getting better
Misleading the people, the mass still suffer, oh Jah
Scarce benefits and spoils
Jah know that we feel it, day and night we cry, cry, cry
Jah know that we feel it, who can help a weeping soul like I


Said I had a close one yesterday
Jah put an angel over me, be strong
Hold a firm meditation
One day things must get better
Don't you go down
Keep your head above the water
One day things must get better, be strong
Hold a firm meditation
One day things must get better
Don't you go down
Keep your head above the water
Say, one day things must get better

The rich is wise in his all conceit
But the fool with overstanding search him out
Poor man mourn the rich riches increase
Be not grieved, riches are not forever
Envy not the oppressor chose none of his ways
Be not wise in his own eyes
Only Jah you must praise
Strive not with a man without cause
If he have done no harm
Let by gone be by gone

Said I had a close one yesterday
Jah put an angel over me
Said I had a close one yesterday
Jah put an angel over me, be strong
Hold a firm meditation
One day things must get better
Don't you go down
Keep your head above the water
One day things must get better, be strong
Hold a firm meditation
One day things must get better
Don't you go down
Keep your head above the water
One day things must get better


**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

3 comments:

Simon Kitururu said...

Ijumaa njema Mkuu na asante kwa hii changamoto !Nakiri imenikuna kichwa!

Yasinta Ngonyani said...

MMMhh! ni jambo la kufikirisha na kufikiri... na ni changamoto kubwa sana Ahsante. Ijumaa njema nawe pia familia yako.

SN said...

Hata mimi najiuliza haya maswali. Tabia ya kuhoji na kuchambua mambo inajengwa kwa muda mrefu.

Binafsi nitasikitika kupita kiasi kama Watanzania wataacha kufuatilia na kuuliza maswali ya msingi baada ya Uchaguzi kupita. Sidhani kama matatizo ya elimu nchini yatakoma baada ya kupiga kura; kwahiyo watakaokuja inabidi waendelee kupewa changamoto na kuhojiwa.

Kwa maneno mengine, tujifunze kuhoji vitu mpaka vieleweke!

Tusubiri... Na wakati huo huo, watakaoshindwa itabidi waanze kujipanga upya -- tokea siku ambayo Rais anaapishwa, na sio miezi sita kabla ya Uchaguzi 2015.