"...leaders meditation is, total power, greedy, and selfishness. Dont really care about the hungry or the shelterless, much less the needier or the fatherless. They only using us as cones in their game of chess..." Morgan Heritage
Kama kuna kitu ambacho mTanzania ama waTanzania wengi wanakifanya sasa ikiwa ni juma moja kabla ya uchaguzi ni NDOTO. Na si ajabu kuwa watu wana ndoto ambazo hawawezi hata kuzikamilisha kwa kuwa WANATEGEMEA KILA KITU KITENDWE NA KIONGOZI.
Lakini labda ni kosa la kiongozi ambaye ANAWAPUMBAZA WANANCHI kuwa yeye ndiye suluhisho la matatizo yao na si sehemu ya suluhisho. Lakini pia wanapuuza ukweli kuwa wao VIONGOZI na WANANCHI ni sehemu ya matatizo yaliyopo. Hivi sasa twaona "mfuriko" kwenye kampeni za chaguzi. Twaona watu wakiwa na "jezi" za vyama zijazo mara moja kwa miaka mitano na cha ajabu wengine MAKAZI yao wanayapuuza. Kuna wakati huwa nawaza TUNAHITAJI KIONGOZI AJE "KUTUKANDIKIA" NYUMBA ZETU? Yaani mfano halisi ni huu hapa chini ambapo sioni kwanini hawa wetu wenye bashasha namna hii wanaishi mazingira kama hayo (ambayo ni mengi saana nyumbani)? Ni kweli kuwa TEGEMEO lao la maisha sasa ni Mbunge mtarajiwa? Wapo wasiotaka kufanya kazi wakitegemea kwa kubadili Rais ama Mbunge yataleta mabadiliko ya maisha. Labda ninaloweza kusema ni kuwa MABADILIKO MAKUU TUHITAJIYO NI YA AKILI ambayo yatawafanya wale waliopo ama wapya tuwawekao watambue nia ama mahitaji yetu.
La kukumbuka ni kuwa KABLA HAWAJAWA MADIWANI, WABUNGE ama hata RAISI, watu hawa huwa WANASIASA na sifa za mwanasiasa sote twazijua.
Lakini tukumbuke kuwa kama hatutabadili fikra, kama hatutajua kile tutakacho na tuhitajicho. Kama hatutakuwa wachapakazi na badala yake tukawekeza kwa hawa wanasiasa, tutaishia kukumbushwa yale aliyoimba Lucky Dube kwenye wimbo wake MONSTER kuwa kubadili mwanasiasa bila kuwawezesha ama kujiwezesha hakutasaidia kwani hawawezi kutimiza ndoto zetu za MAISHA BORA, ELIMU BURE, MLO KWA KILA MWANANCHI nk kwani hawa ni wanasiasa ambao anayetoka anaweza kuwa sawia na aingiaye kwani kwenye siasa "ONE MONISTER DIES, ANOTHER ONE COMES ALIVE."
Tumsikilize Philip Lucky Dube katika kibao hiki MONSTER kipatikanacho kwenye albamu yake ya mwisho kutoka akiwa hai. Albamu iliitwa RESPECT
I had a dream last night
One that will stay with me for a long time
One that will stay with me,
For as long as I live.
We were living in a world, there was no pain
We were living in the world there were no hungry people
Everyone was at peace with one another
There was a man in my dream
He told me he's from the future,
Coming to give something better x 3
Even though I that
Chorus
One monster dies another one comes alive.
I had a dream last night
It was my dream but I know it is a dream
Of a lot of people in the world
To be living in a world, with no homeless people
To be living in a world where little children
Don't have to die, because their parents are poor
When we came to this world
We were prepared to fight a battle.
But we found a war
When we came to this world,
We were prepared to fight demons
But we found the devil himself
There was a man in my dream he told me he's here
To gimme something better even though I know that,
Chorus
ONE MONISTER DIES, ANOTHER ONE COMES ALIVE.
Till fade.
**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment