Saturday, November 13, 2010

HONGERA TOVUTI YA BUNGE

Labda na nyingine za serikali zitaiga mfano huu....
UKURASA WA BUNGE
Nimekuwa mkereketwa mkubwa wa namna ambavyo tovuti za vyombo ama vitengo vya serikali zinavyopuuzwa na kutokwenda na wakati. Hili ni kuanzia Ikulu mpaka kwenye balozi zetu.
Aprili 19 nilipotoa maoni kwenye post hii ya Da Subi, nilisema "Ingia TOVUTI YA IKULU (http://ikulu.go.tz/)uone utakachokutana nacho. Anyway, hao wako busy, basi twende kwenye SHIRIKA LA UTANGAZAI TANZANIA (http://www.tbc.go.tz/)ambayo ilikuwa hewani kwa wiki moja baada ya hapo iko matengenezoni kwa miezi sasa. Who cares.
Lakini zinazofanya kazi nazo umeona updates zake? Angalia hii ya Idara ya Mawasiliano Ikulu (http://mawasilianoikulu.blogspot.com/)ambayo licha ya Rais ambaye ni msafiri kuliko uhitaji, bado updates zao ni za kusikitisha.
Anyway, labda hilo si tatizo. Kuna ambao wanaweka HABARI ZA UONGO. Kama nilivyoandika kwenye post yangu ya leo kuhusu tovuti ya UBALOZI WA TANZANIA HAPA MAREKANI. Nimeiona web yao baada ya kukutana na maelezo haya ya Uncle John Kitime aliyesema "Umekosa website za vichekesho? Basi google Tanzanian Embassy USA, kisha fungua ukurasa wa Embassy of Tanzania, fungua About Tanza...nia, halafu fungua People and culture hapo ndo utajua kumbe Ze Comedy wako wengi. Je ulijua kuwa Zouk na ndombolo ni tradional music wa Tanzania? Je ulijua kuwa Pilau kizungu ni wild rice? Je... ulijua chapati ni bread? Halafu kuna michapo mingine kuhusu mtunzi wa wimbo wa Taifa nk"
Isome hapa (http://www.tanzaniaembassy-us.org/tzepeo.html)
Labda nikwambie kaka kuwa ukitaka kujua yanakoanzia haya, basi angalia tovuti hizi za vyuo kama zilivyoelezwa na mdau hapa (http://issamichuzi.blogspot.com/2010/02/yaaawnnext-please.html)
NI MWENDO WA KINYONGA, LAKINI TUTAFIKA TUUUUU!!"

Lakini leo nilipokuwa nawasiliana na Kaka Jeff Msangi, tukajadili mawili matatu kuhusu Bunge na ndipo aliponijuvya kuhusu UFANISI WA KITENGO CHAO CHA SASA CHA MTANDAO.
Wamekwisha weka picha na taarifa za wabunge wote waliochaguliwa na pia hata za mkutano wa Mhe Spika baada ya kuchaguliwa upo.
Tatizo nililoliona na ambalo ningependa kuona waungwana wakilishughulikia ni mfumo wa kuyaandika majina. Mfano, wameandika Mhe. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI ambalo jina limeandikwa moja kwa moja kuanzia la kwanza mpaka la mwisho.
Kisha kuna majina kama Mhe. KAJUMULO TIBAIJUKA PROF. ANNA ambaye yeye wameanza na jina la kati kisha mwisho kisha cheo halafu jina la kwanza
na mwisho tuangalie la Mhe. FAUSTINE ENGELBERT DR.NDUGULILE hapa wameanza jina la mwanzo, kisha la kati halafu "cheo" kisha la mwisho.

ZAIDI YA HAPO PONGEZI KWENU
Hapo twategemea kuona "updates" za wasemacho, wasemapo na wasemavyo

ASANTENI NA HONGERENI KITENGO CHA TOVUTI YA BUNGE.

3 comments:

Faith S Hilary said...

At least something to count on maana itakuwa aibu mtu hata ukiulizwa jina la mbunge wa jimbo fulani hulijui, so hii ndio "Google" (The answer to everything - not really)

malkiory said...

Tovuti ya bunge linajitahidi kusema ukweli. Najua hata CV za waheshiwa zingishawekwa kama siyo wahusika wanachelewesha. Kwenye tovuti ya bunge lililopita baadhi ya wabunge na mawziri CV zao hazikuonekana kabisa bila ya maelezo yeyote. Nadhani ni jambo jema kwa watanzania kuelewa backgrounds za wabunge na maziri wao.

emu-three said...

Ngoja nami niifuate nione kilichomo, angalau nipate cha kusema