Friday, January 28, 2011

Them, I & Them...YOUTHS TODAY....MORGAN HERITAGE

Rais wa zamani wa Tunisia Zine al-Abidine Ben Ali
"...see someone looks a mountain top to run to, the mountain looks somewhere to run to. See someone run out of space, what a big disgrace"

Haya ndiyo maneno anayomalizia nayo Jah Petes wa Morgan Heritage kwenye wimbo huu YOUTHS TODAY. Wimbo una zaidi ya miaka 2, lakini athari ama yaliyoimbwa ndio twayaona sasa. Tumeona TUNISA ambako kujiunguza na kufariki kwa kijana mmoja kumesababisha Raisi ambaye analaumiwa kwa mengi kuondolewa madarakani. Sasa tumeona maandamano yakiamka Algeria, Misri na jana Yemen.
Nimekumbuka kurejea maelezo na mahusiano ya maudhui ya kibao hiki na maisha yetu ya sasa baada ya kuangalia hali ya sasa, kumuangalia KIJANA WA KITANZANIA na kurejea kusoma kwa umakini makala makini kwenye tovuti ya VIJANAFM.COM yenye kichwa cha habari Vijana wa Tanzania tuamke!(ipitie hapa). Nimesema MAKALA MAKINI na pengine ambayo kila kijana wa kiTanzania anastahili kuisoma na pengine kuuchukia ukweli wake ili aweze kuwa sehemu ya badiliko lihitajikalo. Ndugu watano (Nyuma L-R) Lukes, Gramps, Jah Petes (Mbele L-R) Dada yao Una na Mr Mojo Morgan wanaounda kundi zima la Morgan Heritage a.k.a ROCKAZ. Watembelee HAPA
Nimekuwa nikisema kuwa MPAKA KESHO ITAKAPOHESABIKA KUWA LEO, BASI VIJANA HATUTAENDELEA. Maana kubwa ya sentensi yangu ni kuwa mambo ya msemo wa VIJANA NI TAIFA LA KESHO hauna maana.
Msemo huu hauna maana kwangu kwa kuwa wazee wanaendelea kung'ang'ania madaraka mpaka vijana wanapoelekea kuuacha ujana na wakati huo ndipo tunapojikuta tumekosa la kufanya. Hakuna ubishi kuwa wazee wengi na hasa kwenye siasa za nyumbani wana uzoefu, lakini tusisahau kuwa "The trouble with experience is that by the time you have it you are too old to take advantage of it. " — Jimmy Connors
Ndio maana twaona namna ambavyo "wazee" wetu waliojikita kwenye siasa walivyoishiwa na kuanza kutetea yasiyo na maana na yasiyo na tija kwa taifa.
Ni wakati wa VIJANA KUAMKA NA KUANZA KUNYOOSHA MAPITO ya maumivu tunayopitishwa na "waheshimiwa" hawa.
Twaona ilivyo nchini kwetu na Afrika kwa ujumla jinsi vijana wanavyohangaika kwelikweli kutaka "kuiona kesho". Katika hili, tunawasikia Morgan Heritage katika wimbo wao YOUTH TODAY wakilizungumzia hili. Mfano ni hapa mwanzo ambapo Jah Petes anaimba namna ambavyo tunashuhudia yaendeleayo kuwakumba na kuwaathiri vijana bila kutafuta suluhisho anaposema "How much more do we need to see before we realize we all need to change our lives for the better world in this time? Now the time has come, let's not wait 'till it's gone. Don't wait too long".
Youths in TUNISA
Photo Credits:SkyNews.com Youths in Algeria
Photo Credits:AlArabiya.net
Youths in Egypt
Photo Credits:Ben Curtis / AP via Worldnews.com
Youths in Yemen
Photo Credits: TheState.com
Lakini Gramps katika ubeti wa pili anazungumzia maumivu / mateso ambayo vijana wanayapata kwa maamuzi ambayo hawakushiriki kuyafanya na kisha anahimiza kuwa hakuna wa kulamu bali kuamua na kuungana kuyafanyia kazi mabadiliko. Gramps ni kama anaona athari za yanayotokea katika nchi za Afrika, ambapo viongozi waliokalia madaraka kwa miaka mingi kuliko umri wa idadi kubwa ya vijana uwaonao hapo kwenye picha, wamefanya maamuzi yaliyowafanya vijana hao kuchoka na sasa wanaamua KUFANYIA KAZI MABADILIKO. Anasema "now the youth they feel the pain, for the choices made yesterday, there's no one out to blame we all have to work towards the change"
Basi ni wakati ambao lazima VIJANA TUAMKE na kuacha kutegemea waliopitiliza kwenye nafasi ambazo hawana uwezo wa kuzishikilia. Wanatapatapa na kuhaha na sisi (bila kujijua) tunatapatapa tukiwafuata wao. Hivi unajua athari ya kumfuata asiyejua aendako? Unajua anakoweza kukufikisha kama utaendelea kumfuata ilhali yeye anaendelea kukukimbia na kutafuta pa kujificha? Tunapowaona wao kama "milima" ilhali milima inatafuta bonde la kujificha (kwa kuwa wameshaishiwa) basi ujue TUNAAIBIKA. Ndio anayofungia nayo Jah Petes anaposema
"see someone looks a hills to run to,
the youths a look somewhere to run to,
see someone looks around to run to,
the ROCKAZ looks somewhere to run to,
see someone looks a mountain top to run to, the mountain looks somewhere to run to. See someone run out of space, what a big disgrace"
Wasikilize Morgan Heritage hapa katika kibao chao mwanana YOUTH TODAY kipatikanacho katika albamu yao waliyoiita MISSION IN PROGRESS

**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

3 comments:

emu-three said...

UJUMBE MURUA MKUU, LAKINI JE..UTAWAFIKIA WALENGWA, NA UKIWAFIKIA UTASOMWA, NA UKISOMWA ...E KWELI UTAFANYIWA KAZI...sijui, naona kwenye chini yetu bado ni ndoto...angalia sasa DAR IMEGEUKA KUWA GIZA...NANI ANASEMA KITU, KIMIYAAAA..WENZETU MKATE UNAPANDISHWA BEI, VIONGOZI WANATAFUTANA...LEO HII GIZA TOTORO...VIJANA WAPO!

chib said...

Nimekupata vyema Mzee wa Changamoto

SN said...

Tokea siku ya pili ya yale maandamano nimekuwa nafuatilia kila kinachoendelea. Ukisikiliza mawazo, mitazamo ya vijana waliokuwa wanalala Tahrir, lazima utikise kichwa; yaani itikadi zao zinaambukiza sana.

Bahati nzuri, sio propaganda tu. Wanaona mbali -- maumivu wanayopata sasa hivi inamaanisha watoto na wajukuu zao wataishi vema kwa amani miaka 50 baadae.

Nadhani tukishaanza kufikiria na kujipanga kwa ajili ya maisha zaidi ya miaka 10-20 baadae, basi ndio hapo tutapoamka.