Tuesday, February 8, 2011

Familia huishia wapi?


Tumezaliwa watano. Nina dada wakubwa waili na Kaka wadogo wawili. Yamaanisha ni mimi niliye kati. Na sina shaka kuwa wengi tutakubali kuwa hii ni familia. Na kama ambavyo nilishasema, nafurahia saana uhusiano tulio nao baina yetu. Lakini pia kuna Baba na Mama. Nao naamini tutawahesabu kama familia. Nao kila mmoja ana ndugu zake waliozaliwa pamoja. Hao kwao ni familia. Ni kwa mamtiki hiyo nahisi kuwa nao ni familia yetu maana ni familia ya sehemu ya familia yetu. Sasa mjomba na Shangazi wote si wana familia katika miji yao? Na hao ni familia za wazazi wetu na sisi na wazazi ni familia. Ina maana nisiwaite familia?
Najiuliza kama sisi sote si familia kwa mwendo huu na kama sivyo, basi basi naendelea kujiuliza kuwa hivi familia huishia wapi? Ama niseme mtu ni ndugu yako mpaka uzazi upi?

6 comments:

Anonymous said...

Kweli swali lako linaleta mkanganyiko kidogo,maana mambo ya familia yana mlolongo mrefu. Kwa familia za Kiafrika utakuta uhusiano unaendelea tokea kwa babu mpaka kitukuu,ambayo inajumuisha ndugu wote ulowataja.
Wenzetu wa Magharibi wanatukosoa eti familia za hvyo zinasababisha uzembe na utegemezi.
i.e. 'Extended family is caused by lazness of family members'

emu-three said...

Mhh hoja yako mkuu inanipeleka enzi za `ADAMU NA HAWA'
Wao ndio chimbuko letu, wakazaa, ikaeenda weeeeeeeeeeeeh, oh hadi tukapataikana sisi.
Sasa huu unaoitwa mti wa familia, toka unaowaona ukaazaa, wakaazaa...watazaaa, na hata mwisho wewe hawatakujua tena, au kujuana familia ilipotoka, kwasabau kubwa hatuna utaratibu wa kuweka kumbukumbu za kifamilia, ili waje wengine baadaye watukumbuke: TUMETOKA KWA UDONGO TUTAREJEA MAVUMBINI!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

we enedelea kujiliza. ila sasa familia karibia zote kama ulivyozisema huishia kwenye migogoro, kutoelewana na kutafutana

familia ni zaidi ya hiki unachokitaja

Unknown said...

Hatimaye huishia mautini hiyo Familia ila kila mmoja ndani yake kwa wakati wake mavumbini hurudi.

Kwa nini nimesema hivi, mlolongo wa historia ya binadamu kwa mujibu wa vitabu vya neno la Mungu ina tanabaishwa hivyo.

Ukifuatilia tangu mwanzo wa kuumbwa kwa mwanadamu mpaka leo hii jibu la FAMILIA HUISHIA WAPI litakuwa bayana. MLITOKA MAVUMBINI NA MAVUMBINI MTARUDI.

Emmanuel said...

Katika hili mimi nina haya tu tu. Familia haina mwisho. Anayesema huishia kwenye mgogoro siamini maana kama kweli wewe ndugu yako anafanya vibaya utakuwa unaumia hata kama unajifanya huhusiki. Pili familia nyingi za kiafrika zinanufaika na kitu kimoja kinaitwa "social wealth",kusaidia na kufarijiana. Wenzetu wa magharibu wana "material wealth" ambayo inamsaidia mtu mwenyewe labda na wale wachache na sio zaidi. Na ukiwa msumbufu sana hata kama ni mzazi hawachelewi kukumalizia ili wao waendelee kuponda raha. Wengine wanashindwa wafanye nini, wana pesa lakini hawapata faraja katika jamii. Hiki cha mwisho waafrika tunayo sana. Suala la uzembe pia ni kubwa sana kwetu, sina kipingamizi na siwezi kutetea. Unaturudisha sana nyuma. Lakini, mabadiliko yapo na tutaweza. Tuendelee kujiuliza na kutafakari zaidi

Rachel Siwa said...

mmmhhh kaka umwewaza kweli hata mimi sina jibu la hilo, nafurahi kusikia maoni ili nijifunze. Ahsante kaka Mubelwa kwa mada hii!!!!!!!.