Thursday, February 10, 2011

ELIMU...Labda ni UJINGA BINAFSI unaoendekeza UBINAFSI

Ikiwa utaweza KUSOMA hapa, na pengine kuamua kama utakalosoma ni BUSARA ama UJINGA, basi ujue kuwa nawe umepitia ama kupata ELIMU.
Na kama UMESOMA na kufikia kiwango ch kutotambua kuwa uwazalo wewe ni UJINGA na si lile awazalo umdhaniaye kuwa mjinga, basi ujue kuwa nawe UMELIMIKA.
Kwani....Elimu ni nini? Ni kusoma na kuandika?
Malcom Forbes aliwahi kusem kuwa "Education's purpose is to replace an empty mind with an open one."
SWALI HAPA NI KUWA UNA-REPLACE NA OPEN MIND ILI IJE KUJAZWA NA NANI?
Kwaniiiiiiii....... Umeshawahi kumsoma "MZEE WA UJINGA-BUSARA" (hapa) kisha ukaamua kama kila aandikalo ni UJINGA ama BUSARA ama VYOTE? Haijalishi umewaza nini, kama UMEMSOMA basi utambue kuwa UNA ELIMU (japo elimu ya awali kuweza kusoma) na pia kama ameweza kuandika ujue kuwa naye ANA ELIMU kwani anastahili kuwa na elimu kuweza kuandika.
LAKINI matumizi ya ELIMU ni yapi?
ELIMU ni ile inayomuwezesha mtu kuisaka amani kwa kutumia vita?
ELIMU ni ile inayomuwezesha mtu atengeneze "zana kali" za vita zinazoweza kuua watu wengi kwa mkupuo na kuwatisha wengine?
ELIMU ni ile itakayomuwezesha aliyenayo kujikinga na mizinga na zana kali za minzani wake?
Wcha nikurejeshe kidoogo katika ANDIKO lake Kaka Ndesanjo Macha kuhusu ELIMU YETU, ELIMU KWETU NA ELIMU KWA WENZETU.
Katika makala aliyoyatoa nami kuyanukuu HAPA, akasema "wakoloni walipokuja hawakuchimba kwa undani falsafa na tamaduni zetu. Na wale waliofanya hivyo, walishindwa kutuelewa kwa undani maana, kwanza walikuwa wanatudharau sana, na pili, walikuwa wakiamini kuwa tamaduni zao zilikuwa ni bora zaidi. Wao walikuwa wastaarabu na sisi tulikuwa ni washenzi.
Kwa kuwa waliamini kuwa tamaduni zao ni bora walitumia silaha mbili kuu za kufunga watu minyororo ya utumwa wa akili: elimu na dini. Wakatumia elimu na dini kutusahaulisha yote tuliyokuwa tumerithishwa. Historia yao ikawa ndio yetu. Utamaduni wao ukawa wetu, imani zao zikawa zetu. Watakatifu wao wakawa watakatifu wetu. Kumbukumbu zao zikawa kumbukumbu zetu. Urithi wao ukawa ndio wetu."
Lakini narejea kujiuliza ELIMU NI NINI? ALIYEELIMIKA NI NANI? NA NI KWELI KUWA ELIMU IMFAAYO MTU WA MAGHARIBI NDIYO IMFAAYO WA MASHARIKI?

Labda ni UBINAFSI ambao unamfanya MJINGA kujiona ana ELIMU kwa kupuuza kujifunza (japo) kile aaminicho kuwa ni UJUNGA wa mwenzake.

Labda ni namna nionavyo tatizo, na pengine hilo ndilo tatizo.
Nawaza kwa sauti tuuuu!!!!!!!!!!!!!! (Thinking Out Loud)

2 comments:

Simon Kitururu said...

Mmmmh!

emu-three said...

Mhhh, kuna jamaa alisema kuwa `kama ukiwa mdadisi sana kwa kila kitu mwisho wake `utakosa yote'
Kuna kisa kimoja jamaa waliambiwa kuwa ili wafaulu katika matatizo yao inabidi watafute ngombe...
'Mmoja akaluliza ngombe huyu mweupe au mweusi' akajibiwa mweupe.
'Mzee au ...'
Akaibiwa asiwe mzee au wakawaida, awe wa kati na kati na kati...
Maswali yakaendelea kiasi kwamba, huyo waliyekuja kuambiwa baadaye ikawa vigumu kumpata...
Ina maana walivyoambiwa ng'ombe, wangelichukua ngombe yoyote atakayetokea karibu yao angekubalika! Lakini wakajiongezea uzito wao wenyewe kwa kuwa wadadisi!
Je udadisi huu ndio elimu? Na je walikuwa na makosa?
Elimu sasa ina-udadisi mwingi...ukiangalai somo la sayansi kwa mfano, limegawanyika katika nyanja mbalimbali...biolojia, kemia fiskia, na humo ndani katika kila nyanja kuna vipengele...najiuliza KWANINI...NDIO KWASABABU KICHWA CHA BINADAMU KIMEJAA UDADISI, NA mara nyingi udadisi huu unafikia hata `kutaka kumjua MUNGU YUKOJE? kwanini alituumba hivi isiwe hivi...tunajichubua, tunafanya mengi ya ajabu...HAYA YOTE NI ELIMU?
Mhhh, elimu ni kujua `kitu kipya' na hicho kitu kiwe na manufaa kwako na wengine. Na kuyajua mzingira yako na jinsi ya kupambana nayo, kiurahisi ...au na muendelezo wake....lakini kama elimu hiyo itakuwa ya `kuharibu' mmmmh, nina mashaka nayo...utauliza huyu aliyetengeneza bomu la nyukilia alikua hana `elimu'...anayo, lakini sio nia yake `kuangamiza'...naona niishie hapa kwani nitakuwa `mdadisi'a mwisho wa siku nitashindwa ....