Sunday, February 27, 2011

Kuwezesha chanzo cha tatizo ili kupata suluhisho?..Kwanini????

DAWA YA MOTO NI MOTO.... PHOTO CREDITS: CNN.com
Si ndio WAHENGA (wanaopingwa na Kaka Kamala) walivyosema? Basi kuna ambao wako tofauti kidoogo na Kakangu Luta Kamala ambao wanaamini kuwa unaweza kuzuia vurugu kwa kuwekeza katika chanzo cha vurugu. Mmmmhhhhh!!!!!!!!!!!
Yeah... Majimbo mawili hapa nchini Marekani yako kwenye mjadala mnono wa kuwawezesha wanafunzi na waalimu wa vyuo vikuu KUJILINDA KWA KUINGIA MADARASANI WAKIWA NA BASTOLA.
MJADALA HUU WA TEXAS na HUU WA ARIZONA yaonekana kuzidi kuchukua taswira mpya kila uchao kutokana na BIASHARA ya silaha kuwa kubwa hapa nchini, suala zima la HAKI YA MSINGI YA RAIA KUJILINDA na pia kutokana na matukio kadhaa ambayo yamekuwa yakijitokeza kwenye shule na vyuo kadhaa hapa nchini.
Lakini nawaza kuwa hawa wanaoamini kuwa kila mwanafunzi na mwalimu akiwa na silaha ndio kutakuwa na usalama WANAWAZA NINI?
Nawaza kama watu wenye matatizo ya kushindwa kuzuia hasira zao watakuwa ni sehemu ya usalama ama hatari vyuoni?
Vipi wale wanaochukia watu na kufanya maamuzi ya papo kwa hapo?
Na ile sheria ya "kuua kwa kutokusudia" kwa kuwa umeua ndani ya muda mfupi wa kukerwa itakuwaje hapa?
Maana ukimuudhi mtu hahitaji kwenda mbali kutafuta silaha (ambapo mwendo huo waweza kumfanya awaze mara kadhaa juu ya kile anachotaka kufanya), bali ni kuingiza mkono mfukoni na kufyatua.
Mmmmmmmhhhh!!!
Vipi kuhusu suala zima la shabaha? Vyuo vina maelfu ya wanachuo, na kama kila mmoja atajaribu kumlenga mmoja anayetaka kuua watu, na shabaha isiwe sawia, nahisi "waokozi watauana na kuua watu wengi kuliko ambavyo mmoja anayezuiwa angeua"
WALIOFIKIRIA HILI KUWA SULUHISHO WALIWAZA NINI?
Achana na hao....
Jana nilitumiwa ujumbe huu wa barua pepe na rafiki yangu aliyeweka maswali kadhaa ya KWANINI?
Na alinifanya NIWAZE ZAIDI YA KUCHEKA na kuwaza ALIYEANDIKA HAYA ALIFIKIRIA NINI?
Labda kuna ukweli (yawezekana usiuone kulingana na mazingira) lakini FIKIRIA FIKRA ZA MWANDISHI....ALIWAZA / WALIWAZA NINI?
PHOTO CREDITS: Kinesis Marketing UK
.Why do supermarkets make the sick walk all the way to the back of the store to get their prescriptions while healthy people can buy cigarettes at the front?
.Why do people order double cheeseburgers, large fries, and a diet coke.
.Why do banks leave vault doors open and then chain the pens to the counters.
.Why do we leave cars worth thousands of dollars in our driveways and put our useless junk in the garage.
EVER WONDER ...
.Why the sun lightens our hair, but darkens our skin?
.Why can't women put on mascara with their mouth closed?
.Why don't you ever see the headline 'Psychic Wins Lottery'?
.Why is 'abbreviated' such a long word?
.Why is it that doctors call what they do 'practice'?
.Why is lemon juice made with artificial flavoring, and dish washing liquid made with real lemons?
.Why is the man who invests all your money called a broker?
.Why is the time of day with the slowest traffic called rush hour?
.Why isn't there mouse-flavored cat food?
.Why didn't Noah swat those two mosquitoes?
.Why do they sterilize the needle for lethal injections?
.You know that indestructible black box that is used on airplanes? Why don't they make the whole plane out of that stuff?!
.Why don't sheep shrink when it rains?
.Why are they called apartments when they are all stuck together?
.If flying is so safe, why do they call the airport the terminal?

***"Waliwaza nini ni kipengele cha kuelimishana tukifurahia. Hiki kitakuwa kikikuletea habari za kweli na kushangaza kuhusu watu ambao wamefanya yale ambayo unaweza kujiuliza kuwa WALIWAZA NINI? wakati wanatenda haya.
Kitakuwa na habari fupifupi kutoka ulimwenguni kote. Kwa habari zaidi kuhusu kipengele hiki
BOFYA HAPA"***

8 comments:

Albert Kissima said...

Dah! Hii ya walimu na wanafunzi na namna yao ya kujilinda; ni la aina yake kwa kweli, pengine labda "namna walionavyo tatizo, ni tatizo" kwani badala ya kutatua naona mbinu hiyo inaongeza makali ya tatizo. Itafikia mahali watu watajilinda na Ak47(ndio hivi kweli!!!?) na hata na mabomu. Lakini yote ya yote, bado nawaza pia kuwa wanaoshadia mbinu hii WALIWAZA NINI?

Huyu aulizaye maswali naye kuna kitu/vitu aliwaza. Sipati picha nini kilimsukuma hadi akaamua kuwaza hivi. Swali lipo pale pale kuwa huyu ndugu ALIWAZA NINI hadi akaamua kuwaza hivi?

Kwani na huyu aliyeweka kipengele hiki cha WALIWAZA NINI, unafikiri naye aliwaza nini eti?:-)

Anonymous said...

mzee wa changa moto unafanya vizuri sana lakini siunajua sio woote waoingia katika glob yako english inapanda unajua wengine waliogopa umande kwahiyo jaribu tu kutafsiri kwa kiswahili wengine tupatekujua kinachoendelea ulimwenguni napenda sana kuingia ktk blog yako lakini kiinglish kinanipiga chenga ni hayo tu mkuu mungu akubariki sana uendelee kutuabarisha

Mzee wa Changamoto said...

Ndugu zangu Albert na Anon, kwanza niwashukuru kwa kutembelea hapa. Kisha nishukuru kwa kutumia muda wenu kusoma na pia kutoa maoni. NINATHAMINI SAANA HILI.
Kaka Albert, mara zote huwa una changamoto kali. ASANTE
Ndugu yangu Anon, ni kweli kuwa si wote wanaelewa kiingereza. Nami huwa najaribu kutumia kiSwahili fasaha pale niwezapo. Lakini kwa hili sikutaka kubadili lililoulizwa kwa sababu ya ugumu wa lugha na maana na pia kubakisha hali halisi iliyozungumzwa. Lakini sasa kwa manufaa ya wale ambao umewasemea, nitajaribu kutafsiri. NASISITIZA KUWA HII SI TAFSIRI RASMI. Na naomba mwenye maneno m'badala ama sahihi zaidi anisaidie.
Yaliyoulizwa hapa ni

• Kwanini Supermarket zinawafanya wagonjwa watembee mpaka nyuma ya majengo yao kununua dawa ilhali watu wenye afya wanaweza kununua sigara mbele ya jingo hilo?
• Kwanini watu wanaenda kununua vyakula (vinavyosemekana kuwa vya afya kama) doublecheeseburger, na chips (viazi vya kukaanga) na kasha kuagiza kinywaji cha Diet Coke (ambacho ni kati ya Coka cola zinazosemekana kuwa za “afya” zaidi)?
• Kwanini benki zinaacha milango wazi kasha wanaweka kamba kwenye peni katika kaunta zao?
• Kwanini tunalaza magari yaliyo na thamani ya maelfu ya dola kwenye veranda za maegeshi na kuweka mifuko ya taka ndani ya nyumba?
UMESHAWAHI KUJIULIZA….
• Kwanini jua linafanya nywele zetu zipauke, lakini linafanya ngozi zetu kuwa nyeusi?
• Kwanini wanawake hawawezi kupodoa macho na nyusi wakiwa wamefunga mdomo?
• Kwanini hujawahi kuona kichwa cha habari kikisomeka “Mtabiri ameshinda Bahati Nasibu”?
• Kwanini “kifupisho” ni neon refu?
• Kwanini kile kinachofanywa na madaktari (matibabu) huitwa ‘mazoezi’?
• Kwanini juisi ya limao hutengenezwa kwa kemikali za kuweka ladha ilhali sabuni ya vyombo hutumia limao halisi?
• Kwanini mtu anayewekeza pesa yae yote huitwa ‘broker’ (ambayo inaweza kutafsirika kama kuchacha)
• Kwanini muda wa siku ulio na msongamano mkubwa wa magari unaitwa rush hour (ambayo kwa tafsiri ya neon hilo waweza kusema muda wa kuwahi)
• Kwanini hakuna chakula cha paka chenye ladha ya panya?
• Kwanini Noah hakuwapia makofi wale mbu wawili? (Hii wala sijaielewa na mimi)
• Kwanini wanachemsha sindano wanazotumia kuchoma dawa ya kuua?
• Unajua kile kisanduku cheusi kisichoharibika kinachotumika kwenye ndege? Kwanini wasitengeneze ndege nzima kwa kutumia malighafi inayotengeneza hicho kisanduku?
• Kwanini kondoo hanywei inaponyesha? (hapa pia sijaelewa)
• Kwanini wanaziita apartments (nyumbani tunaziita flat) wakati “zimepandanishwa”?
• Kama usafiri wa anga ni wa salama, kwanini vwanja vya ndege vinaitwa terminal (neon ambalo moja ya maana yake ni “kisababishacho kifo”)?

NAAMINI NIMEJARIBU KUKIDHI MAHITAJI YAKO NDUGU YANGU.

emu-three said...

Hii jamani haiji, wanachukulia moja kwa moja usemi usemao, dawa ya moto ni moto...Naogopa kuwa viongozi wetu wanaweza wakaiga hili,...Mungu aupushilie mbali!
'Kwanini, kila kitu tuige, ina maana sisi hatuna akili ya kufikiri'
'Kwanini kila kizuri ni kile kinatoka `majuu' ina maana sisi hatuwezi!
Ni hayo tu mkuu kwa sasa

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

eti kuna haki za binadamu zinazozuia raia wote kuuwawa! ndo maana mataifa ya kiislamu yamekataa kuondoa sheria ya kifo wakati watu wanamiliki viuwavyo

Simon Kitururu said...

Rasta umeniwazisha yani! Wee achatu!:-(

Unknown said...

Tunaweza sasa kujimudu kama kila tulilokuwa tunaambiwa ni bora, ili mradi litoke magharibi, watu wengi walilikubali na kuliingiza katika mfumo.

Ayi Kwei Armah, alisema tena linaingizwa hata kama wanasiasa hawajalielewa vizuri. Nasema hivi kwa sababu;

Jambo jipya linaletwa na nchi zilizoendelea (nchi za magharibi) Lakini wanatulazimisha sisi wananchi tulipokee. Kushinikizwa tuukubali ushoga ama na mambo mengine ni matokeo ya tabia ya kukubali kwetu kila kitu.

Hasara ya Mwafrika wa leo na Mtanzania ni kukosa anachoweza kujivunia kama itikadi yake, elimu yake, dini yake, mila na desturi yake: Mwafrika anaonekana akiwa mbioni kuukimbia utu wake, na kila kinachofungamana na hicho eti afananane na umagharibi.

Wamagharibi wamefanikiwa kutufanya nusu watu!!

VIJANA wanawaza umasikini kila kukicha na ukomo wa fikra zao utawadia pindi utakapoisha kabisa ama kupungua kama watunga sera, wanasiasa na viongozi wa Serikali wanavyodai kwa mitazamo yao kuwa ipo siku lakini isiyojulikana kwamba itawezakana fikra na umasikini wenyewe kukoma ama kutoweka!

Hawaishii kufikiri peke yake imefikia hatua wamechanganyikiwa, wanaota umasikini na mwishowe wanajipa matumaini kwamba kama raha inaisha, basi shida nayo itaisha.

Kabla sijaendelea, natanabaisha tofauti za fikra kati ya mtu tajiri na mtu masikini.

Hakuna ubishi kwamba wakati masikini anawaza jinsi ya kujinasua katika hali aliyonayo, tajiri anafikiria jinsi ya kujiongezea rasilimali na wakati mwingine hata umaarufu.

Rachel Siwa said...

mmmhhh hii inatisha sasa!