Maisha ya sasa yanakwenda tofauti na wengi tulivyotarajia. Maisha yamegeuka na si katika imani baina ya watu, bali uchumi na nyanja ama niseme sehemu nyingine nyingi. Watu wamekosa amani ndani mwao (ndani ya mioyo yao), wamekosa amani ndani ya familia zao, wanakosa imani kwa jamii yao, kwa viongozi na hata ulimwengu kwa ujumla. Lakini haya si mageni na wala si kitu kipya masikioni mwa wengi. Hali hii yaweza kuwa mpya maisha mwa wengi maana wamekuwa wakisikia yakitokea kwa wengine na hivyo hawakuweza kuhisi ugumu wake halisi.
Lakini haya ni mabadiliko ya nyakati, na hili laweza kuwa funzo kuwa tujaribu kugeukia pale ambapo tunaamini ndipo palipo na uwezo wa kutufanikisha katika haya yote. Nako ni kwake MUNGU.
Wimbo wa leo ni kuhusu hilo ambapo mwimbaji Dada Comfort Osei-Wusu anatukumbusha kuwa kila kitu kina nyakati. Kama ilivyo kkatika kuzaliwa na kufa, kupanda na kuvuna, hivyo muda / wakati wa kupata amani halisi ni sasa na amani hiyo yapatikana kwake MUNGU.
Msikilize Lady Comfort katika wimbo huu TIME CHANGES uliobeba jina la albamu yake TIME CHANGES
>Nami nakwambia kuwa kila jambo lina mwisho, na "mwisho wa bonde ni mwanzo wa mlima kukupeleka kileleni" NEVER GIVE UP
JUMAPILI NJEMA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
2 comments:
hakika kila kitu na wakati wake. jumapili njema kwako pia familia yako.
Kinachonivutia zaidi ni namna unavyopenda reggae.
Post a Comment