Sunday, June 26, 2011

Unapowaza "kisicho halali" kama njia halali ya kupata "kilicho halali"

Photo Credits: Yahoo! News
Kwa wale watembeleaji wa blogu hii kwa muda mrefu kiasi, watakumbuka bandiko hili nililoeleza kuhusu hali ambayo niliamini kuwa Mimi na yeye sote tuko sahihi. Na sote hatuko sahihi. Nilizungumzia tatizo la gharama za afya hapa Marekani hasa kama huna bima ya afya. NI AGHALI SANA.
Wiki hii nikakumbana na habari ya Bw James Verone (pichani juu) ambaye baada ya kuwa na maumivu kwa muda mrefu, aliamua kutafuta namna ya kupata matibabu na pale alipokosa namna HALALI ya kupata HUDUMA HALALI YA AFYA, akaamua kufikiria njia inayoaminika na kuchukuliwa kama SI HALALI. Ya KWENDA KUPORA BENKI. Lakini dhamira haikuwa kuondoka na pesa, bali kutenda kinachoonekana kuwa ni kosa ili apelekwe jela ambako kwa mujibu wa sheria anastahili kuhudumiwa na serikali. Hivyo akaenda benki na kumpa mhudumu wa benki "note" kwamba anataka DOLA MOJA. Kama ilivyo katika taratibu za uporaji wa benki, mhudumu akaita polisi wakati "Babu" akisubiri kukamatwa. Verone ananukuliwa akisema "I told the teller that I would sit over here and wait for police."
Ni kweli. Alikamatwa, akapelekwa jela ambako amesema kama hukumu yake haitakuwa kali, basi atamwambia jaji kuwa atarudia kufanya alilofanya.
Lakini "mpango wa awali na mkuu" umeshaanza kuonekana kufanikiwa. Tayari Verone ameonana na nesi na alikuwa amepangiwa kuonana na daktari Ijumaa iliyopita. Anataraji kuonana na daktari hivi karibuni kutibiwa mgongo na kifua vinavyomsumbua na kisha kutumikia kifungo chake mpaka atakapotoka ambapo anaamini utakuwa ni muda wa yeye kuanza kukusanya mafao yake ya uzeeni.
Kwenye bandiko hili niliwahi kuandika kuhusu wimbo wa Lucky Dube uliokuwa ukiuliza "Do you wanna be a Well-fed slave or a hungry-free man?". Katika wimbo huo, Lucky Dube aliuliza
"What is the point in being free when you can` t get no job?
What is the point in being free when you can` t get food?
What is the point in going out to work when others can get for free?
What is the point in being free when you don` t have no home?
Now you` ve heard it all it is time to make up your own mind.
To be or not to be........
Do you wanna be a well fed slave or a hungry free man"

Pitia usome na uwaze.
Kusoma habari kamili ya "mpango" wa James Veron, BOFYA HAPA ama ANGALIA VIDEO YA MAHOJIANO YAKE.

Swali pekee ninalojiuliza ni kuwa ALIWAZA NINI? Na pengine ni wangapi wanaowaza awazavyo yeye?
NAWAZA KWA SAUTI TUUU!!!!!!

***"Waliwaza nini ni kipengele cha kuelimishana tukifurahia. Hiki kitakuwa kikikuletea habari za kweli na kushangaza kuhusu watu ambao wamefanya yale ambayo unaweza kujiuliza kuwa WALIWAZA NINI? wakati wanatenda haya. Kitakuwa na habari fupifupi kutoka ulimwenguni kote. Kwa habari zaidi kuhusu kipengele hiki BOFYA HAPA"***

2 comments:

Simon Kitururu said...

Kibano kikizidi akili ya tatuzi hujitokeza pia!

Thomas said...

kwa hapa bongo hayo ndiyo maisha yetu TUNAWAZA NA KUFANYA VISIVYO HALALI ILI TUPATE VILIVYO HALALI na hali ya hapa kwetu ndiyo imeturazimisha kuishi hivyo na tunafanya hayo huku nafsi zikitusuta,