NB: MARUDIO YA MWAKA JANA......
Ni wakati ambao tunatakiwa kuhakikisha kuwa HATUENZI MASHUJAA KWA STAILI AMBAYO TUMEIIGA KUTOKA KWA WALE AMBAO "MASHUJAA" WETU WALIPIGANA NAO KUWAONDOA NCHINI.
Mimi namuangalia(ga) tuuu.....
Mhe. Rais. Ni lini mara ya mwisho ulitoa hotuba yenye kuwataja mashujaa utakaowataja leo? Siku ya mashujaa mwaka jana eeeeeee? Ok!
Leo (Julai 25, 2011) ni
SIKU YA MASHUJAA NCHINI TANZANIA.
Siku hii INAKUMBUKWA kuliko KUENZIwa, jambo ambalo si geni kwa TANZANIA YANGU, kwani hata siku ya uhuru ni vivyo hivyo. Niliandika
HAPA, kwamba naiona kama SIKU YA UHURU INAYOSHEREHEKWA KWA STYLE YA KI-TUMWA. Na nina sababu kadhaa za kuona kuwa namna tunavyosherehekea siku hii (ambayo tunastahili kuiadhimisha) ni DHIHAKA KWA MASHUJAA WA KWELI.
Kwanza ninawaza kuhusu TAFSIRI YA SHUJAA WA TANZANIA.
Ni nani?
Aliishi lini (kama haishi sasa)?
Alitengenezwa ama anatengenezwa vipi?
Kituo cha Televisheni cha History channel wana kauli mbiu isemayo "HISTORY. MADE EVERYDAY". Ninalowaza ni namna ambavyo tunasherehekea siku ya mashujaa ilhali hatuna mashujaa wajao.
Kwenye picha hapo juu wamuona Rais Kikwete katika moja ya "sherehe" nyingi za mashujaa nchini ambazo amehudhuria na kufanya kile ambacho anastahili kufanya, na kisha kuondoka.
KWANI SHUJAA WA LEO HII NI NANI?
Je ni mwalimu kama
Mwalimu huyu Leziel Gowele ambaye alikuwa mwalimu pekee katika shule ya sekondari ya Makonde wilaya ya Ludewa mkoani Iringa?

Je, ni d
ada zetu wanaolea watoto watukutu wa VIONGOZI wetu? Ambao HAWANA MIKATABA YA KAZI, wananyanyaswa, wanabakwa, wanapuuzwa, mishahara midogo na kazi nyingi. Ambao wamelea wengi wa VIONGOZI WETU wa sasa na bado wanaendelea kutothaminiwa na kuitwa ma-house girl? Kama huelewi karaha za maisha yao, TAZAMA VIDEO HII hapa chini
5 comments:
Hii ndiyo Tanzania. pengine tungeacha kutumia pesa nyingi kwenye sherehe za mara moja kwa mwaka na badala yake kuboresha hali halisi za mashujaa wetu.
kule kwa Mjengwa kuna picha ya askari waliopigana vita ya pili ya dunia. ukiwatazama utaona dhahiri jinsi maisha yao yalivyo duni. unadhani serikali ingeamua kuyaboresha maisha yao kwa kupunguza gharama zake zisizo za lazima ingeshindwa?
nadhani bado hatujajua nini kipewe kipaumbele zaidi ya kingine.
Mwalimu Nyerere alipata kusema, KUPANGA NI KUCHAGUA......
nasi tumechagua haya tunayoafanya sasa.
hata wewe ni shujaa ndugu. una ushujaa wako niliwahi kukwambia via Face book
Shujaa ni yule alieteseka kwa kutete haki za binadamu, kutete umma na waliopigania nchi yao, kwa mitutu ya bunduki,alienyanyaswa na akanyanyasika, chukua mfano mzuri wa Martin luther king jr, Role in the Civil Rights Movement, ambae mpaka wamemuuwa kwa ushuja wake, tumuangalie, Mandela spent twenty-seven years ndani ya jela huyu unaweza kukwita Shujaa.. Malcolm X. shujaa, Paul Bogle, Marcus Garvey, chukulia mifano ya hao wazee then ndio umwite mtu shujaa!... Uswahilini kuna vituko sana na naona mwisho Hasheem thabeet mtamwita shujaa lol
Hizi siku-kuu bwana, ni namna ya kujitambuslisha, ni mambo ya kisiasa, labda ingelikuwa na tifa fulani.
Mimi kwanza najiuliza kwenye sherehe kama hizi mambo ya chama yankujaje?
Pili kuwaenzii mashujaa, natumai ingekuwa ni moja ya kuiita historia, vizazi vyetu vikajua, mfano, kuwa na matukio yanayoivuta jamii, ili wawe makini kujua nini kinaendelea.
Wenzetu wanawake makombe ya mpira, ambayo yanakutanisha mataifa mengine, sasa kwa hili utawavuta Watanzania kuuliza kulikoni.
Wengi tusiofuatilia matukio, na hatujui historia,hatukujua kabisa kuwa kulikuwa na sherehe kama hiyo..
Swali linabakia ni NANI SHUJAA WA NCHI, MPAKA TUMSHEREHEKEE, tukumbuke kuwa kuna wanavijiji wanaishi kwa mlo mmoja kwa siku, ...sio wanakijiji, raia wemma..hawa ni mashujaa, kwasababu pamoja na shida zao wanalipa kodi,wanachangia pato la taifa kwa maana nyingine wapo mstari wa mbele kuijenga ncho yao, lakini akifa nani atamjua
Post a Comment