Wednesday, July 25, 2012

TANZANIA YANGU....Na DHIHAKA ya kuwaenzi MASHUJAA

NB: MARUDIO YA MWAKA JANA...... Ni wakati ambao tunatakiwa kuhakikisha kuwa HATUENZI MASHUJAA KWA STAILI AMBAYO TUMEIIGA KUTOKA KWA WALE AMBAO "MASHUJAA" WETU WALIPIGANA NAO KUWAONDOA NCHINI.
Mimi namuangalia(ga) tuuu.....
Mhe. Rais. Ni lini mara ya mwisho ulitoa hotuba yenye kuwataja mashujaa utakaowataja leo? Siku ya mashujaa mwaka jana eeeeeee? Ok!
Leo (Julai 25, 2011) ni SIKU YA MASHUJAA NCHINI TANZANIA.
Siku hii INAKUMBUKWA kuliko KUENZIwa, jambo ambalo si geni kwa TANZANIA YANGU, kwani hata siku ya uhuru ni vivyo hivyo. Niliandika HAPA, kwamba naiona kama SIKU YA UHURU INAYOSHEREHEKWA KWA STYLE YA KI-TUMWA. Na nina sababu kadhaa za kuona kuwa namna tunavyosherehekea siku hii (ambayo tunastahili kuiadhimisha) ni DHIHAKA KWA MASHUJAA WA KWELI.
Kwanza ninawaza kuhusu TAFSIRI YA SHUJAA WA TANZANIA.
Ni nani?
Aliishi lini (kama haishi sasa)?
Alitengenezwa ama anatengenezwa vipi?
Kituo cha Televisheni cha History channel wana kauli mbiu isemayo "HISTORY. MADE EVERYDAY". Ninalowaza ni namna ambavyo tunasherehekea siku ya mashujaa ilhali hatuna mashujaa wajao.
Kwenye picha hapo juu wamuona Rais Kikwete katika moja ya "sherehe" nyingi za mashujaa nchini ambazo amehudhuria na kufanya kile ambacho anastahili kufanya, na kisha kuondoka.
KWANI SHUJAA WA LEO HII NI NANI?
Je ni mwalimu kama Mwalimu huyu Leziel Gowele ambaye alikuwa mwalimu pekee katika shule ya sekondari ya Makonde wilaya ya Ludewa mkoani Iringa?
Je, ni dada zetu wanaolea watoto watukutu wa VIONGOZI wetu? Ambao HAWANA MIKATABA YA KAZI, wananyanyaswa, wanabakwa, wanapuuzwa, mishahara midogo na kazi nyingi. Ambao wamelea wengi wa VIONGOZI WETU wa sasa na bado wanaendelea kutothaminiwa na kuitwa ma-house girl? Kama huelewi karaha za maisha yao, TAZAMA VIDEO HII hapa chini Ama ni askari wetu ambao asilimia kubwa wanaishi katika mazingira yasiyostahili na kila uchao wanaenda kuwalinda WATAWALA wanaoishi "PEPO YA DUNIANI"? Hivi mazingira haya hapa chini yangestahili kuwa katika nyumba za askari polisi, tena kituo cha kati JIJINI DAR-ES-SALAAM?
Labda kuna atakayesema kuwa ni kina Mkwawa, Mirambo, Kinjekitile na wengine wanaoeziwa kwa kumbukumbu ambazo baadhi zina hadhi ya chini na siamini kama kuna watu wengi wanaopata nafasi ya kusimama na kuangalia, kusoma na kuenzi kilichoandikwa. Zaidi ni kwa matumizi ya maelekezo ya kufika mahala fulani ama kukutana mahala fulani.
Iringa
Mbeya
Morogoro
Hawa wote walipigania mambo ambayo leo hii bado yapo na sasa yanatendwa na waTanzania wenzetu. Nina hisia kuwa WAKIFUFUKA, TANZANIA ITAINGIA KATIKA VITA NINAVYOAMINI WATAANZISHA KUMNG'OA MKOLONI MZAWA.
Hivi ni kipi ambacho serikali ya Rais Kikwete itaenda kusema kuwa INAENDELEZA KWA VITENDO katika kuwaenzi mashujaa hawa?
Mbona hatuoni MITAALA YENYE HABARI KAMILI NA ZA KUVUTIA kuhusu MASHUJAA WETU?
Kwanini pesa za GWARIDE, ULINZI, SARE ZA WANAJESHI na "CHA-JUU" zisiwekezwe kwenye kuJENGA MAKUMBUSHO YA KILA SHUJAA huko kwao, kuhakikisha kuna historia ya kutosha katika vitabu na mitandao na kuweka mkakati wa kuhakikisha kila mwanafunzi anasoma kuhusu mashujaa hawa?
Ni kwanini Rais asisitishe gharama za gwaride na hotuba (ambayo anaweza kuitoa kupitia redio na televisheni) na kuhamishia pesa hizo katika harakati za kuwaajiri walimu, kuwajengea nyumba nzuri, kuboresha maisha ya kinamama (ambao nao ni mashujaa kwa kuwa wengi wao hubeba mzigo wa kulea familia), kuboresha maisha ya askari na makazi yao, kujali wafanyakazi wastaafu (na sio mambo ya EAC) na mengine mengi?
Nina wasiwasi kama Rais alishatoa hotuba yoyote inayohusisha yeyote atakayemtaja leo baada ya SHEREHE ZA MASHUJAA MWAKA ULIOPITA.
Kwa ujumla, mfumo wa kusherehekea mashujaa nchini Tanzania ni DHIHAKA.
Na kama unyonyaji unaendelea, rushwa imeshamiri, kuna matabaka katika jamii, hakuna usawa, hakuna huduma muhimu kwa wananchi na mengine mengi, hawa viongozi wanapokwenda kwenye sherehe hizi wanakwenda kufanya nini? Kuwakebehi MASHUJAA kwa kuwa wanaendeleza yale waliyokuwa wakipinga?
Ni wakati wa kuanza kuifunza jamii kuENZI mashujaa wa ngazi zote. Wakati ambao mtoto hatagoma kumsikiliza shujaa (Mama yake) na kukimbilia kumuangalia rais anayekwenda kwenye makaburi ya mashujaa. Wakati ambao watoto hawatawadharau waalimu huku wakiwatukuza kina Mkwawa, Chief Rumanyika, Nyerere, Kawawa Kambona na wengineo.
Wakati ambao tunatakiwa kuhakikisha kuwa HATUENZI MASHUJAA KWA STAILI AMBAYO TUMEIIGA KUTOKA KWA WALE AMBAO MASHUJAA HAWA WALIPIGANA NAO KUWAONDOA NCHINI.
Lakini hii ndio nchi yangu
TANZANIA YANGU......YENYE KUSHEREHEKEA BADALA YA KU-ENZI MASHUJAA. Ni Dhihaka.

Nawaza kwa sauti tuuu!!!!! Na hivi ndivyo niliwazavyo TATIZO, na amini usiamini, labda NAMNA NIONAVYO TATIZO NDIO TATIZO


Tanzania Yangu ni kipengele kinachozungumzia yale yaendeleayo nchini Tanzania na namna ambavyo "ndivyo sivyo" inavyozidi kupamba moto nchini. Kwa matoleo yaliyotangulia BOFYA HAPA


Tuonane "Next Ijayo"

5 comments:

Fadhy Mtanga said...

Hii ndiyo Tanzania. pengine tungeacha kutumia pesa nyingi kwenye sherehe za mara moja kwa mwaka na badala yake kuboresha hali halisi za mashujaa wetu.

kule kwa Mjengwa kuna picha ya askari waliopigana vita ya pili ya dunia. ukiwatazama utaona dhahiri jinsi maisha yao yalivyo duni. unadhani serikali ingeamua kuyaboresha maisha yao kwa kupunguza gharama zake zisizo za lazima ingeshindwa?

nadhani bado hatujajua nini kipewe kipaumbele zaidi ya kingine.

Mwalimu Nyerere alipata kusema, KUPANGA NI KUCHAGUA......

nasi tumechagua haya tunayoafanya sasa.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

hata wewe ni shujaa ndugu. una ushujaa wako niliwahi kukwambia via Face book

Ebou's said...
This comment has been removed by the author.
Ebou's said...

Shujaa ni yule alieteseka kwa kutete haki za binadamu, kutete umma na waliopigania nchi yao, kwa mitutu ya bunduki,alienyanyaswa na akanyanyasika, chukua mfano mzuri wa Martin luther king jr, Role in the Civil Rights Movement, ambae mpaka wamemuuwa kwa ushuja wake, tumuangalie, Mandela spent twenty-seven years ndani ya jela huyu unaweza kukwita Shujaa.. Malcolm X. shujaa, Paul Bogle, Marcus Garvey, chukulia mifano ya hao wazee then ndio umwite mtu shujaa!... Uswahilini kuna vituko sana na naona mwisho Hasheem thabeet mtamwita shujaa lol

emuthree said...

Hizi siku-kuu bwana, ni namna ya kujitambuslisha, ni mambo ya kisiasa, labda ingelikuwa na tifa fulani.
Mimi kwanza najiuliza kwenye sherehe kama hizi mambo ya chama yankujaje?
Pili kuwaenzii mashujaa, natumai ingekuwa ni moja ya kuiita historia, vizazi vyetu vikajua, mfano, kuwa na matukio yanayoivuta jamii, ili wawe makini kujua nini kinaendelea.
Wenzetu wanawake makombe ya mpira, ambayo yanakutanisha mataifa mengine, sasa kwa hili utawavuta Watanzania kuuliza kulikoni.
Wengi tusiofuatilia matukio, na hatujui historia,hatukujua kabisa kuwa kulikuwa na sherehe kama hiyo..
Swali linabakia ni NANI SHUJAA WA NCHI, MPAKA TUMSHEREHEKEE, tukumbuke kuwa kuna wanavijiji wanaishi kwa mlo mmoja kwa siku, ...sio wanakijiji, raia wemma..hawa ni mashujaa, kwasababu pamoja na shida zao wanalipa kodi,wanachangia pato la taifa kwa maana nyingine wapo mstari wa mbele kuijenga ncho yao, lakini akifa nani atamjua