Tuesday, August 30, 2011

Mmmmmhhh!!! Kama navutiwa "kuibiwa" vileeeee!!!

Mimi nawe tunajua kuwa hii ni BAHATI NASIBU. Na aliyeshiriki ama alikuja na namba zake na kuchagua kununua hapo, ama alikuja kisha mashine ikamchagulia namba "randomly".
Lakini hata kabla ya hapo, tukumbukuke kuwa hata mteja huyo kuingia humo kununua (miongoni mwa sehemu nyingi zinazouza tiketi hizo) ni bahati.
Nawaza uhalali wa mwenye duka kutumia BAHATI ya KUBAHATIKA kupata M'BAHATISHA huyu aliyeBAHATIKA kuBAHATISHA hizo robo milioni kutangaza kuwa duka lake lina BAHATI.
Hivi aliwaza nini?????

***"Waliwaza nini ni kipengele cha kuelimishana tukifurahia. Hiki kitakuwa kikikuletea habari za kweli na kushangaza kuhusu watu ambao wamefanya yale ambayo unaweza kujiuliza kuwa WALIWAZA NINI? wakati wanatenda haya. Kitakuwa na habari fupifupi kutoka ulimwenguni kote. Kwa habari zaidi kuhusu kipengele hiki BOFYA HAPA"***

4 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Sasa hapo sijui ni nani mwenye BAHATI?

Unknown said...

ni katika kukurubuni hili na wewe ujaribu kubahatika! ukweli ni kwamba ni rahisi zaidi kupigwa na radi kuliko kushinda bahati nasibu!!!

Unknown said...

MICHEZO ya bahati nasibu inazidi kuongezeka kila kukicha huku waandaaji wa michezo hiyo wakizidi kunufaika huku wananchi wa kawaida wakizidi kutumia vipato vyao vya chini ya dola 1 kwa siku katika kushiriki michezo hiyo.

Inashangaza kuona kwamba hili limekuwa halichunguzwi kiundani na vyombo husika ambavyo vinahusika hasa bodi ya michezo ya kubahatisha, kwani michezo mingi ya bahati nasibu mshiriki anapaswa kuchangia kuanzia kiasi cha shilingi za kitanzania 500 hadi 1000, wakati huohuo Mtanzania wa kawaida anaishi kwa chini ya dola 1 sawa na shilingi 1300.

Vijana ndio wanaoathirika sana na tatizo hili ambapo wamekuwa wakicheza kila siku bila kupata bahati ya kushinda huku wakijipa matumaini kwamba ipo siku watashinda.

Sina maana mbaya katika kulisema hili lakini ninajaribu kuwasilisha uhusika wa vijana hao ambao wamekuwa wakishindwa kupata elimu inayowafaa ili kuweza kujua maana halisi ya michezo hiyo.

Simon Kitururu said...

Ingia tu kichwakichwa Mkuu kwa kuwa nasikia KISAIKOLOJIA lujaribu ni DAWA!