Monday, August 29, 2011

Tanzania yangu..."Inayokazana" kuona ilhali imefumba macho (II)

Katika sehemu ya kwanza ya muendelezo huu niliangalia namna ambavyo TANZANIA YANGU inajitahidi "kufa kupona" kuendelea lakini inapuuza ELIMU. Ukweli wa mambo ni kuwa sio tu watu wanaliona suala hili, lakini wenye mamlaka na dhamana ya kusema haya, WANAPUUZA. Na si ajabu kwa kuwa wao ni wanufaika wa hali ilivyo. Ni suala hili la KUNUFAIKA KWA UHARIBIFU WA VINGINE ambalo linanifanya nione tittle hiyo yafaa hapo juu.
Juzi nilikuwa napitia blogu ya Kaka Michuzi ambapo nilikutana na habari hii toka kwa WAKAZI wa Block 5 na 6 ambao wamelalamikia namna ambavyo shughuli za uchimbaji mchanga zinaathiri mazingira yao. Katika sehemu ya maelezo yao, wanasema "tulikwishatoa taarifa juu ya jambo hili polisi, serikali ya mtaa, kwa mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni kwa DC mwezi June. Lakini hadi hivi leo mwezi August watu hawa wanaochimba mchanga wanaendelea kuchimba mchanga na wamediriki hata kututishia sisi wananchi wa eneo hili la Mivumoni".
Tazama taswira hizi hapa chini kisha nisaidie kutambua iwapo hakuna mkuu wa kaya, kitongoji, kijiji, tarafa, wilaya, mkoa, na hata taifa aliyeona hili?
Ni Tanzania Yangu. Kuelekea MIAKA 50 YA KUWAJALI WANANCHI.
Heaven Help Us All
Kwa wale wanaodhania kuwa hili ni la kwanzakusemwa ama kati ya machache, nikukumbushe hii niliyoiona kwenye blogu ya Kaka Josephat Lukaza ambapo pia niliuliza maswali haya haya kuwa wako wapi ndugu, jamaa na marafiki na viongozi?
Kilicho kibaya ni kuwa hata viongozi wa ngazi mbalimbali wanaona haya japo wanapuuzia.
Wameonywa, wameombwa na bado hawafikirii kama huo ni wajibu wao. Wanayaona maendeleo ya sehemu husika licha ya kuwa yale wanayoweza kuona kama maendeleo (kuuza mchanga) kunadidimiza maendeleo ya uhai na mazingira wa watu wa eneo hilo. NI NANI ALIYE MTUMISHI WA NANI?
HUKU NDIKO "KUKAZANA KUONA ILHALI TUMEFUMBA MACHO".
Ni wakati wa kufumbua macho na kwa waliofumbua basi WAACHE KUTAZAMA BALI WAONE. Ni wakati ambao JAMII lazima ikwepe dhana za kizamani ambazo zimewafanya waweke tumaini kwa watu ambao wanatumia tumaini hilo kuwanyonya na kuwadidimza.
Ni wakati ambao sipendi kuona watu wakipigana, wala wakiuana, bali WAKIWAJIBISHANA NA KUTIMUANA. Na kuwa na HESHIMA KWA KATIBA na wakati ambao hata wale waliovunja katiba wasiitumie katiba hiyohiyo kujilinda.
NI WAKATI WA KUWAFUMBUA WATU MACHO ILI NAO WAAMKE (KAMA KWINGINE) NA KUWAWEZA KUONA.

Tanzania Yangu ni kipengele kinachozungumzia ytale yaendeleayo nchini Tanzania na namna ambavyo "ndivyo sivyo" inavyozidi kupamba moto nchini. Kwa matoleo yaliyotangulia BOFYA HAPA

Tuonane "Next Ijayo"

2 comments:

emu-three said...

Mkuu wewe hujui sasa hivi wakubwa wetu wapo kwenye `honemooni' mpaka ikikaribia kipindi kile kiitwacho cha `KAMPENI' aah, utakulamba hadi miguu...sasa huenda makosa ni yetu, na tusipowahi kufumbua macho, tutajikuta hatupo na wanetu watabaki kushangaa, kumbe, kulikuwa na hiki chetu...matokeo yake ni nini...angalia huko Libya, angalia huko ulaya...mambo yanaanza kutokota, hayatokei hivihivii tu...

Yasinta Ngonyani said...

Dunia haipo tena.