Sunday, August 28, 2011

Thaminisha...... Dj Luke Joe

Dj Luke Joe alipokuwa akizungumza siku ya uzinduzi wa blog ya Vijimambo.
Maisha ni mchakamchaka. Na kwa nchi za ugenini, yaonekana kuwa mchakamchaka zaidi. Ni ugenini huku ambako wengine hawapati muda wa kuwasiliana, kutembeleana, kupigiana simu na hata kufanya ibada, kwa kuwa WAMEBANWA NA KAZI NA MAISHA.
Labda kuna kweli ndani ya hili, na pengine yawezekana ni fikra zetu zinazotufanya tuamini hilo. Lakini kama wengi wanavyosema, KILE UWAZACHO KINAWEZA KUKUTABIRIA MAISHA YAKO YAJAYO. Kwa maana nyingine, kujipanga na kuamua kutekeleza kitu, unaweza kuona mafanikio ambayo hukuyaona awali. Kama nilivyosema HAPA, MAISHA NI TASWIRA.
Leo katika kipengele hiki cha THAMINISHA, nimeona ni vema kutambua mchango wa DJ Luke Joe wa Blog ya Vijimambo. Nakumbuka katika hotuba hii ya Mhe Balozi Maajar siku ya uzinduzi wa blogu ya Vijimambo alihusia matumizi ya mtandao kwa manufaa ya wanajamii walio ndani na nje ya Washington DC. Hii ilikuwa moja ya CHANGAMOTO ambazo alitoa kwa Dj Luke Joe na wote wenye blogu.
Punde baada ya uzinduzi huo, nilipokuwa katika maongezi ya kawaida na Dj Luke, alisema kuwa anahisi anaanza kupunguza jitihada zake kwenye kupiga muziki na kuwekeza zaidi katika blogu. Na sasa mwaka mmoja baadae, naamini ni wengi wanaoishi maeneo ya Washington DC na vitongoji vyake wanaweza kuamini kuwa Vijimambo imekuwa kama chanzo cha habari na matukio mengi yanayotukia ama kutarajia kutukia eneo hili. Ni kiunganishi chema na MUHAMASISHAJI mwema kwa jamii ya hapa.
Nimesema MUHAMASISHAJI (tena kwa herufi kubwa) kwa kuwa sote tuishio vitongoji vya DC tunatambua namna ambavyo chombo ambacho kilikuwa kikihusika na kutukusanya na kutuhamasisha na hata kutuhabarisha kuhusu Tanzania, uTanzania na waTanzania hapa DC kilivyo kwenye mgogoro. Na kwa kukosekana kwake, hakika ilikuwa kama kundi zima limetawanywa bila mchungaji. Na siku za karibuni, jamii yetu imepatwa na misiba mitatu iliyofuatana, na kutokana na wengi kutokuwa na ratiba inayoruhusu kuwa mahala pa msibani ama mawasiliano ya msibani, blogu ya Vijimambo ilikuwa zaidi ya "makutano" kwetu. Ni hapa tulipojua kilichotokea, kilichokuwa kikiendelea na kwa wale ambao kwa namna moja ama nyingine hawakuweza kuhudhuria, waliweza kushiriki kupitia blogu hii. Tumekuwa tukipata habari (toka msibani ambako Dj Luke amekuwa akishiriki), picha na hata video za matukio mbalimbali.
Narejea katika aya yangu ya kwanza, kwamba MAISHA YA HAPA NI MCHAKAMCHAKA, NA NI KWA UGUMU HUO, KUNA HAJA YA KUTHAMINI MUDA WA DJ LUKE ambaye licha ya kuwa na kazi kama tulivyo wengine wengi, bado anaweza kutenga muda wa ziada kufanya haya yote.
Hii imekuwa CHACHU kwangu, na naamini kwa wengine wengi.
Na ndio maana katika kipengele hiki cha THAMINISHA, tumeona tutoe (japo) TUZO HII YA KAULI kwa Dj Luke, ambaye aliyoyafanya (hasa katika kipindi hiki cha misiba) ilikuwa zaidi ya wajibu wa pamoja wa Ubalozi na Jumuiya yetu. Alikuwa kwenye misiba yote, katika matukio yote muhimu na kutuhabarisha maendeleo yote ya vifo, michango, ibada na hata maziko.
HILI SI LA KUPITA BILA KUTHAMINIWA (labda kama hujui ugumu wa aliyoyafanya).
Kwa Kaka Luke, NATHAMINI SANA MCHANGO WAKO. Najua ugumu wa ratiba za maisha ya hapa, najua ugumu wa ku-blog, na najua ugumu na gharama za kusafiri katika kona zote ulizofanya na kushiriki katika matukio yote uliyoshiriki ili kutujuza yote yanayotokea. Ni kwa kutambua ugumu huo, napenda kusema ASANTE.
Na ndio maana naona ni vema kuweka thamani yako nikianimi kuwa WASOMAO HAPA, NAO WATATHAMINISHA UWAFANYIALO
Wimbo huu hapa chini ni maalum kwa ajili ya yale mema ututendeayo. Kwangu mimi, YOU ARE A HERO.

Do you see the smiles on their faces
after you have done what you do best
do you see satisfaction on their faces
after you have blessed themw ith your gift
you don't think iit's much
but to them it means the world
they wake up in the morning and wish you were there
don't have to lie to gain their trust
you have never won a Nobel prize
they have never seen you on the TV
your little contribution makes their lives a little bit better every day

chorus
You're a hero x8

big it up, big it up for the fireman
big it up, big it upfor the street cleaners
big it up for the man aNd the woman
who take care of abandonded children
big it up, big it up for the grandmothers
who are left to take care of the children
big it up, big it up Wo!!


**THAMINISHA ni kipengele kinachounganisha makala ama matoleo mbalimbali ya watu mbalimbali wanaojitolea kuboresha maisha ya wengine na hata wale wanaoona vema kuthaminisha yale waliyotendewa na wengine. Kwa matoleo zaidi BOFYA HAPA**

1 comment:

Ebou's said...

Kwa kweli kamanda wa changamoto yetu mhamasishaji ni mtu anayependa kujifunza mambo mapya kulingana na wakati na jamii inayomzunguka, huwa na matumaini makubwa ya kufaulu katika maisha yake binafsi na katika yale anayopanga kufanya kwa watu wengine. Ni kazi kumbu na sio lele mama kama alivyosima Dj luke hapo awali alipoanza Blog yake.

Hiyo ndio hali halisi ya mtu anaependa kuhamasisha mambo mazuri na yanayokubalika katika jamii Kama Dj Luke wa DMV.

Sote tuna lengo moja cha Msingi tukae mstari wa mbele tuspray love pamoja one LOVE Hongeta sana Luke Vijimambo.

Na changamotoyetu jina umelipatia tupo pamoja kwa kila kilicho sahihi kwa jamii tuipendatu.