Ingenichukua muda kusahihisha Homeworks, lakini wote wangefanya VEMA, TANZANIA ingekuwa sehemu bora ya kuishi kuliko ilivyo sasa.
Napenda "old style" ya ualimu. Ile iliyonikuza na kunisomesha. Ile waliyokuwa wakiifanya waalimu kama Baba yangu ambapo walimu walikuwa wanajua uwezo wa takribani kila mwanafunzi. Walikuwa wanahakikisha kuwa kila mtu anafanya "homework" yake na walikuwa wanasahihisha siku inayofuata. Walimu walikuwa na uwezo wa kutambua kama umefanya mwenyewe homework yako ama umefanyiwa. Halafu kingine nilichokuwa napenda ni ile style ya kubandika matokeo darasani. Yaani kujua nani kawa wa kwanza na nani wa mwisho. Hapo ilikuwa ni lazima usome sana maana ni kuangalia nani ana VEMA nyingi na nani anaongoza darasa. Lakini kwa mtazamo wangu ilikuwa na faida maana yaliyotendeka ilikuwa ni CHANGAMOTO KWETU kuongeza juhudi katika masomo.
Style hii ningeipata nikaweza kuitumia katika BUNGE LA TANZANIA naamini ingesaidia saana. Yaani kuhakikisha kila m'bunge anapoondoka bungeni baada ya kusanyiko haelekei "kutumbua" pesa alizofanya, bali anapewa "homework" ya kufanya jimboni mwake na akirejea kwa "darasa" (kikao) kijacho kwanza ninaangalia nani kafanya nini na kafanikiwa mangapi kisha tunasonga mbele. Yaani kujua nani anajua na kutatua matatizo ya jimboni mwake na kuwasaidia wananchi wake na pia tungejua nani hana ajualo kuhusu shida na mahitaji ya wale awaongozao. Ingetuwezesha kujua nani yuko mstari wa mbele kubadilishana mawazo (pale nitakapowapa group discussion ya kukokotoa maswali) na kutumia "ideas" za wenzake kufanya homework zake kuwasaidia wananchi wake. NINA UHAKIKA kwa mfumo huu lazima TANZANIA YANGU ingekuwa hatua kadhaa mbele kuelekea kwenye mafanikio ya kutatua shida za wenye uhitaji. Lakini licha ya kuwapa hizo "homeworks", wangepewa jukumu la kusaka mahitaji ya wahitaji ambao kwa bahati mbaya wameonekana kujisahau kuyaweka bayana KAMA NILIVYOULIZA NA KUELEZA HAPA. Lakini pia nigejaribu kuwashawishi "maafisa elimu" kuhakikisha MCHUJO WA KUJIUNGA NA SHULE (uchaguzi) unafanyika kwa nyakati tofauti kwa faida na sababu nilizozieleza HAPA
Nimewaza hivi kwa kuwa kuna wakati nawaza kinachowapeleka "wanafunzi" hawa bungeni nashindwa kuelewa. Nashindwa kuamini kama wabunge hawa ndio waliokwenda kwa wananchi na kuomba kura wakiahidi mambo kedekede na kisha KUPOTEA.
1: Iko wapi nguvu ya wananchi kushinikiza m'bunge wao kuishi jimboni?
2: Kwanini katiba isishinikize m'bunge kuwa na kiwango cha chini cha kuishi jimboni mwake kila mwaka? Wapo wabunge ambao wanaenda majimboni kwa nadra sana.
3: Kwanini katiba isishinikize mikutano ya wabunge na WANANCHHI KATIKA SEHEMU ZOTE ALIZOOMBA KURA kabla na baada ya kuhudhuria vikao vya bunge?
4: Kwani wanapokutana bungeni huwa wanasema mahitaji ya jimbo mwao KWA MUJIBU WA NANI? Wao ama wananchi?
5: Wanapoondoka bungeni huwa hawapewi majukumu ya kutekeleza? Ama wakipewa wanaweza kuyatekeleza bila kuwaeleza wananchi? Lakini kama ni majukumu kwa wananchi si tungeona mabadiliko huko tuliko? Namaanisha hata kama hatuambiwi si tungejua kuwa "ujenzi wa hizi zahanati ni manufaa ya m'bunge kwenda kwenye kikao / vikao vya mwaka huu? Kuna mwananchi anayeweza kujibu akiulizwa amenufaika nini na m'bunge wake kwenda kwenye vikao vya kila mwaka.
Sisemi hatujanufaika, (japokuwa sisemi kuwa tumenufaika), ila kama manufaa hatuyaoni bayana na hatuambiwi pia, sijui tufikirieje matumizi ya kodi zetu?
KAMA MWALIMU, ningehakikisha MASWALI YAJIBIWA na HOMEWORKS ZINAFANYWA na naamini mwisho wa muhula NINGEBANDIKA MATOKEO na pia kuyatuma kwa wazazi (wananchi) ili wajue maendeleo ya wanafunzi na kujua nini cha kuwafanya katika muhula ujao wa shule (mhula wa uchaguzi).
Anyway, japo kuna ukweli ndani yake, lakini nafikiri hii ni njozi.
Never Mind!!!
Jicho la ndani ni kipengele ambacho huangalia mambo kwa "undani" zaidi na kujaribu kutafuta suluhisho kutokana na tafakari ya tatizo. Kwa maandiko mengine kuhusu kipengele hiki, BOFYA HAPA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
3 comments:
Kwahiyo mkuu mimi nakupendekeza uwe mwalimu WAO,...
Mmmmh!
mimi naomba niwe mgonga kengele na kuhesabu namba!!!
Post a Comment