Thursday, December 1, 2011

Miaka 21 baada ya kifo chake, 30 baada ya kugundulika UKIMWI...

Ujumbe wake unaendelea kupuuzwa, kizazi chazidi kuteketea. Photo: MUSIC UGANDA.COM
"Today it's me tomorrow someone else
It's me and you we've got to stand up and fight
We share a light in the fight against AIDS
Let's come on out, let's stand together and fight AIDS"

Hiki ni kiitikio cha wimbo ALONE AND FRIGHTENED ambao ulibeba jina la albamu iliyozinduliwa rasmi Sept 29, 1989. Hii ilikuwa ni siku 64 kabla Philly Bongoley Lutaaya hajarejea rasmi nchini mwake Uganda (Des 2, 1989) na kufariki dunia siku 13 baadae (Des 15, 1989). Ina maana leo hii ni miaka 21, miezi 11 na siku 15 tangu amefariki, na USIA aliouimba miaka zaidi ya 21 iliyopita bado ndilo PUNGUFU KUU lililopo katika VITA DHIDI YA UKIMWI katika nchi nyingi barani Afrika.
Tuna msemo mzuuri na wa maana nchini mwetu usemao AISIFIAYE MVUA IMEMNYEA, lakini tusilokumbuka ni kuwa si kila aina ya mvua ikunyeayo hukupa nafasi ya pili ya kukauka na kuwa kama ambaye hakuguswa nayo. Kuna masimulizi ambayo huwakuta watu ambao wanatamani wasingekuwa wasimuliaji wa habari ama hali hizo na licha ya juhudi zao za hali na mali katika kuhakikisha hatupitii yale wapitiayo wao, bado twapuuza na matokeo yake ni sisi kuteketea.
Philly Lutaaya (aliyezaliwa 1951) alikuwa msanii wa kwanza mwenye umaarufu / ushawishi kuwa wazi juu ya kukumbwa na maambukizi ya virusi vya ukimwi na kisha kubadili maisha kwa kutumia kipaji alichokuwa nacho na kilichompa umashuhuri, kuweza kuielimisha jamii kuhusu JANGA LA UKIMWI na pia NAMNA ILIYO SAHIHI KWA JAMII KUPAMBANA NA MARADHI HAYO. Photo: MY HERO.COM
Tatizo la kupuuzia suluhisho halisi la matatizo kwa jamii si kitu kigeni. Tunashangazwa saana na jamii ambayo inapenda kufika 10 bila kufikiria moja na mbili. Aliloimba Philly mwaka 1989 kuwa "ni mimi na wewe tunaostahili kusimama na kupigana vita hii" lilikuwa ndilo suluhisho pekee katika kufanikisha hili.
Kwa mtazamo wa "jicho langu la ndani", naamini aliloeleza Philly ni kuwa tunahitaji kuelimishana zaidi kuhusu janga na madhara. Kuhusu ukweli wa maambukizi na namna tunavyoweza kuishi kwa upendo na kwa miaka miingi tukiwa na virusi na si UKIMWI. Kuelimishana namna ya kuwathamini na kutowatenga waathirika na kuwapa nafasi wanayostahili katika kuisaidia jamii yetu kuelimika kuhusu ugonjwa huu.
TATIZO NI SIASA ZINAPOINGIA KATIKA MAISHA YA WANANCHI.
Sasa hivi (kama alivyosema Rais mstaafu wa Marekani Ronald Regan), kila anayetetea suala la utoaji mimba ni yule ambaye mimba yake haikutolewa. Vivyo hivyo katika hili la Ukimwi. Kamati zaundwa, matumizi yapangwa na "miradi" yaanzishwa lakini waathirika wa virusi hivi wanakuwa watu wa mwisho kabisa katika mchakato mzima na wanakuwa katika upande wa kupokea maelekezo na si kupanga utekelezaji utakaowezesha kufanikisha lengo la kuzuia maambukizi.
Ni vipi tunaweza kuwa na watu wasio waathirika wakazungumzia hisia za kuwa muathirika na kupanga mikakati madhubuti ya kusaidia wengine ambao si waathirika kutofikia hisia na maisha wapitiayo wao?
Haishangazi kuwa VITA DHIDI YA UKIMWI NI MIRADI TOSHA kwani kwa asilimia kuwa yahusisha watu ambao hawana uchungu wa kweli na hawajui uhalisia wa uathirika na pia wanachukuliza vita dhidi ya ukimwi kama miradi.
Ufuatao ni ZAIDI YA WIMBO kwa kuwa ni UJUMBE TOSHA wa namna tunavyoweza kutatua tatizo la UKIMWI hapa ULIMWENGUNI.
PUMZIKA KWA AMANI PHILLY BONGOLEY LUTAAYA

Habari zaidi kuhusu Philly, bofya HAPA
SHUKRANI ZA PEKEE KWA KAKA FADHY MTANGA kwa changamoto hii
Out there somewhere
Alone and frightened
Oh the darkness
The days are long
Life in hiding
No more making new contacts
No more loving arms
Thrown around my neck

Take my hand now
I'm tired and lonely
Give me love
Give me hope
Don't desert me
Don't reject me
All I need is love
And understanding

Chorus:
Today it's me
Tomorrow someone else
It's me and you
We've got to stand up and fight
We share a light
In the fight against AIDS
Let's come on out
Let's stand together
And fight AIDS

In times of joy
In times of sorrow
Let's take a stand
And fight until the end
With open arms
Let's stand up
And speak out to the world
We'll save some lives
Save the children of the world

Let's be open
Advise the young ones
A new generation
To protect and love
Hear them singing
Playing nothing
Let's give them everything
In truth and love

Take the message
Cross the frontier
Break the barrier
We'll fight together
The doors are open
We'll lead the struggle
We won't bow down
In defeat we'll fight on

Chorus

1 comment:

Anonymous said...

asante kaka kwa ujumbe mzuri. nakumbuka kuona video ya Lutaaya ya Ukimwi mwanzoni mwa miaka ya 90. je unaweza kunisaidia kuweza kupata video hiyo, je nitaipata wapi?