Wednesday, November 30, 2011

Ndoto kama hatua...Keep on walking (II)

"May be hoping for a change is a dream, may be life aint as bad as it seems, but if dreaming is the best i can do, then i'll be dreaming my whole life through" Tanya Stephens
Maneno haya ya mwanadada huyu niliyaeleza vema kwenye kipengele hiki hapa. Na kubwa hapa ni kuhusu NGUVU YA KUAMINI NA KUENDELEA KUOTA KATIKA KILE UAMINICHO.
Lakini pia nakumbuka kuwa "kichwa hiki cha post" nilishakitumia katika post hii niliyozungumzia ndoto za Dadangu Lady Jay Dee na zangu pia na kama nilivyosema katika post hiyo, ilikuwa ni MAALUM KWA NDUGU ZANGU WALIOKATA TAMAA YA KUTIMIA KWA NDOTO ZAO.
Katika maisha nimejifunza mengi sana. Na pia nimejifunza kujaribu kurejesha fikra za muunganisho wa matukio ili kuweza kuthamini pale ulipo. Na hili ni tatizo kwa wengi. Watu wengi wameshindwa kuoanisha kilichorokea na kinachotokea sasa na matokeo yake wanashindwa kuwa na FADHILA kwa wale waliowawezesha kufanikiwa walivyo (iwe ni kwa heri ama kwa shari). Niliwahi kueleza HAPA mkasa wa mfanyakazi mwenzangu ambaye nipokutana naye wiki hiyo alinieleza kuwa ANAMSHUKURU MUNGU KUWA HAKUPATA NAFASI YA PROMOTION ALIYOKUWA ANAITAFUTA KWANI KULE ALIKOTAKA KUHAMIA NDIKO WALIKOPUNGUZA WENGI NA WALIPUNGUZA WASIO NA UZOEFU NA KAMA ANGEHAMIA ANGEKUWA HANA UZOEFU WOWOTE. Sura yake ya siku hiyo ilikuwa tofauti na ile aliyokuwa nayo siku aliponiambia kuwa hajapata nafasi aliyokuwa akiiombea. Wakati ule alikuwa na huzuni saana na leo anaonekana kuwa na furaha. Anashukuru Mungu kuwa hakupata nafasi aliyokuwa akijiuliza kwanini ameikosa.
Kuna wengi ambao wako kwenye FANI sahihi lakini wanashindwa kujua ni vipi waboreshe nafasi zao za mafanikio. NA HILI NDILO NINALOTAKA KUZUNGUMZA LEO.
Jana, nilipata nafasi ya kumhoji Dr Donald Thomas. Mhandisi na mwana-anga mstaafu wa NASA ambaye amefanya kazi hapo kwa miaka 20. Na katika miaka hiyo, amekwenda safari za kwenye space mara nne na sasa ni mkurugenzi katika chuo kikuu cha Towson hapa Marekani. Nilikutana kwa mara ya kwanza na Dk Thomas miaka 3 iliyopita ambapo alikuja kazini kwetu kutushukuru kwa kazi tunayofanya ambayo ilikuwa ni muhimu kwa kuwasafirisha kwenda kwenye space. Katika mazungumzo yake akatoa historia yake na namna ambavyo ALIHANGAIKA NA KUVUMILIA kabla hajapata nafasi ya kufanya kile alichokuwa akikipenda zaidi. Ilimchukua miaka 9, alituma maombi mara nne, akaamua kuchukua madarasa ya urubani, scuba diving, kufundisha, kuongeza elimu na mengine ili kufanikisha kile alichotaka kufanya japo hakukuwa na uhakika wa hilo. Lakini aliamini katika atendalo. Habari hiyo ilinivutia saana nikaona nimualike kwenye Club yetu chuoni aweze kuzungumza na kuwahamasisha wanasayansi watarajiwa, na mwezi march mwaka 2009, alikuja chuoni na kuzungumza nasi. WATU WAKAPENDA NA KUJIFUNZA
Dr Thomas nami March 4, 2009.
Baada ya mazungumzo hayo, nilitamani saana kushirikisha wenzangu katika alichozungumza, lakini kwa bahati mbaya SIKUWEZA. Ni kwa kuwa mengi ya aliyozungumza sikuyakumbuka kwa usahihi hivyo nikaona NI VEMA KUMTAFUTA, KISHA NIMREKODI NA KUWEZA KUSHIRIKIANA NA WAPENDWA HAPA. Nilijaribu kiasi (unakumbuka HII POST?) lakini bado haikuwa rahisi. Nikaona njia sahihi ni kumpata na kumrekodi. Tangu katikati ya mwaka 2009 nimekuwa nikiwaza na kujaribu hili, lakini haikuwa rahisi, mpaka JANA (Nov 29, 2011) nilipoweza kumpata kwa mahojiano naye. Na sasa, nikiwa kama mwandishi mwanafunzi, niliweza kujua mengi ya kujiandaa na namna ya kumfanya aeleze mengi zaidi niliyotaka, nilivyotaka na kwa jamii ninayotaka kuigusa. Hili likawa UTHIBITISHO mwingine kuwa KUNA KILA SABABU KATIKA KILA KITOKEACHO. Nikimhoji Dr Donald Thomas Jumanne Nov 29, 2011
FUNZO HAPA NI KUWA kama ningemhoji mwaka niliopenda mimi, pengine nisingepata niliyopata jana, na kama yeye angepata nafasi ya kuingia NASA alipotuma maombi kwa mara ya kwanza, basi yawezekana asingekuwa bora kama alivyokuwa baada ya kuongeza elimu, ujuzi na mengine ili kujiweka sawa. Na mwisho, ni mimi ambaye sikukata tamaa kumtafuta kwa miaka miwili na nikampata na kuongea na yeye kwa kuwa HAKUKATA TAMAA kwa miaka 9 aliyokuwa akisaka nafasi ya kujiunga na NASA na nilipomuuliza wito wake kwa wanafunzi wachanga anasema WASIKATE TAMAA. Akawa kama anahimiza nilichohimiza kuwa USIKATE TAMAA.
Na kwa wewe msomaji, ambaye kwa miaka mingi umekuwa na ndoto ambayo pengine inaonekana kutokamilika.
Kama unachopenda kufanya ni halali na chema, na kama ni mapenzi halisi na ndoto ya maisha yako, basi kabla hujakata tamaa na kuachana nacho, angalia waliofanikiwa kwenye fani ama kazi uitakayo wana SIFA gani ambazo wewe hujakamilisha? Angalia unaweza kujiboresha vipi ili ufanikiwe, na kisha ongeza TALANTA uliyojaaliwa ndani mwako, UTAFANIKIWA.
Na ndio maana narejea kwenye kichwa cha post kuwa NDOTO NI KAMA HATUA.....KEEP ON WALKING
Sikiliza sehemu HII fupi kati ya saa moja la mahojiano yangu na Dr Donald. Nimeweka sehemu ya HISTORIA, HARAKATI ZAKE KUJIUNGA NA NASA, ALIVYOKATA TAMAA BAADA YA KUONA AMEKOSA NAFASI HIYO, HISIA ZAKE SIKU ALIPOPATA na mwisho WITO WAKE KWETU.
FURAHIA UKIJIFUNZA


Na ukitaka kutazama mission moja kati ya nne alizokwenda Dr Don, tazama video hii iliyoeleza kwa ufupi safari yao hiyo.

USISAHAU KUKOSOA / KUSHAURI uaminipo pana kosa ama kuhitaji ushauri. Nathamini saana hilo na ndio njia pekee ya kuniboresha.

1 comment:

Kamwesiga said...

Hakika subira inastahili hata kwa yule aliyekata tamaa.Nimejifunza mengi sana kupitia post hii.