Sunday, November 20, 2011

Ndoa vs Harusi

NDOA vs HARUSI.
Mahusiano yake ni madogo sana (kama yapo) na pia mafanikio ya moja kati ya hayo hayana AKISI ya moja kwa moja kwa jingine. Tofauti baina yake ni kubwa kuliko inavyochukuliwa na umuhimu wa elimu juu ya uelewa wake ni zaidi ya inayotolewa.
Nilielezwa kuwa HARUSI ZOTE ZAFANANA JAPO KILA NDOA NI YA KIPEKEE. Na kuwa waweza kuwa na ndoa bila harusi na harusi isiyo na ndoa ya kweli.
Labda ni wakati wa kuangalia vema na kuwekeza katika NDOA na si HARUSI kama ilivyo kwa wengi hivi sasa.
Unaamini kuwa mafanikio ya ndoa yanategema (kwa namna yoyote ile) maandalizi ya harusi?
Unaamini kuwa mafanikio ya HARUSI yanaweza kuwa na ishara yoyote juu ya mafanikio ya ndoa?
Unaamini kuwa HARUSI yaweza kuwa chanzo cha mvurugano wa NDOA?
Kwanini tuwe na NDOA na HARUSI kama uhusiano wake waweza kutomaanisha lolote kwa pamoja?
Kwani NDOA NA HARUSI NI UTASHI AMA "MFUMO"
Nawaza kwa sauti tuuuuu!!

5 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Hizi ndoa/harusi kwa kweli wengi wanaona kama ni kufurahia tu hawajui kama wanaingia katika maisha gani. Angalia siku hizi watu wanavyoachana wanaoana leo shngwe na vifijo na pesa nyingiiiii zinatumika baada ya mwezi hakuna ndoa...Hivi kwa nini basi watu wasiishi kwanza miaka kadhaa bila kufunga ndoa na kusomana na baada ya hapa unaweza kujua kama kweli mnaweza kuvumiliana milele au vipi. Nami nimewaza tu kwa sauti::::

emuthree said...

Hi mada inalandana na sehemu iliyopo kwenye kisa chetu, `akufaaye kwa ziki...' Ni kweli mkuu harusi naweza kusema inachakachua ndoa...ndoa ndio kiini, lakini haithaminiwi kama ilivyo harusi...huo ni mtizamo wangu!

Mary Damian said...

Ndoa ni AGANO kati ya mke/mume kuishi pamoja kama mke na mume. Harusi ni sherehe ya pongezi/kupongezwa kwa kufanyika agano hilo. Vyote vyaenda pamoja ila inategemea na ufahamu wa mtu, kuna wengine wanafanya harusi kuonesha ufahari, wengine sherehe ndogo tu kwa ajili ya kumbukumbu na AGANO lao hudumu....

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

mhhhhhhhhhhh labda sijui ndoa, lakini weweza kuoa / olewa bila harusi kama nilivyofanya

MswahiliFlani said...

Sio leo bila ya harusi mhhhh labda umefumaniwa na kuozeshwa kwa nguvu ni kweli aliyosema muhusika kule juu ila harusi si yawale wenye harusi harusi ni wale wanaosheherekea harusi kwani wao ndio waliotaka kuacheza watoto wao na kuatoa kitoka nyumba.