Mama wa Kaka, Rafiki na bloga mwenzetu Addson Omari (Je! Huu ni uungwana blog) amefariki. Kwa mujibu wa Kaka Addson (pichani juu), Mama Shamsa binti Hassan alifariki nyumbani Tanzania jana tarehe 2/12/2012 na kuzikwa siku hiyo hiyo. Habari za kisomo na dua zitawajia baadae kidogo.
Blogu hii ilifanikiwa kuungana na bloga wengine Sunday Shomari (Sunday Shomari blog), Ebou Shatry (Swahili Villa blog), Dj Luke Joe (Vijimambo blog) na Da Yasinta "Kapulya" Ngonyani (Maisha na Mafanikio blog) kuwasiliana naye na kumfariji Kaka yetu kwa msiba huo.
Kaka Addson pia anapatikana kupitia simu ya mkononi namba +1 301 222 7739.
Pichani (L-R) ni Kaka Sunday Shomari akiwa na binti wa Addson aitwaye Naima (huyu aliyonionyesha jana ni post tosha. Itakuja baadae), Kaka Ebou Shatry, Kaka Addson nami tukiwa nyumbani kwa mfiwa Baltimore Maryland kuungana naye katika kusherehekea na kuenzi maisha ya Mama yake mpenzi.
Rafiki yangu Glorie Ngahyoma alisema "Death leaves a heartache no one can heal, love leaves a memory no one can steal"
Nami nakubaliana naye. La kukumbuka ni kuwa PANAPO MAJAALIWA, TUTAONANA TENA.
Kama alivyosema Beres Hammond katika wimbo I'ii Live again, naamini sote tutaonana tukimtegemea Mungu mkarimu na msamehefu.
Bwana alitoa, na sasa ametwaa. Mapenzi yake yatimizwe
Picha kwa hisani ya Kaka Sunday Shomari.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
3 comments:
Katika maisha USHIRIKIANO ni jambo nzuri sana. Nawasifu kaka zanngu kwa jambo mlolofanya kuwa na kaka Mrope kwa siku hiyo ya 2/12. Kaka Mrope pole sana. Nakuomba uwe mvumilivu najua ni jinsi gani inauma kufiwa na mama mzazi. Mungu alitoa na Mungu amechukua pia sisi tulimpenda lakini Mungu amempenda zaidi. Mama Huku uliko tuombee na sisi. Ustarehe kwa amani. Amina
Pole Mfalme! R.I.P Mama!
Poleni sana kaka Mrope pamoja na familia yote nyumbani Tanzania.
Mungu ailaze roho ya mama yetu mahali pema.Amen!!
Post a Comment