International Women's Day

International Women's Day

IMETOSHA

IMETOSHA

KUMRADHI

Kutokana na kubanwa na masomo, mabandiko hayatakuwa kila siku kama awali.
NAWAPENDAFriday, March 30, 2012

Kila la kheri Blog ya Vijimambo.

Oktoba 24, 2010, blogu hii iliandika makala ya kuzinduliwa kwa blog ya Vijimambo (bofya hapa kujikumbusha) ambako kulifanywa na Mhe Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa nchi za Marekani na Mexico Mhe. Mwanaidi Maajar.
Leo hii, blog hiyo inatimiza miaka miwili.
BLOGU YA CHANGAMOTOYETU INATOA PONGEZI ZA DHATI KWA BLOGU YA VIJIMAMBO.
Na hii ndio ratiba na maelezo ya kitakachotendeka katika kuadhimisha miaka hiyo.
Sherehe zitaanzia saa 4:00 Asubuhi (10:00am) Mpaka saa 12:00 jioni (6:00 pm) kwa mechi za soccer kugombea Kombe la VIJIMAMBO timu zitakazoshiriki ni:
Burundi kutoka Arizona
Tanzanite kutoka Atlanta, GA
DC Nyarugusu Watanzania Kutoka DC.
Vitambi FC Wakenya Kutoka DC
Malawi kutoka DC
na Stars United.

Mechi zitachezewa
8000 Walker Mill Rd,
Capitol Heights, MD 20747

Na kufuatiwa na Sherehe ya usiku zitakazoanza saa 1:00 jioni (7:00 pm) Tafadhali naomba uzingatie muda.
RADIO MBAO ITARUSHA PARTY YA VIJIMAMBO LIVE

Napenda kutoka shukurani kwa Ubalozi wa Tanzania Nchini Marekani, Wadhamini waliojitokeza na shukurani za pekee ziwaendee Wadau wa VIJIMAMBO waliojitokeza na kujitolea kuleta chakula, vinywaji na kupamba ukumbi ili sote kwa pamoja tufanikishe sherehe hizi kwani pamoja tunaweza.

PARTY YA USIKU NI KWA WATU WAZIMA TU

DRESS TO IMPRESS

No comments: