Hapo awali nilipata kuandika kuhusu NDOA vs HARUSI ambapo nilieleza lile ninaloamini kuwa "Mahusiano yake ni madogo sana (kama yapo) na pia mafanikio ya moja kati ya hayo hayana AKISI ya moja kwa moja kwa jingine. Tofauti baina yake ni kubwa kuliko inavyochukuliwa na umuhimu wa elimu juu ya uelewa wake ni zaidi ya inayotolewa.
Nilielezwa kuwa HARUSI ZOTE ZAFANANA JAPO KILA NDOA NI YA KIPEKEE. Na kuwa waweza kuwa na ndoa bila harusi na harusi isiyo na ndoa ya kweli."
Kisha nikarejea kwenye SWALI LA MSINGI kuwa "Kwanini tuwe na NDOA na HARUSI kama uhusiano wake waweza kutomaanisha lolote kwa pamoja?"
Lakini kabla ya NDOA na hata HARUSI kunakuwa na MAZOEA YANAYOTOKANA NA MAKUZI tuliyokuzwa kabla hatujakutana na "asali wa moyo" wetu. Na haya yana nafasi kubwa saana katika maisha yetu.
Ni wazi kuwa jamii nyingi za kiAfrika zimejengwa ama kujijenga kwenye mfumo ambao MWANAUME NI KICHWA CHA FAMILIA. Na hili linaifanya jamii iwaone wanawake kama "daraja la pili" katika familia.
Na ndio maana hata inapotokea mwanaume akafanya baadhi ya mambo "yasiyokubalika", anaweza kuonekana kama anafanya "jambo la kiume" ilhali jambo hilo likitendwa na mwanamke, itaonekana KITUKO.
Mfano mdogo ni ULEVI. Kwa mwanaume kulewa mpaka kesho yake akaokotwa mtaroni yaweza kuwa "uanaume" ilhali mwanamke akilewa akawa anaanguka na kuamka mpaka akafika kwake, anaweza kuwa "gumzo la mtaa". Anyway. Tuachane na haya
Lakini pia kuna MAKUZI yawafanyao kinadada "KUNYWEA" katika mahusiano, na hasa katika hatua za mapenzi na unyumba, jambo ambalo humfanya kijana kujiaminisha kuwa hiyo ndiyo tabia halisi ya binti, na kwa kuwa binti huyo ameonyesha utayari wa kuvumilia karibu kila upuuzi wa mwanaume, inamjengea u-sugu wa ujinga mwanaume.
Ukweli wa mambo ni kuwa JAMII YETU HAIJENGI MAZINGIRA HALISI YA NDOA kabla ya ndoa.
Labda ni kwamba HATUWAFUNDISHI WATARAJIWA KUHUSU MAISHA HALISI YA NDOA (na namaanisha ndoa na sio "vishikizi vidogo vya ndoa" mnavyofundishana kwenye kitchen party na jando na unyago).
Tatizo kubwa ni kuwa watu wengi HAWAJIANDAI KUINGIA KWENYE NDOA na wengi wao wanashindwa hata kutofautisha kati ya NDOA na HARUSI na matokeo yake, kile kiitwacho MIPANGO YA NDOA huonekana kuwa na thamani na kufika tamati pale HARUSI (ambayo wengi huiita ndoa) INAPOFUNGWA.
Ni kama vile watu wanaamka asubuhi baada ya harusi na kujiuliza "now, what next?"
Maana ni kama AMEFIKIA TAMATI YA MIPANGO YAKE YOOTE na sasa anaanza upya kusaka kitakachomkalisha kwenye ndoa.
Haya ni MAZOEA KWENYE JAMII YETU, AMBAYO NAYO HULETA MAKUZI AMBAYO KUYATENGANISHA UKUBWANI SI KAZI RAHISI.
Na kwa maana nyingine, ni hayahaya MAKUZI ambayo yanakuwa sehemu ya ndoa zetu na kwa asilimia kubwa hayawi kwa faida yetu.
Labda kwa ndugu zangu mlio kwenye mchakato wa kumtafuta wa kuishi naye, ni vema kuangalia mambo muhimu katika maisha ambayo mngependa kuyakamilisha, na kisha kuangalia namna ambavyo mtaweza kuyakamilisha na mwisho kuangalia yule atakayeweza kukusaidia kuyakamilisha.
Kama ambavyo nimekuwa nikieleza kwenye vipindi mbalimbali vya radio ninavyoshiriki, "UWE NA UFAHAMU WA KILE UNACHOTAKA (VIGEZO), KISHA ANGALIA KAMA YULE AJAYE ANA VIGEZO HIVYO". Kuwa makini kutoweka vigezo visivyovikika lakini pia, kuwa makini kwa kutoanza kupanga vigezo kuweza kuhitimisha lengo lako la kuwa na fulani. Kuwa makini katika mipango yako na kuepuka "KUTAKA NDOA KAMA YA FULANI" kwani maneno hapo juu yanajieleza kuwa "HARUSI ZOTE ZAFANANA JAPO KILA NDOA NI YA KIPEKEE".
Katika kujazia harakati hizi za maandalizi mazuri ya ndoa, napenda kukukaribisha kusikiliza maelezo haya hapa yanayoeleza kuhusu NJIA 10 ZINAZOWEZA KUKUEPUSHA KUOANA NA MTU ASIYE SAHIHI.
Karibu katika maelezo haya juu ya Njia kumi za kukuepusha kuoa mtu asiye sahihi. Maelezo haya yaliandikwa na Dr Nafisa Sekandari na Hosai Mojaddid. Sehemu ya andiko hili lilitokana na maelezo ya Rabbi Dov Heller wa Massachussets. Yalibandikwa kwenye kipengele hiki cha Mental Health for Muslims.
Yametafsiriwa na Jovitha Mchalla na kuhaririwa na kusimuliwa nami
KARIBU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
6 comments:
Pia naweza kusema huwa nashangaa sherehe za harusi/ndoa zinavyokuwa kubwa na zaidi zinakuwa kubwa na halafu hazizumu ..kwa kweli sielewi kabisaaaa!!!
Ni somo tosha kwa sisi tunaojipanga kuingia huko... nimeipenda mnoooo
Kama nilivyowaza ndivyo ilivyo kazi nzuri na mimi nitawafikishia wale ambao wanatarajia kuishi maisha ya ndoa ili wasiharibu gharama zao..Bandio, dada Yasinta Kijah, tukazi buti kuelimisha jamii!
very nice lesson kwa ambao hawajaingia NDOANI.nimejifunza kitu for sure
Ahsante kwa post nzuri kaka
inafikirisha kwa kweli
Post a Comment