Thursday, March 8, 2012

Kwenu wanawake, ASANTENI

Tribute to the Women of the World
This is a humble sampling in tribute to some of the great women throughout history ... set to the song, Hero, by Mariah Carey.

Kila mwaka wanawake na walimwengu kote ulimwenguni huadhimisha SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE DUNIANI ambayo husherehekewa tarehe 8 Machi.
Mamia ya shughuli na matukio hufanyika ndani ya mwezi mzima wa Machi kusherehekea na kuadhimisha harakati za wanawake duniani katika Uchumi, Siasa na ukombozi wa Jamii ambapo Serikali, Vikundi vya wanawake na mashirika mbalimbali huchagua kauli mbiu kuakisi masuala ya kijinsia katika jamii husika na ulimwengu kwa ujumla.
Kauli mbiu ya mwaka huu kutoka Umoja wa Mataifa ni WAWEZESHE WANAWAKE WA VIJIJI, KUOMESHA UMASKINI.
Maisha yangu yalipitia malezi ya Mama zangu wadogo na Dada zangu. Hawa nao ni sehemu kubwa ya maisha niliyo sasa. Nikiwa mhangaikaji asiyeonekana kuwa na mafanikio ya karibu maishani, waliendelea kunishauri, kunipa moyo na kunisaidia katika kile nilichoamini kuwa ni fanikio langu lijalo. Kwa asilimia kubwa najivunia uwepo wao na kwa kuwa kwa pamoja wote wamekuwa MSAADA MNYOOFU kwangu kwa kuwa na suluhisho lisilohitaji mimi kudhihirisha kitu ili kulifikia. WALIKUWA, WAMEKUWA NA NAAMINI WATAENDELEA KUWA UPANDE WANGU.
Lakini pia nina Dada wadogo ambao nao kwa nafasi waliyokuwa nayo walikuwa chachu saana ya mimi kufanikisha nitakalo. Nakumbuka nikiwa Times Fm kuna wakati ambao "feedback" pekee ambayo ningeipata ni kutoka kwa Kaka na Dada zangu wadogo ambao walijitahidi kunisikiliza kila uchao na kunipongeza ama kunicheka "nilipochemsha" jambo ambalo liliongeza ufanisi kwangu. Kwa hiyo kwa kina Dada Abeella, Byela, Atu, Juliana na wengine (ambao mmeshakuwa Mama Wadogo na mashangazi), nawashukuru, nawapenda na natambua kuwa mmekuwa sehemu kuu ya changamoto zilizonifikisha hapa nilipo.
Kuna Dada zangu wa hiari ambao kiiiila siku nawasiliana nao. Iwe ni kwa kusoma kwenye mitandao yao ama wao kusoma kwangu. Iwe ni kwa kuwasiliana kwenye facebook, messenger, msn ama aina yoyote ya mawasiliani ya kijamii. NAWAPENDA SAANA.
Mmekuwa nguzo muhimu ya kile nionacho kama mafanikio na mmefanikisha kuboreka kwa HIMAYA HII ambayo ni sehemu ya maisha yangu pia. Kwa kina mtabibu wa blog, Dada Subi, Da Yasinta wa Maisha na Mafanikio na Dada "muamshaji" Koero wa Vukani, Da Sophy wa Bambataa, Dada Agnes wa Kiduchu, Da Sarp wa Angalia Bongo, Da Faith wa "Ulimwengu Mdogo", mwanamke wa shoka Da MiJAH, Dadangu Dina wa Marios, Da Edna wa "mchakato wa maisha" (strive for life), Dada Happy Katabazi uwapaye hofu viongozi kwa kalamuyo, Dada Jackline Charles, Dada mpiganaji Judith Wambura, Dada zangu wajasiriamali Marium Yazawa na Shamim wa Zeze, Dada mwenye wito wa mitindo na mavazi Scola wa Passion4fashion, mshairi wa kutazama Upande wa Pili Da Serina, Dada Sophie wa Sophie Club, Da Mary Damian na Da mkubwa Chemi wa Swahili Time. Dada-Rafiki Makrina a.k.a Mama Paul na Da Sarafina Msuya, shukrani kwa uwepo wenu. Dada Annie wa Brizzleleo, Da Maryam, Da Maidama wa TMark, Da Jestina George, Da Jane Siame J2Wisdom, Da Susan wa Karisan Media, Da Mignonne Clara wa Nyumbani Kwetu, Da Rachel Isaac Siwa wa Swahili na Waswahili, Da Rose wa Mbeyela wa Be You na wengine wote.
Kwa kinamama nyooote mliogusa maisha yangu kwa namna yoyote ile, nawapenda na kila siku naona na kudhihirishiwa thamani yenu. Lakini leo kwa kuwa wametenga siku ya kuwaenzi hapa, NAWAOMBEA MAFANIKIO KATIKA KILA JEMA MTENDALO.
Kwa kinamama mlioonesha njia sahihi tangu awali, twawashukuru kwa mwanga mliotuwashia.
Kwa kinamama ambao mnatufunza kuhusu "upande wa pili wa dunia" nanyi pia twashukuru kuwa uwepo wenu watukumbusha kuwa dunia haijajazwa na wale watendao tupendayo tu.
Katika kuadhimisha hili, NAUNGANA NA WANAWAKE, WASICHANA NA WALIMWENGU WOTE KATIKA KUKOMESHA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WASICHANA.
Naungana na Lucky Dube pia katika kuwaombea wanawake kwa MUNGU. Nawaacha na kibao chake GOD BLESS THE WOMEN ambacho mashairi yake yako hapo chini. Sikia anavyowaombea na kuwashukuru. Akiwaita HEROES
HESHIMA KWENU KINAMAMA NYOTE

In the middle of the night I heard her pray so bitterly and so softly yeah...
She prayed for her children
She prayed for their education,
Then she prayed for the man that left her with her children.
We, praise heroes everyday
But there are those that we forget To praise
The women of this world.
They do not run from anything
They stand and fight for what's right
They do not run from anything
They stand and fight for what's right


Chorus
Oh oh oh...
God bless the women

Even when times are so hard
They are so cool, calm and collected.
They do not run from anything,
They stand and fight for what is right
They do not run from responsibilities
They stand and fight for what Is right

Chorus till fade...

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante sana kwa hii heshima tukufu mwenyezi mungu na awabariki wanawake wote na pia akiana baba kwani bila wao hatungekuwepo.

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Ngoja niongee Kiswahili cha Kisukuma

"Sijui kama kuna mtu mwingine anayeweza kuandika hivi unavoandikaga. Sijui inakuchukuaga muda gani kumaliza"

Ni kweli akina mama wanastahili pongezi zao kwani bila wao tusingekuwa na jamii. Sala yako hapo basi na ikajidhihirishe katika kweli. Amen !!!

Anonymous said...

Ubarikiwe Mubelwa! Si jambo jambo dogo kwangu kutajwa kwenye list hiyo. Akina baba wenye akili wanatuwezesha kuendelea mbele zaidi...Heshima kwao!!