Saturday, March 10, 2012

Mawazo ya sauti (I).....OMBI

Mmoja wa marafiki zangu wa Facebook alileta OMBI kuwa nikusanye yale NIWAZAYO KWA SAUTI na kutoa mkusanyo wa kijitabu. Sikuamini kama nimeshawaza vya kutosha kiasi cha kukusanya "kijitabu". Kisha akasema "basi yakusanye na kuyaweka mahala pamoja ambapo tunaweza kuyarejea kwa pamoja".
Nimeona nifanye hivyo hapa, kwani wapo WASOMAJI WANGU WAPENDWA wasio wanachama ama marafiki zangu kulee facebook.
Na haya yafuatayo ni baadhi ya MAWAZO YANGU YA SAUTI ambayo nimekuwa nikiwaza kwenye status zangu za Facebook.
KARIBU


Ndoto na UFUNUO ni matokeo ya matendo yako. Ukiota na usifuatilie ama usione kikitokea utaita ndoto. Ukiamka na kufuatilia kisha ukafanikiwa utaita UFUNUO. Yawezekana kila UFUNUO ni NDOTO ILIYOFANYIWA KAZI hivyo ushauri wangu ni kuwa UKIOTA KILICHO CHEMA, AMKA, NENDA KATENDEE KAZI. Utaifanya kuwa UFUNUO. Hahahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.
Nawaza kwa sauti tuuuu!!!!

Furaha ni "akiba" ya sikitiko lijalo na vivyo hivyo ni kinyume chake. Azaliwapo mtoto furahi ukijua kuwa yeye ama wewe utakufa (hapo mtasikitika) mkiamini kuwa (kama mlitenda wema) mtakutana mbinguni (mkifurahi). Ajaye huondoka na pengine huja tena. Tenda wema ili mwisho wa "mzunguko" huu, uwe mwenye furaha.
Nawaza kwa sauti tuuuuuu!!!!

Ni kwanini twaiita BIMA YA MAISHA ilhali hatuwezi kukusanya mafao yake mpaka baada ya kufa? Ni kweli twastahili kuiita "Life insurance"? Ama ni "post-life insurane" au tuwe wazi kuiita "Death Insurance"? Aaaaah!!
Nawaza kwa sauti tuuuuuu!!!!

PARADOKSI YA JAMII YANGU....Leo hii "nyuma ya kisasa" ni ile yenye game room na gym badala ya study room. Mji wa kisasa ni ule wenye clubs na bars nyingi badala ya Maktaba..... Na bado twasema twataka kujenga jamii bora yenye kuthamini elimu.
Nawaza kwa sauti tuuuu!!!!!

UPDATE: Mpango wa kuwapiku waMarekani, Urusi, Japan na wengineo kwenye mambo ya "space" unaendelea vema. Tunapanga kwenda JUANI na tumegundua kuwa ni lazima tutue kule USIKU. Tuna-calculate take-off time ili tu-land USIKU. Kama kuna volunteer awasiliane nami...
Nawaza kwa sauti tuuuuuu!!!

PARADOKSI YA TANZANIA YANGU: Leo hii tuna wanasiasa ambao wanasema kuipiga vita rushwa ni mpaka wawe kwenye uongozi na uongozi huo hawaupati bila kutoa rushwa. Ina maana wanastahili kutoa rudhwa ili waweze kupata nafasi ya kuipinga rushwa. Swali ni kuwa WATAPINGAJE RUSHWA IKIWA NI LAZIMA WAITUMIE KUFIKA NAFASI ZA KUIPINGA?
Nawaza kwa sauti tuuuuuu!!!!!

Tatizo la kumuelimisha mtu anayedhani "ANAKUZIDI AKILI AMA WEREVU" ni kuwa kadri unapomuelimisha jinsi ulivyo sahihi, yeye anazidi kujidhihirisha kuwa hauna akili hata za kutambua kuwa ana akili kukuzidi.
Hapo sasaaa.
Hatakuelewa mpaka umuelimishe na ukimuelimisha anazidi kuona "ujinga" wako.
Gggggggggrrrrrrrrrrrrr!!!!!!!!!!!!
NAWAZA KWA SAUTI TUUUUUU

NAWAZA KUWA kazi ya mwendesha mashtaka si kusaka sababu za mshitakiwa kutenda alivyotenda, bali kumfanya mshitakiwa kuwa mwanzo na mwisho wa tendo /kosa alilotenda. Kwani wakisaka chanzo cha mtu kutenda makosa si wataishia kutomfunga wanayetaka alale jela? Na kumfunga wanayemtuhumu ni "kipimo cha ubora wa kazi zao"
Mmmmmmhhhhhhhhhhhhh!!!!!!
NAWAZA KWA SAUTI TUUU!!!!!!!!!!!!!

Hivi wajua kuwa UEREVU WA WENGINE WAONEKANA AMA KUSIFIKA KUTOKANA NA UJINGA WAO? Yaani wanaonekana kuwa na akili kwa kuwa hawana akili za kuwaza akili. Wanaonekana watiifu kwa kuwa ni wanafiki na wenye kupendwa na wakubwa wa kazi zao kwa kuwa ni wasaliti.
Labda WANA AKILI KWA KUWA HAWANA AKILI.
Ggggggrrrrrrrrrrrr!!!!!!!
Nawaza kwa sauti tuuuuu!!!!

NIMEFUNZWA kuwa HUWEZI KUMSHINDA ADUI YAKO MPAKA UMPENDE.
OK!!!!! Nililoelewa ni kuwa unastahili kumpenda adui ushindanyaye naye, na ukishampenda ina maana hatakuwa adui kwako na akishakuwa MPENDWA KWAKO, hamtashindana kwa nia mbaya, bali MTASHIRIKIANA.
NAKUBALIANA NAYO....... Wewe je?
Nawaza kwa sauti tuuuu....!!!!!!

Mtu anayetaka kuzuia maendeleo ya mwenzake ni yule anayejitahidi kumfanya mwenzie abaki ktk kiwango cha chini. Tatizo ni kuwa ukitaka abaki, itabidi umshikilie pale. Yaani nawe ubaki ambapo unataka usiyempenda abaki. Hivyo, aliyefanikiwa kuzuia maendeleo ya mwenzake ni yule ambaye naye hataendelea akijaribu kumzuia mwenzake. Ina maana afanikiwaye kumzuia mwenzake anakuwa kajizuia na mwenyewe.
Nawaza kwa sauti tuuu!!

Nimefunzwa kuwa KUONGEA NI KAMA MTIHANI. Kabla ya kuanza una maksi zote lkn uanzapo tu waanza jipunguzia ama kuzilinda. Na UJINGA ni vivyo hivyo, haupo kwa yeyote kama wote watakuwa kimya. Ukianza kuongea waonesha kiasi kilichomo ndani mwako.
Kwa maana nyingine HAKUNA MJINGA kama hakuna asemaye.
CHUNGA USEMACHO KWANI WAJIPIMISHA UJINGA / UEREVU WAKO
Nawaza kwa sauti tuuuuuuuuuuuuuuuu

KUIGA ni kama "bahati". Kwamba kuna "bahati nzuri" na "bahati mbaya". Yaani hata anayesema HAIGI, anaiga kutokuiga. Na pengine kutokufanya upende kuiga ni kuiga waliokataa kuiga. Ina maana hakuna asiyeiga japo yawezekana wapenda uigaji wako zaidi ya wa mwenzako.
Kwa kuwa sote twaiga, basi thamini "igo" lako, hakikisha haliathiri wasiolipenda na endelea KUHESHIMU WAIGAO USIYOIGA
Nawaza kwa sauti tuuuuu!!!!

ISOME, IWAZE NA HATA MAONI TOA KIMOYOMOYO.
WanaHistoria wanasema ilichukua miaka milioni kadhaa kwa nyani kugeuka mtu.
Ok!
Sasa kama miaka iliendelea kuongezeka na nyani waliendelea kuwepo, kwanini hatuoni nyani wapya wakigeuka watu kila miaka yao milioni kadhaa itimiapo tangu wawepo?
Nawaza kwa sauti tuuuuuuuuuuuu!!!!!

"Maisha huku hayafai. Nifanyie dili nije huko."
Nauliza "kisichofaa ni kipi hasa?" najibiwa "hakuna dili kabisa. Kila kitu chapanda bei. Huku sio mahala pa kuishi wala kuendesha maisha"
Nauliza "kwanini vinapanda bei?" najibiwa " wazungu na wachina wanakimbilia huku. Viwanja na nyumba za kukodi zinapanda bei? Wanafungua biashara kila mahali"
Nawaza..Kama hawa wanakuja huko, na wewe unasema hakuna dili, wamefata nini?

OK!!
"Wataalamu" wanasema addiction iliyo kuu ni watu kuwa ONLINE kwa muda mrefu. Na wana ushahidi kwa kuwa wamekuwa wakikaa online kuangalia watu wanavyokaa online na sasa wamehakikisha kuwa hilo ni tatizo. Kwanini wao wasijione ma-addicts pia? Siku hizi wezi wanapata pesa kwa kuwasaka wezi, wala rushwa wanawavumbua wala rushwa na addicts wa PC wanasema wanakaa kuchunguza addicts wa PC.
Nawaza kwa sauti tuuuuuu!!!!!

u-CHANYA wa u-HASI wao.
Atunzaye siri apendwa japo afanya hivyo kwa kuwa HAMUAMINI yeyote.
Asiye tegemezi apendwa japo afanya hivyo kwa kuwa HAAMINI kama kuna wa kumfanyia apendayo.
Aliye jasiri apendwa japo afanya hivyo kwa kuwa HAAMINI kama kuna haja ya kutegemea kwingine.
Apendaye apendwa japo afanya hivyo kwa kuwa HAAMINI kama wengine... watambua THAMANI YA UPENDO
TUPENDE U-HASI KWANI NDIO ULETAO U-CHANYA WETU
Nawaza kwa sauti tuuuuu!!!!

MASWALI MENGINE BWANAAA..
Bosi wangu ananiuliza "ni mara ngapi mawazo yako yame-concentrate 100% ktk kazi?" namwambia SIKUMBUKI.
Ati anakasirika na kuuliza KWANINI?
Namwambia "nikiwaza 100% katika kazi, sina % ya ziada kuwaza kuwa nime-concentrate 100% katika kazi. Na nikishawaza hata kwa 0.001% kuhusu concentration yangu ya kazi, ina maana sina 100% kazini."
Akacheka na kuondoka.
NIKAMUULIZA KIMOYOMOYO...UNANITEGA?

NDIO... Kuna JUU.
Na JUU yaweza kutokuwa ile JUU uliyokuwa ukiiota na kuitamani. Na pengine JUU ya "hadhi" sio ile JUU ya "kipato" ama hata ya "utekelezaji"
NA katika JUU hiyo, bado kuna "kati" na "chini".
BASI USHAURI WANGU NI KUWA....
Kama huko JUU hauko JUU, basi shuka CHINI ili uwe JUU....
Hivi naeleweka????
NAWAZA KWA SAUTI TU!!!

NAWAZA faida za "kinyumenyume"
Yaani HUJUI kuwa ulilala mpaka utakapoamka. Usipoamka....meet you in zion
Hujui USAHIHI mpaka utakapoona MAKOSA.
Huoni MAENDELEO mpaka ujue asiyeendelea ama kisichoendelea kilivyo.
Hutoitambua DHAMBI mpaka ujue upande wa pili wa kile uitacho dhambi.
Kwani unaamini HAKUNA FAIDA ya upande uuitao m'baya ambao kwa "kuukimbia" kunakufanya uonekane "mwema" na "mtakatifu"?
NAWAZA KWA SAUTI TUUUUU!!!

MAFANIKIO
Ni kitu cha ajabu na TATA kwelikweli.... Kwa sababu
-Kila mtu hukiomba japo si kila akiombaye anataka kukitumia kwa wema ama lililo jema
-UFANISI wa wengine ambao wanasema WAMEFANIKIWA ktk watendayo kwaikwaza ama kuiadhibu jamii.
-Ili UFANIKIWE kumkamata ALIYEFANIKIWA kufanya yasiyo mema, ni lazima MAFANIKIO yako yazidi MAFANIKIO yake japo wote mwafanikiwa katika mambo yanayopingana.
NAWAZA KWA SAUTI TUUUUUUU!!!

We (human beings) lives in the world of "delayed-now".There is no such a thing called THIS MOMENT because from the moment you think of it to the time you say it, it's not "THIS moment" anymore. May be "that-this moment". Hahahahahahaaaaaaaaaaa
Just THINKING OUT LOUD!!!!!!

CHOO....Labda ni jina tu kulingana na matumizi, kwani kulingana na uhitaji chaweza kuwa chumba na chumba ama sebule kuwa choo.
NAWAZA KWA SAUTI TUUUU!!!!!!

Labda UONGO ni UKWELI usio sahihi kwa wakati usemwao
NAWAZA KWA SAUTI TUUUUU!!!

1 comment:

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Tatizo ni kwamba inabidi tufikiri mno ili kuelewa unachokisema katika huu uwazaji wako wa sauti... Na wengi wetu hatutaki kufikiri.

Hebu tuwekee udaku bwana ili tutoe maoni....

...> Asante kwa kuyaweka haya maoni pamoja. Nimemaliza kuyachapisha na nitakuwa namung'unya pole pole mpaka nitakapoyamaliza (kama kunamalizika!)