Tuesday, May 15, 2012

Familia...Huishia wapi?

Leo ni siku ya familia duniani. Na SIKU HII IMENIREJESHA KWENYE SWALI LANGU LA MIAKA MICHACHE ILIYOPITA......Familia huishia wapi? Tumezaliwa watano. Nina dada wakubwa waili na Kaka wadogo wawili. Yamaanisha ni mimi niliye kati. Na sina shaka kuwa wengi tutakubali kuwa hii ni familia. Na kama ambavyo nilishasema, nafurahia saana uhusiano tulio nao baina yetu. Lakini pia kuna Baba na Mama. Nao naamini tutawahesabu kama familia. Nao kila mmoja ana ndugu zake waliozaliwa pamoja. Hao kwao ni familia. Ni kwa mamtiki hiyo nahisi kuwa nao ni familia yetu maana ni familia ya sehemu ya familia yetu. Sasa mjomba na Shangazi wote si wana familia katika miji yao? Na hao ni familia za wazazi wetu na sisi na wazazi ni familia. Ina maana nisiwaite familia?
Najiuliza kama sisi sote si familia kwa mwendo huu na kama sivyo, basi basi naendelea kujiuliza kuwa hivi familia huishia wapi? Ama niseme mtu ni ndugu yako mpaka uzazi upi?

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Mimi pia nina shida hii ya kujua familia ni wapi inaanza na wapi inaishia. Huwa mara nyingi nabishana na BBW hapa:- Yeye anasema familia ni watoto yeye na mimi...na mimi nasema HAPANA wao sio ndugu wala familia yangu isipokuwa kaka zangu watano na marehemu mdogo wangu Asifiwe wao ndio FAMILIA YANGU..Je? ipo sahihi hii?

emuthree said...

Familia ni pana ni wewe mwenyewe tu utaamua kuiwekea mipaka,wapi familia yako unataka iishie, wengine kwenye shughuli huigawa familia kwa mtizamo huu:
Familia ya kikeni na familia ya kiumeni, na familia yako wewe mwenyewe kama umeoa na uan watoto, ila wewe upo ndani ya familia ya kiumeni,kitaratibu za kiafrika...
Mfano kama wewe ni mtoto kwenye familia ya baba na mama yako, familia ya kikeni ni ile familia ya mama yako..huko kuna mjomba nk.

Famili ya kiumeni ni ya akina baba zako, napohapo utampata shangazi, ambaye ni dada wa baba zako nk...
Na ndipo hapo nikagundua kuwa shangazi anapatikana kote, kiumeni na kikeni...kwa sisi waafrika au sio,
Na hapo nikajiuliza shangazi yupi mwenye sifa ....maana kila harusi au shughuli wajomba na shangazi ndio wanapewa kipa umbele...