Wednesday, June 27, 2012

Ibada ya kumuaga ndugu yetu Domitian Rutakyamirwa itafanyika Leo Jumatano June 27, 2012 saa 10 jioni (4pm) katika kanisa la 
The Way of the Cross Gospel Ministries. 
3621 Campus Drive, 
College Park. MD. 20705 


Ndg. Domitian aliyekuwa mume wa Dada Bernadetha Kaiza na mkazi wa Washington DC alifariki asubuhi ya Juni 18, 2012 saa mbili na dakika 55 asubuhi (8:55 am) katika hospitali ya George Washington University, Washington DC na atasafirishwa wiki hii kwenda Tanzania kwa mazishi 


Tunapenda kuwashukuru waTanzania wote na jamii zao kwa ushirikiano waliouonyesha katika kipindi chote cha kuuguza, kufariji wafiwa na maandalizi ya kumsafirisha mwenzetu. 
Tunaomba tuzingatie muda katika ibada hii kwani wenzetu wa funeral home wenye kushughulikia mwili, watakuwepo pale kanisani kwa wakati na kwa muda maalum 


 Kwa maelezo zaidi na maelekezo tafadhali wasiliana na: 
Idd Sandali (Rais wa Jumuiya ya waTanzania DMV) 301-613-5165 
 Henry Kente: 240-938-2452 
 Bernadetha Kaiza: 240-704-5891 
 Marmetha (Mimi) Kente 301-693-4550 
 Mubelwa Bandio: 240-281-0574

No comments: