Kama ambavyo tuliwaarifu hapo awali, Shirika la
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kupitia mpango wake wa WESTADI ulithibitisha
kugharamia mwili wa Ndugu yetu Domitian Rutakyamirwa pamoja na mwanafamilia
mmoja atakayesindikiza mwili, hivyo harambee ya kuchangia gharama za kusafirisha
mwili wake iliyokuwa imepangwa kufanyika hii leo haitafanyika tena.
Ibada ya kumuaga itafanyika siku ya Jumatano saa KUMI JIONI katika
kanisa la
The Way of the Cross Gospel Ministries.
3621
Campus Drive,
College Park. MD. 20705
College Park. MD. 20705
Ndg. Domitian aliyekuwa
mume wa Dada Bernadetha Kaiza na mkazi wa Washington DC alifariki asubuhi ya
Juni 18, 2012 saa mbili na dakika 55 asubuhi (8:55 am) katika hospitali ya
George Washington University, Washington DC.
Msiba
upo nyumbani kwa familia ya Mr & Mrs Deo Mosha.
Anwani
ni:
4402 Hatties Progress Dr,
Bowie, MD. 20720
Kwa
maelezo zaidi na maelekezo tafadhali wasiliana na:
Idd Sandali (Rais wa Jumuiya ya waTanzania DMV)
301-613-5165
Henry Kente: 240-938-2452
Bernadetha Kaiza: 240-704-5891
Marmetha (Mimi) Kente 301-693-4550
Mubelwa Bandio: 240-281-0574
No comments:
Post a Comment