Saturday, June 23, 2012

Tanzania yangu.... NA UDHAIFU WA KUKIRI UDHAIFU WAKE


"Mtu kuitwa DHAIFU,MJINGA, MPUNBAVU wala sio kutotii mamlaka. Ni kueleza mtu alivyo. Na haya sio matusi,ni HADHI ya mtu kulingana na na atendayo.
Kama anavyoweza kuwa SHUJAA. Kwa hiyo, ukitenda jambo jua unajipa hadhi. Na usitegemee kufanya UJINGA halafu uitwe SHUJAA kwa tafsiri ya "muitaji" Kwa nyakati tofauti mtu hupitia HADHI zote hizi, na NI UJINGA, UPUMBAVU NA UDHAIFU KUJIAMINISHA KUWA RAIS HAWEZI KUWA MJINGA, MPUMBAVU NA DHAIFU kwani kilicho ndani mwa rais, ndicho kilicho kwa binadamu yeyote..........UBINADAMU. Ambao.....ukamilifu wake ni kutokamilika. Napayuka kimyakimya tuuuuuuuuu!!!!!!!!!"

Ndivyo nilivyoandika kwenye ukurasa wangu wa FACEBOOK. Hii ilitokana na kile kilichotokea wiki hii ambapo Mbunge wa Ubingo kwa tiketi ya CHADEMA Mhe. John Mnyika alitolewa nje ya bunge kwa kukataa kufuta kauli yake kuhusu UDHAIFU WA RAIS.

Nadhani kumtoa Mhe. Mnyika bungeni kwa kugoma kufuta neno UDHAIFU WA RAIS lilikuwa jambo la kiDHAIFU sana kwa Naibu Spika. Na pengine nilitaraji kusikia wabunge wengine wakitaka kujadili UDHAIFU uliojitokeza katika kukabiliana na UDHAIFU alioelezwa kuwa nao Kaka John Mnyika alipoelezea UDHAIFU wa rais wetu.
Kwani Rais ni nani asiwe Dhaifu? Na ni kiongozi gani wa mamlaka ya kutunga sheria asiyempa mtu nafasi ya kufafanua analosema? Huu ni UOGA unaotufanya tuwe DHAIFU kukiri UDHAIFU wetu utuleteao UDHAIFU kwenye nchi yetu DHAIFU.

Rais kama binadamu yeyote anaweza kuanguka katika mambo yote manne.
Kujua kuwa anajua. 
Kujua kuwa hajui. 
Kutojua kuwa anajua na 
Kutojua kuwa hajui. 

Kwa maana nyingine, Rais kama binadamu mwingine anaweza kuwa KATIKA NGAZI ZOTE ZA UFAHAMU, KUANZIA MWEREVU MPAKA MPUMBAVU.

Ni ujinga kumfanya mtu kuwa kama Mungu na ni udhaifu mkubwa kujua fika kuwa binadamu si Mungu na bado ukampa hadhi asiyostahili. Bunge ni chombo kikubwa nchini na umakini wa kukiendesha unahitajika. Niliwahi kuandika post isomekayo Ujinga mkuu ni kuwa MJINGA WA UJINGA WAKO ambamo niliandika "Hakuna ubishi kuwa kati ya vitu ambavyo hatutaki kujifunza, ama niseme kati ya vitu ambavyo ni "DONDA NDUGU" nchini Tanzania, basi ni KUTOJIFUNZA KUTOKANA NA MAKOSA TULIYOFANYA. Naamini kuwa ufanisi wa BUNGE na SERIKALI ya Tanzania UNADIDIMIZWA na mambo mengi ikiwemo KUTOANDALIWA KWA WATAWALA / VIONGOZI TULIONAO. Labda hata kina Mwl Nyerere hawakuandaliwa lakini walikuwa na kipaji na hata moyo na nia ya kuongoza na walikuwawaadilifu. Tumeona namna ambavyo watu wasio na ujuzi katika SAYANSI YA SIASA, UONGOZI na hata KIPAJI CHA UONGOZI wakijiwezesha kupata nafasi na kisha kuchaguliwa kuchukua nafasi mbalimbali na hasa za UUNGE nchini mwetu, lakini kibaya zaidi ni kuwa watu hao hao wanateuliwa kushika nyadhifa kubwa ndani ya nchi yetu bila ya kuwa na kile kinachoaminika kuwa utoshelezi a nafasi wazikwaazo. Kwa maneno mengine ni kuwa HAWAANDALIWI."

Labda wabunge wa sasa na hasa Naibu Spika hawafunzwi kuwatumikia wananchi wa Tanzania kwa kumuacha Mhe. Mnyika awafafanulie waTanzania ni kipi alimaanisha alipogusia suala la UDHAIFU WA RAIS na kwa kuwa BINADAMU KAMILI NI YULE ASIYEKAMILIKA, basi yawezekana hata rais angweza kujifunza kitu kuhusu udhaifu wake na / hata kujifunza kuhusu watu wasivyomuelewa kuhusiana na udhaifu anaodhaniwa kuwa nao.
Kwa maana nyingine, Mhe. Naibu Spika amekuwa kikwazo cha rais kupiga hatua katika kutambua fikra za wananchi wake.

NAWAZA.............. Huyu angekuwa nchini kwetu AKASEMA UDHAIFU WA RAIS namna hii si angefukluzwa nchini?


Tanzania Yangu ni kipengele kinachozungumzia ytale yaendeleayo nchini Tanzania na namna ambavyo "ndivyo sivyo" inavyozidi kupamba moto nchini. Kwa matoleo yaliyotangulia BOFYA HAPA


Tuonane "Next Ijayo"

No comments: