Tunapenda kuwapa taarifa za maendeleo ya mipango ya mazishi ya ndugu yetu Domitian Rutakyamirwa. Mpaka hii leo michango inaendelea lakini bado tuko nyuma. Gharama zinazohitajika ni takriban dola za kiMarekani 15,000.
Kulingana na mahitaji ya fedha na muda mfupi tulionao, tutaanza harambee siku ya Ijumaa (June 22) saa mbili usiku. Harambee hii itafanyika ulipo msiba, nyumbani kwa familia ya Mr & Mrs Deo Mosha.
Anwani ni:
4402 Hatties Progress Dr,
Bowie, MD. 20720
Kama ilivyo desturi yetu, tunaomba ushirikiano wenu katika kufanikisha hili
Kwa wale walio nje ya Washington DC Metro, mnaweza kuchangia kwa akaunti iliyofunguliwa kuwezesha hili.
Akaunti hiyo imefunguliwa katika Bank of America.
Jina KAIZA DOMITIAN CARE AND SUPPORT.
Routing.. 052001633
Account.. 446026881993.
ANWANI:
3344 6th St SE,
Washington DC 20032.
Kwa maelezo zaidi na maelekezo tafadhali wasiliana na:
Idd Sandali (Rais wa Jumuiya ya waTanzania DMV) 301-613-5165
Henry Kente: 240-938-2452
Bernadetha Kaiza: 240-704-5891
Marmetha (Mimi) Kente 301-693-4550
Mubelwa Bandio: 240-281-0574
Kama kawaida yetu, tunaomba kinakaka kuja na vinywaji na kinadada kuleta vyakula.
Msiba huu ni wetu sote, UMOJA, MSHIKAMANO NA USHIRIKIANO WETU, ndio utakaowezesha kusafirisha mwili wa ndugu, rafiki, Jamaa, na mTanzania mwenzetu Domitian kwenda nyumbani Tanzania kwa mazishi.
SISI TULIMPENDA DOMITIAN LAKINI MWENYEZI AMEMPENDA ZAIDI. JINA LAKE LIHIMIDIWE.
No comments:
Post a Comment