Monday, June 18, 2012

MSIBA WASHINGTON DC METRO


Tunasikitika kutangaza msiba wa ndugu yetu Domitian Rutakyamirwa (pichani) aliyefariki leo asubuhi Juni 18, 2012 saa mbili na dakika 55 asubuhi (8:55 am) katika hospitali ya George Washington University, Washington DC.

Marehemu Domi (kama anavyofahamika kwa wengi) ni mume wa Dada Bernadetha Kaiza na wote walikuwa wakiishi Washington DC.

Msiba upo nyumbani kwa familia ya Mr & Mrs Deo Mosha.
Anwani ni:
4402 Hatties Progress Dr, 
Bowie, MD. 20720 
Mipango ya kuusafirisha mwili wa marehemu Domitian kwenda Tanzania inaanza na kama ilivyo desturi yetu, tunaomba ushirikiano wenu katika kufanikisha hili
Kwa maelezo zaidi na maelekezo tafadhali wasiliana na:
Idd Sandali (Rais wa Jumuiya ya waTanzania DMV) 301-613-5165 
Henry Kente: 240-938-2452 
Bernadetha Kaiza: 240-704-5891 
Marmetha (Mimi) Kente 301-693-4550 
Mubelwa Bandio: 240-281-0574 

Kwa wale walio nje ya Washington DC Metro, mnaweza kuchangia kwa akaunti iliyofunguliwa kuwezesha hili.
Akaunti hiyo imefunguliwa katika Bank of America.
Jina KAIZA DOMITIAN CARE AND SUPPORT. 
Routing.. 052001633 
Account.. 446026881993.
ANWANI: 
3344 6th St SE,
Washington DC 20032.

Tutazidi kuwataarifu juu ya maendeleo ya msiba huu zikiwemo gharama na hatua za kumsafirisha marehemu kuelekea nyumbani Tanzania kwa mazishi.
Raha ya milele umpe ee bwana na mwanga wa milele umuangazie.
Mungu aibariki na kuilinda familia ya Ndg. Domitian Rutakyamirwa, awape faraja na kuwatia nguvu katika kipindi hiki kigumu.

 Bwana ametoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Sisi tulimpenda lakini Mungu amempenda zaidi. Astarehe kwa amani.