Wednesday, October 24, 2012

"Kunya anye kuku. Akinya bata......."

Photo Credits LUBP
Septemba 10, 2009 niliandika "bandiko" lenye kichwa kisemacho Unamlaumu Kanumba???? Kwani alimuwakilisha naniiiii???.
Na hiyo ilitokana na LAWAMA NA KASHFA alizopokea Kanumba baada ya kualikwa na kushiriki katika jumba la Big Brother Afrika.
Katika bandiko hilo, niliandika
"Huko alionekana na kuongea na baada ya hapo, watu wamesema meeengi kuhusu yeye (na mimi nilikuwa mmoja wao "waliochonga") lakini baadae nilipoendelea kufuatilia mjadala huu hapa nikawaza. HIVI KANUMBA ALIMUWAKILISHA NANI???
Aliwakilisha kundi la wasomi wachache waTanzania ama kundi la walio wengi wenye elimu ya kati (tena iliyo katika mfumo m'bovu wa kikoloni"?)
Waliomponda wengi wao ni wale "waliosoma" ama wale wanaoishi nje ya nchi ambao nina hakika kuwa hawako kundi moja na Kanumba.
Kanumba alimuwakilisha kijana halisi wa kitanzania ambaye amekulia mazingira ya kusota na kujiwekezea katika juhudi za kazi (na kashfa kiasi) kukuza jina lake. Na kwa hakika kama hili kundi ndilo ambalo Kanumba anapatikana basi tujiulize ushiriki wake kulingana na hawa "wenzake".
Si la wale ambao kwa mihangaiko yao ama ya wawawezeshao (usisahau ufisadi) wameweza kwenda kusoma na kujua "this and that".
(Kanumba) Ni mwakilishi wa kundi letu sisi ambao serikali imetusahau na kutojishughulisha nasi kisha inataka kuja kujivunia sifa za wachache wetu wanaobahatika kufanikiwa.
Si unaijua tena Tanzania yangu. Ivunayo isipopanda (bofya)
Kama Kanumba anawakilisha mamilioni ya vijana wa kiTanzania ambao wana elimu kama yake, unadhani unaweza kumuweka na vijana wanapi ambao wataweza kukaa nyuma ya Camera na kuongea kama alivyoongea???........
Na pengine kwa mazingira aliyosomea, kukulia na hata afanyiayo kazi, tulitaraji Kanumba awe na kingereza cha kiwango gani??
Mbona tupo wengi wenye kiwango hicho na tunawaona wengi hata nchi za nje (kama hapa Marekani) ambao wametoka kwao (mfano waMexico) na kuishi hapa miongo kadhaa na bado hawezi kuunganisha sentensi? Ni kweli kuwa Kanumba kafanya vibaya namna hiyo na si kwamba kuna sababu ya ziada kumshambulia? DaMdogo Candy katika "ulimwengu wake mdogo" ameuliza kwanini watu wengine wako hivi?? (Bofya hapa kumsoma) na japo ilikuwa kabla hili "halijalipuka", lakini ni "walewale" kina sie aliokuwa akijiuliza.
Kanumba alifanya alivyofanya na ni kwa "nguvu zake mwenyewe" bila msaada wa ziada.
Labda angeweza kufanya vema zaidi kama angepitia njia njema zaidi lakini hakupitia.
Na si yeye tu apitiaye alikopitia, bali ni wengi tunaopitishwa huko."
SASA HUYO NI MAREHEMU KANUMBA.
Hivi karibuni, NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA UFUNDI wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Philipo Augustino Mulugo akifanya "presentation" nchini Afrika Kusini ambako kwa hakika tunajikuta tukiwaza mengi kuhusu UWAKILISHI WETU KWENYE MAJUKWAA YA KIMATAIFA.
Maswali yanakuwa mengi.
1: Ni nani aliandaa presentation hiyo?
2: Ni nani aliihariri (if any) na kuhakikisha "inatiririka" ipasavyo?
3: Iliandaliwa kwa anayeifahamu ama asiyeifahamu Tanzania?
4: Ni kweli kuwa waliohudhuria waliaminishwa kuwa yule ndiye mtu sahihi zaidi kueleza waelezwacho?
5: Yalifanyika mazoezi ya ku-present hilo?
TAZAMA KISHA FIKIRIA kuhusu "JUKWAA" alilokuwepo Marehemu Kanumba (Big Brother Africa) na hili alilokuwepo Mhe. Naibu Waziri wa Elimu (The Innovation Africa Summit) na kisha ufikirie ni nani aliyekuwa palipostahili umakini wa kunena wanenayo? Maelezo kamili ya video hii yanasema "Hon. Philipo Augustino Mulugo -- Deputy Minister of Education and Vocational Training, Tanzania, speaking on Education for Employment, Developing Skills for Vocation at the Innovation Africa Summit - 5th-7th October 2012 at the Westin Hotel, Cape Town, South Africa. Supported by the Government of South Africa and co-hosted by AfricanBrains and the University of the Western Cape."
Angalia
 (i) Presentation yenyewe,
(ii) Usahihi wa taarifa hiyo
(iii) Uwasilishwaji wake
KARIBU

1 comment:

emuthree said...

Mimi hapo sitii neno, nawazia tu, mfano angesimama Mrusi, akazungumza kiingereza chake cha Kirusi,...na wenzetu hawa, walikuwa hawababaishwi na lugha za kigeni, anakimwanga kirusi cha kwao, kama walivyo Wachina na Wajerumani....

Kwasababu labda ni ngozi nyeupe,yeye hatutaona kuwa hajasoma, kwa vile hajui kiingereza kila cha buli buli!

Nazidi kuwaza hivi mtoto wa Kiingereza ambaye anajua kingereza darasa la kwanza, sijui huko kwao wana madarasa kama haya, akasimama hapo nakuongea kiingereza maana ni lugha yake , ataongea kiingereza vizuri, huyo tutamuita kasoma hadi chuo kikuu au sio? Kwa vile anajua kiingereza kizuri au sio, basi kasoma saana, Eti?

Ni nawaza tu mkuu, labda nipo nje ya mada!